Kazi ya TANESCO ni nini?

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
5,054
4,499
Nilikuwa napitia maendeleo ya mwanangu shuleni. Yeye yuko darasa la saba. Nikawa napitia mitihani yake ya nyuma. Katika mtihani wake wa somo la maarifa kulikuwa na swali hili (la mtindo wa multiple choice):

5) Kazi ya TANESCO ni:
(a) Kuzalisha umeme
(b) Kusambaza umeme
(c) Kukata umeme
(d) Kusoma mita

Mtoto alikuwa amejibu (c) na mwalimu wake akampa vyema! Mimi sikukubaliana naye. Wakati tunabishana naye umeme ukakatika. Mtoto akasema, 'Sasa baba unabishi nini, hao si TANESCO wamefanya kazi yao?'
Ilibidi nikubali na nikaongeza vyema ya pili juu ya ile ya mwalimu. Jee ungalikuwa wewe ungefanya nini?

Happy New Year!
 
(e) abcd are correct
 
anasoma chuo gani? hapa mtaani kwetu kuna chuo aisee Ila TCU wala Nacte hawajawahi kukiona
Anasoma shule ya International Academy, ada yao si mchezo. Necta ndiyo wahusika siyo Nacte. Lakini, kwani vipi si kapatia?
 
Halafu ghafla tangazo kwenye redio.

"Tanesco tunaangaza maisha yako"
 
Kugawa giza.

Kwani kirefu cha neno TANESCO ni kipi?
(a) Tanzania National Electricity Supply Company
(b) Tanzania No Electricity Supply Company
(c) Tanzania Night Supply Company
Jee kuna haja ya kupeleka mswada bungeni wa kubadilisha jina la kampuni hii? Jina lake tunapendekeza liwe lipi ili liendane na falsafa ya Hapa Kazi Tu?

Ila kwa kipindi hichi kifupi shirika hili nalipa pongezi, mgawo umepungua sana. Sijui wanahofia kufungiwa magufuli?
 
magumash ubabaishaji
Rushwa hawajali wateja...... nikikuta mfanyakazi wa tanesco analiwa na Chui haki namkatia Chui kachumbari ili amtafune vizuri hili ni jipu kuu ankoo chato anahitaji nguvu za ziada kulitusua maana Anza na wafyagiaji mpaka ngazi za juu ni uchafu
 
Last edited:
Back
Top Bottom