Mugishagwe
JF-Expert Member
- Apr 28, 2006
- 300
- 58
Wapinzani waanza na uzushi Bungeni
2006-06-20 11:03:33
Na Nelson Goima, Dodoma
Katika muda usiozidi saa moja Bungeni jana, vigogo wawili wa kambi ya upinzani, walilazimika kufuta kauli za uongo, walizotoa wakati wakisoma maoni ya kambi yao juu ya Hotuba za Bajeti? ya Serikali na Hotuba ya Mipango na Uchumi.
Vigogo hao ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Bw. Hamad Rashid Mohamed, aliyetoa maoni juu ya Bajeti ya Serikali.
Bw. Hamad alilidanganya Bunge kwa kudai eti kuwa Rais Jakaya Kikwete anaiogopa ndege ya kisasa ya Rais, hatua iliyomfanya hivi karibuni kudandia lifti ya ndege hadi Dodoma.
Kigogo mwingine ni Msemaji katika Wizara ya Mipango, Bw. Kabwe Zitto, aliyedai kuwa watu serikalini wamenona na wana majumba ya kifahari Pretoria, Afrika Kusini.
Zitto alisema watu hao ni waliotia saini mkataba wa kuendesha menejimenti ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kampuni ya NetGroup Solution ya Afrika Kusini.
Alisema mkataba huo umetumbukiza nchi pabaya na kusababisha matatizo makubwa ya umeme, lakini walioingia mkataba huo wamenona na wana majumba Pretoria. Pretoria ni mji mkuu wa Afrika Kusini.
Wa kwanza kutoa maoni alikuwa Zitto, ambaye alisoma maelezo mengi na baadaye akachomeka suala hilo la NetGroup Solution na TANESCO.
Alisema mkataba baina ya makampuni hayo haujainufaisha nchi na pia ingawa NetGroup inakaribia kuondoka, kuna watu wamenufaika.
Mara tu Zitto alipoanza kutoa madai hayo, Mnadhimu Mkuu wa Serikali Bungeni, Bw. Juma Akukweti, alisimama na kueleza kuwa utaratibu wa Bunge umekiukwa.
Kanuni za Bunge Kifungu cha 50 kinasema mbunge hatakiwi kusema jambo la uongo bungeni, hivyo Mheshimiwa Naibu Spika namuomba Mbunge afute kauli yake au atoe ushahidi wa madai yake kuwa watu walioingia mkataba huo, sasa wamenona na wana majumba Pretoria, alisema Bw. Akukweti, ambaye pia ni Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge.
Papo hapo, Naibu Spika Bi. Anne Makinda, alimtaka Zitto athibitishe kauli yake au alete ushahidi, ambapo alisema anaondoa hoja yake. Hivyo, akaruhusiwa kuendelea kutoa maoni yake.
Alipomaliza Zitto, alifuatia Bw. Hamad Rashid kutoa maoni ya wapinzani kuhusu Hotuba ya Bajeti.
Alisoma maelezo marefu, lakini kama ilivyokuwa kwa Zitto naye alichomekea suala la ndege la Rais.
Bw. Hamad alidai kuwa ndege hiyo ya Rais iliyonunuliwa kwa mabilioni ya fedha, hivi sasa imebaki white elephant, kwani haitembei na wala haitumiwi na mwenyewe(Rais).
Alidai kuwa wao wapinzani walipinga kununuliwa kwa ndege hiyo ya kifahari pamoja na radar kubwa, iliyopo Dar es Salaam.
Alidai kuwa wakati ndege hiyo inanunuliwa walielezwa kuwa ingemwezesha Rais kusafiri raha mustarehe bila usumbufu, lakini hivi sasa Rais anadandia lifti na anaiacha ndege yake.
Baada ya kutoa kauli hiyo, Bw. Akukweti alisimama na kusema Kifungu cha 50 kinaeleza kuwa maelezo anayotoa Mbunge ndani ya Bunge, lazima yawe sahihi na siyo ya kubahatisha.
Tungependa kufahamu kama Mheshimiwa Mbunge ana ushahidi kuwa ni kweli Rais anadandia lifti. Kama ana ushahidi atoe na kama hana afute kauli.
Ndipo Naibu Spika, Bi Anne Makinda, alimtaka Bw. Hamad afute kauli yake au atoe ushahidi, ambapo Bw. Hamad alisema Mheshimiwa Naibu Spika sisi katika mazoea yetu ya kawaida, tunapomuona Rais ambaye ana ndege yake maalum anatumia usafiri mwingine, tunachukulia kuwa amepewa lifti.
Baada ya kutoa jibu hilo, Hamad alibanwa na Naibu Spika atoe ushahidi ni ndege gani iliyompa lifti Rais au afute kauli yake kama hana ushahidi, Bw. Hamad alisema naondoa hoja yangu.
Baada ya hapo alipewa ruhusa ya kuendelea kutoa maoni yake.
SOURCE: Nipashe