Kazi ya uopoaji maiti 30 mgodini bado imekwama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kazi ya uopoaji maiti 30 mgodini bado imekwama

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Mar 30, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,403
  Likes Received: 81,429
  Trophy Points: 280
  Kazi ya uopoaji maiti 30 mgodini bado imekwama

  Imeandikwa na David Azaria, Geita; Tarehe: 30th March 2009 @ 20:22

  HabariLeo

  Kazi ya uopoaji miili zaidi ya 30 ya watu waliofukiwa ndani ya mgodi wa dhahabu wilayani hapa, ikihusisha wataalamu wa uokoaji wakiongozwa na wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) imekwama. Zaidi ya watu 30 wanahofiwa kufa baada ya kufukiwa ndani ya mgodi wa kijiji cha Mgusu kata ya Mtakuja wilayani hapa, katika moja ya mashimo ya dhahabu ambayo yanamilikiwa na kampuni ya uchimbaji ya Shanta Mine. Hadi jana saa 9 alasiri uopoaji wa miili hiyo ulikuwa haujaanza kutokana na wataalamu wa uokoaji na wa mgodi wa Geita kuangalia namna ya kupandisha vifaa vya uokoaji mlimani liliko shimo hilo.

  Hata hivyo tayari vijana wapatao 40 tayari walikuwa wameandaliwa kuingia ndani ya mashimo kwa ajili ya uopoaji, huku Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ikiwa imepiga kambi eneo la tukio. Akizungumza jana na wananchi wa kijiji hicho katika eneo la tukio, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. James Msekela, alisema uongozi wa serikali ya Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, imekubaliana na uongozi wa mgodi wa Geita kufanya kazi ya uopoaji.

  “Jamani tayari tumepata ufumbuzi wa suala hili, tumekubaliana na wenzetu wa mgodi wa Geita watusaidie katika uopoaji wa wenzetu waliofukiwa kama watakuwa hai itakuwa ni jambo la kumshukuru Mungu, lakini kama tayari watakuwa wamepoteza maisha basi angalau tupate miili yao na kuifanyia mazishi kwa heshima zote kwa sababu ni watoto na ndugu zetu,” alisema Dk. Msekela.

  Tukio hilo lilitokea juzi saa 12 asubuhi, baada ya zaidi ya wachimbaji 30 waliokuwa wamekesha ndani ya shimo hilo wakichimba dhahabu, kufukiwa na udongo kutokana na shimo kuporomoka. Mara baada ya kufukiwa, mvua kubwa ilinyesha na kusababisha maji kujaa katika shimo hilo ambalo linadaiwa kuwa na kina cha meta 100.

  Akisimulia tukio hilo mmoja wa walionusurika ambaye alizungumza na wachimbaji wenzake sekunde chache kabla ya shimo kuporomoka, Charles Suleiman (28), alidai kuwa usiku huo saa saba usiku aliugua ghafla na hivyo wenzake kumtaka atoke nje ili aende nyumbani kupumzika. “Niliwatii kwa sababu kichwa kiliniuma sana, nikatoka nje na kwenda nyumbani kulala, ilipofikja saa 11 alfajiri nilianza safari ya kuendelea na kazi na niliwakuta wenzangu wanaanza kutoa mawe ya madini,’’ alidai.

  Aliongeza kuwa alipofika walimwomba kamba wafungie viroba vyenye mawe, “nilichukua kamba na kuwapa wakajipanga ndani ya shimo kuanzia chini huku mimi nikiwa juu kupokea na kuweka pembeni’’. “Hata hivyo katika hali ya kushangaza wenzangu wakiwa tayari wameingia shimoni ghafla nilisikia mshindo mkubwa hata mimi huku juu nikayumba kutokana na eneo zima kutetema.

  “Baada ya hali kutulia kidogo nilipokuja kuangalia kwenye mlango wa shimo nikaona limefukiwa huku moshi wa mchanga ukifuka kwa wingi kupitia mashimo mbalimbali kwa sababu mengi ya mashimo haya yamekutana chini kwa chini,’’ aliongeza na kufafanua. Alibainisha kuwa baada ya kuona hali hiyo alikimbia hadi kijijini na kutoa taarifa kwa wananchi wengine ambao nao kwa haraka walifika katika eneo la tukio na baada ya kushuhudia hali hiyo, walitoa taarifa kwa uongozi wa wilaya ambao nao kwa haraka uliwasili katika eneo la tukio.

  Baadhi ya majina ya watu wanaohofiwa kufukiwa ndani ya shimo ni pamoja na Mabeta Ngulati, Emmanuel Sumbuko, Nyahika Ryoba, Nendi Magembe, Luzenge Busu, Matondo Shaaban, Matondo Buliki, Emmanuel Blandi, Mwikwabe Chacha, Mathayo Shashala, Jumanne Mbeho na Nesi Simon.
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ni nchi ambayo haijajiandaa na majanga, kamati ya Ulinzi na Usalama kama inashindwa kupanga mikakati ya kulinda ndugu zetu Albino, mtaweza kweli kuokoa watu katika janga kubwa kama hilo. Hii yote inatokana na mikataba mibovu, haya haya madini kama tungekuwa na mikataba mizuri tukapata fedha nzuri sehemu zenye madini lazime ziwe na vikosi vya dharula. Sasa mpaka kuomba msaada kwa Mgodi wa Geita hii ni aibu kubwa sana. Lakini hata hiyo 3% wanayopata wanunue vifaa vya maafa. Wananchi ni muhumu kwa Taifa.

  Treni imeanguka juzi tu, hatuna hata vifaa vya kukatia mabehewa, eti vifaa viagiziwe Tabora. Hivi hawa watawala wako "serious" na wananchi. Hivyo vifaa visafirishwe kwa treni, badala hata zile chopa za polisi ili viwahi. Huu ni ujuha, huenda kuna watu mule ndani ya treni wangetoka wazima. Lakini muda huenda ndio utawaua.

  Hatuna zimamoto katika miji yetu, moto unatokea Bagamoyo, Zimamoto wanatoka Dar. Kweli thamani ya mtanzania iko chini sana toka kwa hawa watawala.
   
Loading...