Kazi za CAG ni zipi?

Aug 10, 2011
81
9
kila mara tunaposikia kuna tatizo la rushwa au ubadhilifu wa fedha za umma mara nyingi nimekuwa nikisikia Ofsi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali inafanya uchunguzi..

Kutokana na sakata la Jairo mie nimeelewa tofauti kumbe kazi ya CAG ni kukagua matumizi ya pesa zilizotoka bila kujali matumizi yake! kama bajeti 1 ya wizara inapitishwa kwa milioni 500 na hilo linaonekana ni jambo la kawaida sasa hii ofsi inasaidia nini?

Je tuna wizara ngapi nchi hii ambazo zinapitishwa kwa mamilioni ya shillingi? Kweli serikali yetu iko serious katika kuleta mabadiliko kwa ajili ya watanzania? sipati majibu labda wadau tusaidiane kazi za CAG na lengo lake hasa nini? na ina msaada gani kwa ajili ya kulinda ufujaji wa mali za umma?
 
Haiingii akilin kwa mkaguzi mkuu koshindwa kuona '' disciplinary offence katika jambo lililowazi ambalo mamlaka yalimnyima kauli mtoto wa mkulima kufanya maamuzi sahihi.

Napendekeza aliyesimamia na kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma hizi na aliykubali kutangaza matokeo haya wote wakapimwe kama kwa kipindi hiki wako sawasawa. Jamani mbona hii ni haibu sana wapendwa.
 
Hivi huyu tunaemuita CAG kwa maana ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali,ni kweli anakagua na kudhibiti au anakagua tu?

Kwa maneno mengine,kama sheria inamruhusu kukagua na kisha kutoa mapendeze yake tu,nini sasa anachodhibiti hapa?

Nafikiri jina sahihi kutokana na hali halisi iliyopo,huyu CAG wa sasa anastahili kuitwa "Auditor General" tu wa serikali na si huku kumvika "kilemba cha ukoka" kama ilivyo sasa.
 
Nchi hii taasisi nyingi ni kama mbwa asie na meno, CAG, TAKUKURU, SSRA, TCRA na vingine vingi sioni kazi yake zaidi vinaundwa kisiasa kupeana ajira tu, maamuzi yote yako serikalini.
 
Hivi huyu tunaemuita CAG kwa maana ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali,ni kweli anakagua na kudhibiti au anakagua tu?

Kwa maneno mengine,kama sheria inamruhusu kukagua na kisha kutoa mapendeze yake tu,nini sasa anachodhibiti hapa?

Nafikiri jina sahihi kutokana na hali halisi iliyopo,huyu CAG wa sasa anastahili kuitwa "Auditor General" tu wa serikali na si huku kumvika "kilemba cha ukoka" kama ilivyo sasa.
Nakubaliana na wewe Mkuu. Kazi ya kudhibiti kwa kweli haionekani. Inaweza kuna ni jina la cheo tu. Taasisi anayoiongoza inaitwa "National Audit Office".
 
Tukiwa Mwanza katika kikao cha kutoa maoni ya katiba mpya tulikubaliana kuwa CAG abaki kuwa Auditor General tu.hili kwenye katiba mpya halikuzingatiwa.Wenzetu AFRO-SAI wamejitoa katika Controlership.
 
Hivi huyu tunaemuita CAG kwa maana ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali,ni kweli anakagua na kudhibiti au anakagua tu?

Kwa maneno mengine,kama sheria inamruhusu kukagua na kisha kutoa mapendeze yake tu,nini sasa anachodhibiti hapa?

Nafikiri jina sahihi kutokana na hali halisi iliyopo,huyu CAG wa sasa anastahili kuitwa "Auditor General" tu wa serikali na si huku kumvika "kilemba cha ukoka" kama ilivyo sasa.

Angeweza kuwa Controller kama angekuwa 99% or 100% Independent.Na kwa hali ilvyo alitakiwa kuwa Mdhibiti na Mkaguzi wa fedha za serikali na mashirika ya Umma.Na pia anayohaki ya kufanya Audit kwenye makampuni na mashirika ya nje.

Cha kujiuliza UHURU anao?Je tunafuata misingi na sheria za utawala bora uliotukuka?Nchi nyingi za kiafrika watendaji wanawaogopa sana wanasiasa hasa walioko kwenye UTAWALA.

Huyu CAG kama akiteuliwa Rais na Bunge likafanya blessing then hata Mahesabu yake yangekuwa yanatoka kwa CAG na kwenda moja kwa moja bungeni.

Kaka Salaryslip jiulize swali dogo tu wakati ukisubiri majibu ya kuudhi toka kwetu............

Bunge letu liko HURU?Wabunge?Maspika na wenyeviti wa Bunge je?

Ukipata majibu basi hata swali lako la CAG utapata jibu zuri japo la kuudhi.
 
Tukiwa Mwanza katika kikao cha kutoa maoni ya katiba mpya tulikubaliana kuwa CAG abaki kuwa Auditor General tu.hili kwenye katiba mpya halikuzingatiwa.Wenzetu AFRO-SAI wamejitoa katika Controlership.

Asante sana kwa taarifa hii.Nimegundua kumbe ni mtazamo wa wengi tu.
 
Siku zote namwita auditor general......anakagua ccm wao wanaiba.......
 
CAG anatakiwa kudhibiti kwanza kabla ya kukagua. Hivyo anavyoripoti udhaifu kwenye matumizi ya fedha za umma kwa kiasi kikubwa na yeye anahusika kwa kushindwa kuweka na kusimamia mifumo thabiti ya kudhibiti matumizi mabaya ya pesa za umma.
 
Angeweza kuwa Controller kama angekuwa 99% or 100% Independent.Na kwa hali ilvyo alitakiwa kuwa Mdhibiti na Mkaguzi wa fedha za serikali na mashirika ya Umma.Na pia anayohaki ya kufanya Audit kwenye makampuni na mashirika ya nje.

Cha kujiuliza UHURU anao?Je tunafuata misingi na sheria za utawala bora uliotukuka?Nchi nyingi za kiafrika watendaji wanawaogopa sana wanasiasa hasa walioko kwenye UTAWALA.

Huyu CAG kama akiteuliwa Rais na Bunge likafanya blessing then hata Mahesabu yake yangekuwa yanatoka kwa CAG na kwenda moja kwa moja bungeni.

Kaka Salaryslip jiulize swali dogo tu wakati ukisubiri majibu ya kuudhi toka kwetu............

Bunge letu liko HURU?Wabunge?Maspika na wenyeviti wa Bunge je?

Ukipata majibu basi hata swali lako la CAG utapata jibu zuri japo la kuudhi.
Nafikiri swala la udhibiti halina uhusiano na uhuru. Hawezi kudhibiti kwa sababu anakagua baada ya kuwa fedha zimeshatumika. Angekuwa anakagua kabla malipo hayajafanyika basi angeweza kudhibiti. Kwa hiyo ofisi hiyo ni bora ikaitwa AuG yani Auditor General
 
Kudhibiti inawezekana kama maana halisi ya controler ni kumanage fedha za serikali na umma zitumike kama ilivyopangwa.Na hii ni pamoja na kujaribu kucontrol over pricing ya vifaa na miradi.
 
Back
Top Bottom