Kazi ya wabunge wa tanzania

tata mura

JF-Expert Member
Sep 27, 2012
275
49
Nawapongeza Wabunge wote, wawe wa kuchaguliwa/ kuteuliwa kwa kazi yao nzuri waifanyayo wawapo bungeni. Hivi ni kweli hakuna majukumu mengine yawahusuyo wabunge wetu nje ya Bunge hususani ya kijamii?. Walio wengi nawasikia majukwaani wakijitahidi kuosha majina yao, kwa itikadi ya Vyama vyao kwa mtindo wa makombola.

Mimi nafikiri kuna wajibu wa kuwaomba Wabunge wetu baada ya kupewa uraji na wananchi waelezee walichokifanya ndani ya jimbo lake. Mfano mzuri ni mh. MB. Tundu Lisu kwa maneno yake unaweza fikiri kweli kiongozi ni huyu! lakini fika kwenye jimbo lake hakuna hata dalili ya maendeleo. Mimi nilifanikiwa kupita pale nikasimuliwa kisa kimoja ambacho sikuamini masikio yangu na kughubikwa na sitofahamu nyingi, hivi kweli kwa mtu anayeongoza watu anaweza kuzuia jamii anayo iongoza kutopokea msaada wa kimaendeleo bila njia mubadala? kuna Company moja ili wachimbia kisima wananchi baada ya kuona wana shida ya maji kiongozi makini na mwona mbali aliwashawishi wananchi wakifukie kwa mawe na kweli wakafanya hivyo bila kujua madhara yake. Na sasa nasikia huko wanataabika sana wananchi kwa shida ya maji, Tundu yeye haonekani tena anatanua kwa zilizopo chini ya kapeti nasikia uchaguzi ujao anajipanga kugombea Singida mjini sijui huku aliko kuhalibu anamwachia nani. Yapo mengi nikiyaweka hapa wagumu wa kuelewa watafikili namwalibia cv yake. Kwa anayebisha atembelee jimboni kwake ajione, najua wapo wengi Wabunge wastaili kama hii, lakini hili ni kosa letu la kumwamini kiongozi kupita kiasi yaani hata akikwambi andamana juu ya kwa nini uende chooni baada ya mlo kwa usiye fikilia utaandamana na kunyenyua bango juu.


Bora kusadiki kuliko kufikilika
 
Back
Top Bottom