Kazi ya Mayor wa jiji la Dar ni nini ?

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,224
2,000
Ndugu wana jf matumaini yangu mtachangia kwa somo hilo hapo juu, kwa kweli Mayor wa dar huwa simsikii kabisa au hata kumsoma katika magazeti akichangia chochote au kafanya hiki au kile ukilinganisha na mayor wa majiji mengine duniani huenda ninaweza kupata ufunuo kidogo kutoka kwenu wataalamu wa kazi hii.

Kila nchi ina kanuni zake kitaifa kwa kazi zinazofanywa na mayor, kwa mfano UK Boris Johnson ana uwezo wa kukuza uchumi wa jiji na mamlaka ya mipango miji na kadhalika, uwezo pia ana uwezo wa kusaini mikataba ya nje kama alivyoingia mkataba na marehemu Hugo chaves wa Venezuela la mafuta.

Pia kwa NY aliekuwa Mayor wa jiji alikuwa na mamlaka makubwa pia alipiga marufuku uvutaji wa sigara sehemu nyingi na ikapita pia public health ni jukumu lake, majukumu hayo ya NY yamefuatwa na miji mingi duniani kama German na Italy na pia Dublin ikijiandaa, pia tukimwangalia Mayor wa Mexico city alitoa amri ya kukubali abortion na ikapita bila kupingwa.

Pia ndio wanalo jukumu la kupanga bajeti ya jiji lote au kusimamia, nijuavyo meya anauwezo hata kupokea wageni, kusimamia kura, kutoa maamuzi wakati wa mafuriko na athari zote kubwa. Sasa hao watu na kazi zao zinaonekana kimataifa na watu wenye uwezo mkubwa na wengine wana nguvu kitaifa kuzidi hata mawaziri wakuu na mishahara yao minono lakini, hebu tumjadili Mayor wetu wa jiji asanteni.
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
34,424
2,000
Mayor wa DSM ni nani kwani? Sykes au Kimbisa? Yusuph Mwenda Meya kinondoni,Jelly Silaa mayor wa ILALA,wa temeke ni nani?
 
Somoche

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
4,517
2,000
Masaburi ovyooo...yani hata kujenga ile stand ya Ubungo anababaisha tu...
 
Somoche

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
4,517
2,000
Sielewi kabisa nn maana ya kuwa na Meya au Mkurugenzi wa JiJi la Dar....hawana lolote wanalofanya..watu hawa hawasafishi miji....hawana mipango yeyote ya kuendeleza jiji ni upuuzi tu na wizi
 
TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
9,665
2,000
Kazi yake ni kutetea uozo wowote wa Jiji pale wabunge wanapolalamika.
Pia anatakiwa kuwa hodari wa kutukana ili atukane pale anapozidiwa hoja.
 
Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
14,810
2,000
Ndugu wana jf matumaini yangu mtachangia kwa somo hilo hapo juu, kwa kweli Mayor wa dar huwa simsikii kabisa au hata kumsoma katika magazeti akichangia chochote au kafanya hiki au kile ukilinganisha na mayor wa majiji mengine duniani huenda ninaweza kupata ufunuo kidogo kutoka kwenu wataalamu wa kazi hii.

Kila nchi ina kanuni zake kitaifa kwa kazi zinazofanywa na mayor, kwa mfano UK Boris Johnson ana uwezo wa kukuza uchumi wa jiji na mamlaka ya mipango miji na kadhalika, uwezo pia ana uwezo wa kusaini mikataba ya nje kama alivyoingia mkataba na marehemu Hugo chaves wa Venezuela la mafuta.

Pia kwa NY aliekuwa Mayor wa jiji alikuwa na mamlaka makubwa pia alipiga marufuku uvutaji wa sigara sehemu nyingi na ikapita pia public health ni jukumu lake, majukumu hayo ya NY yamefuatwa na miji mingi duniani kama German na Italy na pia Dublin ikijiandaa, pia tukimwangalia Mayor wa Mexico city alitoa amri ya kukubali abortion na ikapita bila kupingwa.

Pia ndio wanalo jukumu la kupanga bajeti ya jiji lote au kusimamia, nijuavyo meya anauwezo hata kupokea wageni, kusimamia kura, kutoa maamuzi wakati wa mafuriko na athari zote kubwa. Sasa hao watu na kazi zao zinaonekana kimataifa na watu wenye uwezo mkubwa na wengine wana nguvu kitaifa kuzidi hata mawaziri wakuu na mishahara yao minono lakini, hebu tumjadili Mayor wetu wa jiji asanteni.

Mkuu tatizo la Tanzania, system yetu tuliiga ya uongozaji wa serikali kutoka kwa mwingereza, sasa tatizo kubwa wenzetu wanaenda na wakati na kubadili utekelezaji wa mambo yao kutokana na wakati. Sisi bado tuko pale pale wanabadili kujinufaisha wao viongozi sio matakwa ya walalahoi hapo ndipo kwenye tatizo. Unakuta rais anachagua wakuu wa mikoa wilaya etc uliza kazi wanazofanya utacheka mwenyewe.
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,224
2,000

Mkuu tatizo la Tanzania, system yetu tuliiga ya uongozaji wa serikali kutoka kwa mwingereza, sasa tatizo kubwa wenzetu wanaenda na wakati na kubadili utekelezaji wa mambo yao kutokana na wakati. Sisi bado tuko pale pale wanabadili kujinufaisha wao viongozi sio matakwa ya walalahoi hapo ndipo kwenye tatizo. Unakuta rais anachagua wakuu wa mikoa wilaya etc uliza kazi wanazofanya utacheka mwenyewe.
Inasikitisha mtu una mamlaka ya nchi na inazidi kuzorota kila siku hadi siku halafu hata uchungu maendeleo kama ya wenzetu hawana, hivi unaishi humu humu nchini na una uwezo wa kuibadilisha na kusonga mbele, what's the point of living in a luxury house and drive a posh car wakati barabara unayopita inanuka kwa vinyesi
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,224
2,000
Aiseeee Dar-Es-Salaam ina Ma-Mayor wanne? Matumizi mabaya ya kodi za wananchi.
Cha kushangaza wote wakiugua ni kukimbilia nje na kusoma wakasome nje lakini wanaporudi na kuona maendeleo ya wenzetu hata mshipa hauwashtuki akikuta mfuko wa rambo umejaa kinyesi anaona sawa tu, sijui wanawaza nini baada ya kupata madaraka.
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,224
2,000
Acheni polojo kujadili shibe za watu bwana je cheo hicho ungekuwa nacho ww ingekuwaje
Hatujadili shibe za watu mkuu ila ni kutaka kuona maendeleo ya jiji kuwa katika hadhi nzuri kama miundombinu yote maana ukizingatia majukumu ya meya ndio hayo. Ningepata cheo hicho ningeubali mji na kuuweka sawa kama bajeti ningeipanga mimi
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,224
2,000
Kwanza kazi za meya ni nini????

Hawana faida kwa watanzania
Kwa Tanzania kwa kweli ni title tu lakini kwa majukumu sidhani kama ana kazi yoyote ndio maana nilitaka kujua maana laiti wangejua majukumu ya mameya duniani nadhani wangelifanyia kazi, unajuwa Mayor wana kazi nyingi kupita mawaziri na majukumu kuliko baadhi ya PM's ndio maana top Mayor wanalipwa mpaka 400,000m (Tsh) kwa mwezi lakini wanachapa kazi na heshima kubwa
 
ndechilio shoo

JF-Expert Member
Feb 16, 2013
999
1,225
meya wa dar yupo chanika kwenye chuo chake cha ugavi na shule yake inaitwa dk didasi secondary school ipo chanika mwisho kama unaenda mvuti
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom