Kazi za Kitaaluma Kugawiwa kwa Fadhila! Tumekwisha

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,707
71,017
Kuna kazi ambazo huwezi mpa mtu hata kama unampenda sana kama hana taaluma hiyo.
Hatuwezi kumpa Pasco wa JF ukuu wa kitengo cha upasuaji MOI kwa kufurahishwa na michango yake JF. Wala Mbwana Samatta kuwa Katibu Tawala Simiyu kwa vile ni mcheza mpira mahiri.
Nimesikia orodha ya ma DAS imetoka na wengi ni vijana watumikaji kisiasa bila utaalamu.
Kwa wanao fahamu, kazi ya DAS (Katibu Tawala Wilaya) sio ya kisiasa wala ya blabla na watendaji wa kazi hiyo walikuwa wanaandaliwa rasmi toka zamani katika chuo chetu cha Mzumbe.
Ni kazi ya kiutawala inayosimamia sheria na taratibu za utumishi ndani ya wilaya. Huyu ndio mtaalamu wa kumuongoza mtawala wa siasa (DC) asiende harijojo.
Sasa orodha iliyotoka ETI hata watu wenye weledi mdogo kama Mtela Mwampamba wamepewa u DAS sio tuu ni kichekesho bali ni matusi kwa hiyo wilaya aliyopelekwa.
DAS,RAS au Katibu mkuu wa wizara akiwa bogus ni maafa katika sehemu hiyo.
Sio wivu kama watu wenye akili nyepesi watakavyo fikiri bali tujiulize Taifa hili tunalipeleka wapi? Hakika kwa mwendo huu ndani ya miaka 3 tutakuwa watu wa migogoro itayo hitaji msaada wa nje.
 
Ifike mahali DAS iwe ni kama kazi zngne znavyopatikana, kazi ztangazwe watu waombe wafanyiwe interview ya nguvu ndo wapate kazi hzo, sio kuchaguana.
Mbona IPO katika standing orders hiyo mkuu! Namna gani ya kumpata mtumishi huyo. Huyo ni mtumishi wa kudumu sio wa kuingia na kutumbua kama kina Polepole ambao Leo ni DC kesho akinuniana na Makonda unamtumbua.
 
Kuna kazi ambazo huwezi mpa mtu hata kama unampenda sana kama hana taaluma hiyo.
Hatuwezi kumpa Pasco wa JF ukuu wa kitengo cha upasuaji MOI kwa kufurahishwa na michango yake JF. Wala Mbwana Samatta kuwa Katibu Tawala Simiyu kwa vile ni mcheza mpira mahiri.
Nimesikia orodha ya ma DAS imetoka na wengi ni vijana watumikaji kisiasa bila utaalamu.
Kwa wanao fahamu, kazi ya DAS (Katibu Tawala Wilaya) sio ya kisiasa wala ya blabla na watendaji wa kazi hiyo walikuwa wanaandaliwa rasmi toka zamani katika chuo chetu cha Mzumbe.
Ni kazi ya kiutawala inayosimamia sheria na taratibu za utumishi ndani ya wilaya. Huyu ndio mtaalamu wa kumuongoza mtawala wa siasa (DC) asiende harijojo.
Sasa orodha iliyotoka ETI hata watu wenye weledi mdogo kama Mtela Mwampamba wamepewa u DAS sio tuu ni kichekesho bali ni matusi kwa hiyo wilaya aliyopelekwa.
DAS,RAS au Katibu mkuu wa wizara akiwa bogus ni maafa katika sehemu hiyo.
Sio wivu kama watu wenye akili nyepesi watakavyo fikiri bali tujiulize Taifa hili tunalipeleka wapi? Hakika kwa mwendo huu ndani ya miaka 3 tutakuwa watu wa migogoro itayo hitaji msaada wa nje.
Umesema kweli mkuu, nimeona jina la dogo Abubakar Asenga!!!! Nimebaki kushangaa DAS ñi taaluma si kazi ya kisiasa naona mvurugano mkubwa unakuja huko mbele ngoja tusubiri tuone kitakachotokea
 
inshort kuchanganya civil service na siasa ni kuharibu working machinery of the state. hili jambo halipaswi kuungwa mkono bila kuangalia tofauti zetu.
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom