Bob Lee Swagger
JF-Expert Member
- Oct 21, 2011
- 1,362
- 515
Mimi nadhani ni wakati wetu sisi wananchi kujifunza badala ya kuendelea kulaumu maana Kilichotokea ACT ni uamsho juu ya madaraka na kutenganisha Uongozi wa Chama kama chombo kinachosimamia wanachama na uongozi wa nchi unaowakilisha watu wote bila kujali matabaka yao.
ACT kuwa na cheo cha Kiongozi ndio mpango mzima japo tumeona Zitto kapewa majukumu makubwa zaidi na hii inatokana na mazoea yetu sisi wote maana JK ni Kiongozi na Mwenyekiti wa CCM, Mbowe ni Mwenyekiti na kiongozi wa Chadema, Lipumba ni Mwenyekit na Kiongozi wa CUF, vivyo hivyo vyama vyote vya siasa nchi kila kiongozi amechukua majukumu mengi na makubwa kuendesha chama na kutangaza itikadi na sera za chama kwa wananchi, matokeo yake kumekuwa na vurugu kubwa juu ya nani sauti ya chama.
nakumbuka wakati fulani nilikutana na Marafiki wa Slaa nikataka kushauri mabadiliko ktk uongozi kuwepo na viongozi wa chama na viongozi wa Kitaifa nikaona watu wenyewe hatuelewani nikameza maneno yangu maana niliuliza tu kwa nini muwe wafuasi marafiki wa Slaa lakini sio wafuasi wa Chadema? wakajibu wao wanakubaliana na vision ya Dr.Slaa tu...Jibu zuri kabisa lakini hawakuelewa undani wake.
Hivyo iwe mwanzo mzuri kwetu na vyama kujitambua kwamba hakuna sababu ya kujirundikia madaraka maana inakupa majukumu mengi mtu mmoja kupita kiasi. Hili ndilo tatizo letu na tujifunze na nina hakka ACT watarekebisha majukumu baina ya Kiongozi na Mwenyekiti kulingana na muundo huu lakini ukweli ni kwamba hivi ndivyo inavyotakiwa. Na vyama vinginevyo wafuatie maana hii ndio demokrasia.
Kwahiyo inamaana kuwa hayo madaraka aliyonayo supreme leader zzk sio mengi na makubwa?! au unadhan hicho kilichoandikwa kwenye katiba ni madaraka madogo?!
Watanzania bana unaandika kitu na kukisahau hapo hapo!