Kazi ya ualimu ni ngumu sana. Hii ilitokea live darasani!!!!!!!!????

rifwima

JF-Expert Member
Apr 21, 2010
507
212
Kuna ticha mmoja ambaye alikuwa katika mafunzo kwa vitendo. Siku ya siku assessor alikuwa anakuja kwa ajili ya kuangalia swala zima kama kijana kaiva kwenye vitendo. Mwalimu huyo aliandaa zana zote za kufundishia na kujifunzia (teaching materials and teaching and learning aids). Lakini alisahau zana moja ambayo ni (Duster/futio la ubao).

Kijana akaanza kupiga chaki almost akajaza ubao wote isipokuwa sehemu ndogo tu. Akakumbuka hakuwa na futio, jasho likaanza kumtoka, kawaza akakumbuka ana kitambaa mfukoni so akakichukuwa akafutia ubao then akaendelea kufundisha mijasho ikiendelea kumtoka kwa sababu ya hofu ya kufukuzia points.

Mijasho ilipozidi, kwa kujisahau akajinyuka/akajifutia usoni ule mtambala alougeuza kuwa futio. Alichange sura na kuwa white haijawahi tokea. Madenti na assesor wote mbavu kwisheney!!!!!!


UALIMU NI KAZI SANA.
 
Mwalimu gani ana nidhamu ya uoga hivyo?

Alishindwa nini kunyanyua mwanafunzi mmoja na kumuagiza akalete ufutio?!

Ndio taifa la vijana wenye nidhamu za uoga,kama walimu wao ndio wako hivyo!
 
pamoja mkuu, alafu na kamshahara kalikotengwa kwa maticha nadhani kalichangia kwani ndo yuko hatua ya mwisho aanze kukapokea. tichaz oyeeeeeee
 
pamoja mkuu, alafu na kamshahara kalikotengwa kwa maticha nadhani kalichangia kwani ndo yuko hatua ya mwisho aanze kukapokea. tichaz oyeeeeeee


Yaani Jamaa alipendeza usoni usipime. Sijui assesor alimpa grade gani, lakini ningekuwa mie ningempiga ushauri nasaha wa kutosha then nampa A
 
Back
Top Bottom