Kazi ya kusaka Mabilioni nje yaanza: Rostam, Mbowe, Ngeleja wahojiwa!

habariyamujini

JF-Expert Member
May 16, 2013
3,094
456
- Mbowe adaiwa kumiliki Jumba Dubai, Ngeleja naye yumo

Mwenyekiti wa Chama ch Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja na Mfanyabiashara maarufu Rostam Aziz wamehojiwa kuhusu kuwa na utajiri mkubwa nje ya nchi, Raia Mwema limearifiwa.

Wanasiasa hao wamehojiwa na kikosi kazi maalum kilichoundwa na serikali hivi karibuni kwa ajili ya kutafuta mali mbalimbali zilizofichwa nje ya nchi na watu mbalimbali wenye nyadhifa kubwa.

Ingawa watendaji wakuu wa kikosi kazi hicho wamekataa kuthibitisha au kukana kuhusu kuojiwa kwa wanasiasa hao, gazeti hili limeambiwa wanasiasa hao ni sehemu ya watu zaidi ya 100 wanaochunguzwa na vyombo vya dola.

Kikosi hicho kiliundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kinaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Dk. Edward Hoseah na wawakilishi kutoka Jeshi la Polisi, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wataalam wa masuala ya kibenki.

Chanzo cha kuaminika cha gazeti hili kilisema Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, alihojiwa kutokana na maelezo kuwa alinunua jumba la kifahari Dubai, Desemba mwaka 2011.

"Kutokana na wadhifa wake kwa umma, Mbowe ilibidi achunguzwe kutokana na ununuzi wa nyumba alioufanya nchini Dubai, Desemba mwaka 2011"

"Uchunguzi wake ni mahususi kwa sababu tumefuatilia akaunti zake na ikaonekana hakuwahi kutumia njia ya benki kufanya malipo.

"Hii maana yake ni kwamba kama alifanya malipo, basi alifanya kwa kutumia fedha taslim (cash)
.

"Sasa ni lazima ichunguzwe maana si kawaida kwa kiongozi kama yeye kusafiri na mabilioni yote ya kununua jumba kule Dubai na kulipa cash. Ndiyo maana yeye anafanyiwa uchunguzi mahususi," kilisema chanzo cha kuaminika cha gazeti hili.

Rostam ni miongoni mwa wafanyabiashara maarufu hapa nchini na Raia Mwema limeelezwa kwamba alihojiwa kutokana na kumiliki jumba katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati na gazeti hili limeelezwa pia kuwa ana akaunti kadhaa nje ya nchi.

Dubai ni kimbilio la wafanyabiashara maarufu, Rostam aliwahi kuwa mbunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na alipata pia kuwa Mweka Hazina wa chama hicho.

Hadi tunakwenda mitamboni, gazeti hili lilikuwa halijafahamu ni kwa sababu ya mali zipi hasa Ngeleja anazo lakini wakati akiwa Waziri na Nishati na Madini, kulikuwa na minong'ono kwamba alikuwa miongoni mwa mawaziri vijana wenye ukwasi mkubwa aliokuwaa ndani ya muda mfupi.

Alipoulizwa na Raia Mwema kuhusu alichohojiwa alipoitwa na kikosi kazi, Ngeleja alijibu kwa ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu yake ya mkononi; "Samahani, mimi si msemaji wa suala hilo." Hata alipoombwa na mwandishi walau kukanusha au kukataa kuwa alihojiwa - Ngeleja alijibu kwa ufupi, "Ahsante"

Kwa sasa, waziri huyo wa zamani wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete yupo safarini nje ya nchi.

Alipotafutwa wiki hii kuelezea upande wake kuhusu alichohojiwa, Rostam hakujibu simu wala ujumbe mfupi wa maneno aliotumiwa na mwandishi.

Mbowe hakuwa tayari kueleza kuhusu kuhojiwa huko ingawa Ofisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene, aliyeeleza kuwa ameagizwa kujibu kwa niaba ya mkuu huyo wa upinzani alisema; "Si jambo la ajabu kwa Mbowe kuwa na mali nje ya nchi kwa vile ni mfanyabiashara na ana biashara hadi nje ya nchi."

Kikosi kazi kinafanya kazi zake katika mazingira ya usiri na tangu kilipoanza kazi mapema mwaka huu hakijawahi kutoa taarifa rasmi kuhusu shughuli zake.

Mmoja wa wajumbe wa kikosi kazi hicho, Dk. Hoseah alikataa kuzungumza chochote kuhusu watu waliowahoji kwa maelezo kuwa msemaji wa shughuli yao ni Werema.

Werema hakutaka kukana wala kuthibitisha taarifa hii isipokuwa katika mazungumzo ya nyuma na vyombo vya habari aliwahi kusema kwamba ni kinyume cha maadili kwa tume hiyo kutoa taarifa kuhusu watu iliowahoji.

Raia Mwema linafahamu kwamba mtu kuhojiwa na kikosi hicho haimaanishi moja kwa moja kwamba ni fisadi isipokuwa mahojiano yanafanyika kwa minajili ya kukusanya taarifa.

Novemba mwaka jana, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe alitoa hoja binafsi bungeni akitaka ufanyike uchunguzi wa fedha na mali haramu kutoka Tanzania zilizofichwa katika nchi mbalimbali duniani.

Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, raia wake hawaruhusiwi kufungua akaunti katika nchi za kigeni pasipo ruhusa ya Ofisi ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

Katika hoja yake binafsi, Zitto alitaka Bunge lipewe nguvu ya kuunda Kamati Teule ambayo itachunguza na kubaini ni akina nani wanamiliki akaunti na mali ughaibuni lakini serikali iliamua yenyewe kuwa ndiyo itafuatilia kwa kutumia vyombo vyake.

Chanzo: Raia Mwema 23rd October 2013 (Soma kiambatisho)

MY TAKE:
KUMBE MBOWE NAYE WAMO JAPO HAWAVUMI?? basi hakuna msafi hapa duniani.

Tangu October 23, 2013, |

Na Peter Ambilikile

SIRI nzito imefichuka kuwa miongoni mwa walioficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi yumo mmoja wa wanasiasa maarufu anayetajwa kuwa anataka kuwania urais mwaka 2015. Sakata la mabilioni ya fedha za Tanzania kufichwa nchini Uswisi liliibuliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema), ambapo kwa sasa yupo nchini humo kwa ajili ya kufuatilia kwa kina fedha hizo na waliozificha. Hata hivyo, kutokana na uzito wa suala hilo, Kamati Maalumu ya Bunge imepewa jukumu la kufuatilia fedha hizo ambazo baada ya kubainika kufichwa ziliibua mjadala mkubwa nchini huku wanasiasa kadhaa wakitaka walioficha watajwe hadharani na ikiwezekana zitaifishwe. Taarifa ambazo Jambo Leo imezipata zinaeleza kuwa miongoni mwa majina ya watu ambao wanadaiwa kuweka fedha hizo yumo mwanasiasa maarufu anayetajwa kuwania urais (jina tunalo). "Tuna taarifa za uhakika kuwa mmoja wa wanasiasa anayetajwa kutaka kuwania urais mwaka 2015 naye anahusishwa kuwa ameficha fedha Uswisi. Tunaamini Zitto atakuja na ukweli maana analifuatilia kwa karibu," kilidokeza chanzo chetu cha habari.

Hata hivyo, Zitto wakati anazungumzia suala hilo kabla ya kuondoka kwenda Uswisi alisema Watanzania watafahamu ukweli kuhusu fedha hizo kuanzia walioficha majina na akaunti zao. Akitoa maoni yake kuhusu mabilioni ya fedha za Tanzania kufichwa nchini Uswisi, Mbunge wa Jimbo la Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), alisema ni vema ikafahamika mtu au mfanyabiashara kuweka fedha nje ya nchi yake si kosa. Alifafanua kuwa kosa linaweza kujitokeza iwapo katika kuweka fedha hizo taratibu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambayo huidhinisha suala hilo haukufuatwa. "Mfanyabiashara au mtu yeyote anaweza kuweka fedha nje kama amekubaliwa na taratibu husika za BoT.

"Kama amekubaliwa hakuna pingamizi na atakuwa huru kuweka fedha zake, katika hilo hawezi kupata msukosuko kwani kila kipengele ametimiza kikiwemo cha kukatwa kodi halali ya fedha hizo," alisema.

Hata hivyo, alisema fedha hizo ambazo zinadaiwa kufichwa nchini Uswisi zinaweza kuwa na mambo makubwa mawili, moja zimefuata utaratibu au kutofuata taratibu za BoT.

"Inawezeka kuna ajenda nyingine ya fedha hizo kufichwa kwa sababu tu ya kutaka kukwepa kulipa kodi halali na kujipatia fedha kwa njia isiyokuwa sahihi," alisisitiza.

Pia alisema inawezekana sababu nyingine ya kuficha fedha hizo ni kwamba zimepatikana kwa njia haramu ikiwemo ya biashara ya dawa za kulevya au kamisheni iliyotokana na njia isiyo halali na kufanya wenye fedha hizo kuzifichwa nje ya Tanzania.

Alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa jina la mwanasiasa anayetaka kuwania urais mwaka 2015 kuwa anadaiwa kuweka fedha Uswis akishirikiana na wenzake, alijibu kuwa katika maisha yake haamini habari za kusikia bali anataka habari ambazo zimethibitishwa.

"Niwaombe Watanzania wenzangu kuwa hakuna sababu ya kuishi kwa kusikia habari za fununu, ni vema mkafanyakazi kwa taarifa za uthibitisho. Siku hizi imekuwa ni mambo ya kawaida watu kushutumiana na kuchafuana kwa kutaja majina ya watu bila ushahidi.

"Hili si jambo nzuri tunapaswa kubadilika. Ni dhambi hata kwa Mwenyezi Mungu kumshutumu mtu bila sababu," alisema.

Kuhusu sakata hilo, alisema Bunge liliunda kamati ya kuchunguza suala hilo na bado inamalizia kazi hiyo na kwamba ripoti yake itakabidhiwa katika vikao vijavyo vya Bunge, hivyo ni vema Watanzania wakawa na subira na si kuanza kutajana majina kwa lengo la kuchafuana.

"Nimefurahishwa na juhudi zinazofanywa na Zitto kuhusu ya jambo hilo na ninaamini kwa vile ni miongoni mwa watu wanaolichunguza atakuja na majina ya watu waliotorosha fedha hizo nje ya nchi na kuwataka Watanzania wasubiri," alisema.

Pia alisema kama ni kweli anayetajwa ni mgombea urais mtarajiwa basi sifa zake zitaishia hapo kwani hata baba wa taifa aliwahi kusema mtu anayetumia fedha kuingia Ikulu atakuwa amezipata wapi na atazirudishaje. Mwenyekiti wa Demokratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila alisema haamini kama Zitto anaweza kuwa na majibu sahihi maana hao hao ambao wameficha fedha ana maslahi nao kisiasa.

"Pamoja na porojo na propaganda zinazotolewa na Zitto jibu atakalokuja nalo baada ya kutoka Uswisi halitakuwa na mshiko kutokana na yeye kuwa na maslahi tofauti na watu wanavyofikiri," alisema Mtikila.

Hata hivyo, Zitto amekuwa akizungumzia msimamo wake kuwa atahakikisha analisimamia na Watanzania watapata ukweli na kamwe hatayumbishwa na mtu yeyote katika suala hilo. Kabla ya kuondoka mwishoni mwa wiki iliyopita kwenda Uswisi, Zitto aliwataka Watanzania wamuamini kwani anakwenda kutafuta ukweli na wote ambao watakaohusika majina yao atayaanika hadharani.

source:
logo.png

1.png

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja na Mfanyabiashara maarufu, Rostam Aziz, wamehojiwa kuhusu kuwa na utajiri mkubwa nje ya nchi.

Wanasiasa hao wamehojiwa na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na serikali hivi karibuni kwa ajili ya kutafuta mali mbalimbali zilizofichwa nje ya nchi na watu mbalimbai wenye nyadhifa kubwa.

Ingawa watendaji wakuu wa kikosi kazi hicho wamekataa kuthibitisha au kukana kuhusu kuhojiwa kwa wanasiasa hao, Raia Mwema limeambiwa wanasiasa hao ni sehemu tu ya watu zaidi ya 100 wanaochunguzwa na vyombo vya dola.

Kikosi hicho kiliundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kinaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah na wawakilishi kutoka Jeshi la Polisi, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na waatalamu wa masuala ya kibenki.

Chanzo cha kuaminika cha kilisema Mbowe ambaye pia ndiye Kiongozi wa Upinzani Bungeni,alihojiwa kutokana na maelezo kuwa alinunua jumba la kifahari nchini Dubai, Desemba mwaka 2011.

"Kutokana na wadhifa wake kwa umma, Mbowe ilibidi achunguzwe kutokana na ununuzi wa nyumba alioufanya nchini Dubai, Desemba mwaka 2011.

Uchunguzi wake ni mahususi kwa sababu tumefuatilia akaunti zake na ikaonekana hakuwahi kutumia njia ya benki kufanya malipo.

"Hii maana yake ni kwamba kama alifanya malipo, basi alifanya kwa kutumia fedha taslim (cash). Sasa ni lazima ichunguzwe maana si kawaida kwa kiongozi kama yeye kusafiri na mamilioni yote ya kununua jumba kule Dubai na kulipa cash. Ndiyo maana yeye anafanyiwa uchunguzi mahususi,"kilisema chanzo cha kuaminika cha gazeti hili.

Rostam ni miongoni mwa wafanyabiashara maarufu hapa nchini na Raia Mwema limeelezwa kwamba alihojiwa kutokana na kumiliki jumba katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati na imeelezwa pia kuwa ana akaunti kadhaa nje ya nchi.

Dubai ni kimbilio la wafanyabiashara wengi kutokana na nafuu ya kodi inayotolewa na serikali ya nchi hiyo na pia uwepo wa biashara na usalama mkubwa uliopo.

Zaidi ya kuwa mfanyabiashara maarufu, Rostam aliwahi kuwa mbunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na alipata pia kuwa Mweka Hazina wa chama hicho.

Hadi tunakwenda mitamboni, gazeti hili lilikuwa halijafahamu ni kwa sababu ya mali zipi hasa ambazo Ngeleja anazo lakini wakati akiwa Waziri wa Nishati na Madini, kulikuwa na minong'ono kwamba alikuwa miongoni mwa mawaziri vijana wenye ukwasi mkubwa alioukwaa ndani ya muda mfupi.

Alipoulizwa na Raia Mwema kuhusu alichohojiwa alipoitwa na kikosi kazi, Ngeleja alijibu kwa ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu yake ya mkononi; "Samahani, mimi si msemaji wa suala hilo." Hata alipoombwa na mwandishi walau kukanusha au kukataa kuwa alihojiwa – Ngeleja alijibu kwa ufupi, "Ahsante."

Kwa sasa, waziri huyo wa zamani wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete yuko safarini nje ya nchi.

Alipotafutwa wiki hii kueleza upande wake kuhusu alichohojiwa, Rostam hakujibu simu wala ujumbe mfupi wa maneno aliotumiwa na mwandishi.

Mbowe hakuwa tayari kueleza kuhusu kuhojiwa huko ingawa Ofisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene, aliyeeleza kuwa ameagizwa kujibu kwa niaba ya mkuu huyo wa upinzani, alisema; "si jambo la ajabu kwa Mbowe kuwa na mali nje ya nchi kwa vile ni mfanyabiashara na ana biashara hadi nje ya nchi."

Kikosi kazi kinafanya kazi zake katika mazingira ya usiri na tangu kilipoanza kazi mapema mwaka huu, hakijawahi kutoa taarifa rasmi kuhusu shughuli zake.

Mmoja wa wajumbe wa kikosi kazi hicho, Dk. Hoseah alikataa kuzungumza chochote kuhusu watu waliowahoji kwa maelezo kuwa msemaji wa shughuli yao ni Werema.

Werema hakutaka kukana wala kuthibitisha taarifa hii isipokuwa katika mazungumzo ya nyuma na vyombo vya habari aliwahi kusema kwamba ni kinyume cha maadili kwa tume hiyo kutoa taarifa kuhusu watu iliowahoji.

Raia Mwema linafahamu kwamba mtu kuhojiwa na kikosi hicho haimaanishi moja kwa moja kwamba ni fisadi isipokuwa mahojiano yanafanyika kwa minajili ya kukusanya taarifa.

Novemba mwaka jana, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, alitoa hoja binafsi bungeni akitaka ufanyike uchunguzi wa fedha na mali haramu kutoka Tanzania zilizofichwa katika nchimbalimbali duniani.

Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, raia wake hawaruhusiwi kufungua akaunti katika nchi za kigeni pasipo ruhusa ya ofisi ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

Katika hoja yake binafsi, Zitto alitaka Bunge lipewe nguvu ya kuunda Kamati Teule ambayo itachunguza na kubaini ni akina nani wanamiliki akaunti na mali ughaibuni lakini serikali iliamua yenyewe kuwa ndiyo itafuatilia kwa kutumia vyombo vyake.

Attachments

  • MBOWE NA ROSTAM MABILIONI.jpg
    MBOWE NA ROSTAM MABILIONI.jpg
    412.3 KB · Views: 1,321
  • ROSTAM NA MBOWE WAHOJIWA MABILIONI USWISI.jpg
    ROSTAM NA MBOWE WAHOJIWA MABILIONI USWISI.jpg
    334 KB · Views: 1,379
  • MBOWE NA ROSTAM MABILIONI.jpg
    MBOWE NA ROSTAM MABILIONI.jpg
    412.1 KB · Views: 1,499
Mbowe ni Mfanyabiashara ambaye hajwahi kuwa implicated kwenye scandal yoyote ya kukwepa kodi au kuliibia Taifa .Sasa mantiki ya Heading ya kumfananisha na Rostam iko wapi kama sio malengo hasi ya kumchafua kisiasa tu?

Hii mentality hasi dhidi ya wafanyabiashara inesababushwa na mfumo wa kimaskini ambao umelifanya taifa hili kuwa na chuki za ajabu huku wezi wa mali za umma wakishangiliwa kama Celebrities!

Sasa hoja ya malipo na njia zilizotumika kulipia inamfanishaje na Rostam?Hapa kuna mbinu za kuwaficha wahalifu na pia kuna harufu ya political witch hunting!

This is another way of political jujutsu!
 
kamanda amebanwa, mkuu naona unalialia tu, waje watuambie hayo majumba ya Dubai ni haki yao wao kua nayo lakini wengine wakiwa nayo ni wezi...haya sasa..halafu cash mkuu, its is cash..au labda ule mfumo wa hawala ndio umetumika hapa...
 
Kuwafananisha Mbowe na Rostam ni uzuzu. Si Mbowe wala chama chake wamewahi kushika dola kwa hiyo kama ana utajiri basi kaupata kwa njia zingine (hata kama haramu) pasi na kutumia madaraka aidha yake au ya chama chake.
kwahiyo upatikanaji haramu wa mali kwa chadema ni RUKSA!!! kama ni RUKSA mnatupa wasiwasi kuwapa nchi watu wanaohalalisha uharamu from the beginning..hamtufai simply as that...
 
Mbowe ni Mfanyabiashara
ambaye hajwahi kuwa implicated kwenye scandal yoyote ya kukwepa kodi au
kuliibia Taifa .Sasa mantiki ya Heading ya kumfananisha na Rostam iko
wapi kama sio malengo hasi ya kumchafua kisiasa tu?

Hii mentality hasi dhidi ya wafanyabiashara inesababushwa na mfumo wa
kimaskini ambao umelifanya taifa hili kuwa na chuki za ajabu huku wezi
wa mali za umma wakishangiliwa kama Celebrities!

Sasa hoja ya malipo na njia zilizotumika kulipia inamfanishaje na
Rostam?Hapa kuna mbinu za kuwaficha wahalifu na pia kuna harufu ya
political witch hunting!

This is another way of political jujutsu!
hajawahi kuwa sasa ndiyo kawa sasa mbowe alianza ufisadi kitambo alikuwa hajastukiwa tu sasa wamembamba ataipata.
 
Mbowe ni Mfanyabiashara ambaye hajawahi kuwa implicated kwenye scandal yoyote ya kukwepa kodi au kuliibia Taifa

Kumekucha.Kama hajawahi basi sasa ndio ameanza.Kuliibia taifa kwaweza kuwa na sura nyingi likiwemo kuchukua ruzuku ya chama (ambazo ni hela za walipa kodi) na kwenda kununua Jengo Dubai.Au kuficha michango ya wafadhili wa nje ya nchi wanaokifadhili chama na kuzipeleka kununua Jengo Dubai.

Mbivu na mbichi zitaeleweka tu uchunguzi uendelee tu.Mafisadi na wezi wako kila kona ikiwemo vyama vya upinzani.Tusubiri uchunguzi uendelee.Kusema hajawahi si hoja.Tuachie tume inayochunguza na mahakama waseme.Usijipe kazi ya tume au mahakama kusema hajawahi au hawezi kuwa na nyumba dubai.
 
Mbowe ni Mfanyabiashara ambaye hajwahi kuwa implicated kwenye scandal yoyote ya kukwepa kodi au kuliibia Taifa .Sasa mantiki ya Heading ya kumfananisha na Rostam iko wapi kama sio malengo hasi ya kumchafua kisiasa tu?

Hii mentality hasi dhidi ya wafanyabiashara inesababushwa na mfumo wa kimaskini ambao umelifanya taifa hili kuwa na chuki za ajabu huku wezi wa mali za umma wakishangiliwa kama Celebrities!

Sasa hoja ya malipo na njia zilizotumika kulipia inamfanishaje na Rostam?Hapa kuna mbinu za kuwaficha wahalifu na pia kuna harufu ya political witch hunting!

This is another way of political jujutsu!

Ni juzi tu mlikurupuka kumtetea DR Slaa kuwa alisahau ku log out kwenye deviice yake na kutumiwa na mtu mwingine. Alipokuja mwenyewe kuweka facts ikawa ni tofauti na assumptions zenu.

Inawezekana ikawa ni political game, ila na nyie mmezidi kukuruka kuwatetea watu ambao hata hamjui biashara wanazozifanya!

Kutokuwa implicated kwenye scandal it doesn't say anything kuwa hajawahi kuliibia taifa au kukwepa kodi.

Kuwa neutral kama huna facts ni vizuri kuliko jumping into conclusions ambazo baadae zitawaumbua.
 
ukanda ule unashida kwenye mambo ya pesa waliowengi ni wezi na tapeli huyu mbowe hela za chama anafuja kumbe upande wa pili fisadi.
kumbe upande mwema upande mnafiki atimuliwe kwenye chama amwachie zito hatumtaki tena.
 
hao waliyo pewa jukumu la kushughurikia hilo swala umewaona. hosea aliye tumika kuisafisha richmond, werema, kibaraka wa magamba na zitto kabwe ambaye namuona ni kigeugeu namba moja, hii ishu itaishia hewani hakuna chochote cha maana tutasikia, serikalini kumejaa watu wachafu ndiyo maana hakuna hata wa kusimamia mwaswala ya msingi kama haya
 
hajawahi kuwa sasa ndiyo kawa sasa mbowe alianza ufisadi kitambo alikuwa hajastukiwa tu sasa wamembamba ataipata.

Watapambana, lakini hawatashinda. Kwa Mbowe hapo wamebugi meeen!!! Ni tume za kikanjanja tu ndizo zinazoweza kufanya ilichokifanya hii tume.
 
kamanda amebanwa, mkuu naona
unalialia tu, waje watuambie hayo majumba ya Dubai ni haki yao wao kua
nayo lakini wengine wakiwa nayo ni wezi...haya sasa..halafu cash mkuu,
its is cash..au labda ule mfumo wa hawala ndio umetumika hapa...
wamhoji vizuri mbowe atakuwa kaficha mali nyingi sana lo! baba anatamaa huyu halafu kwenye mikutano changieni chama chenu kumbe yeye fisadi.
 
Sidhani kama kuna uhalali wa gazeti kuandika kuhusu Mbowe na utajiri wake sababu yeye alikua tajiri hata kabla hajazaliwa.
Mbowe ni kiongozi wa umma ni kweli , lakini akaunti zake kutokua na kumbukumbu za kununua nyumba hazimfanyi kuwa mshukiwa,
Hizi ni propaganda na tumeshaambiwa mapema kuwa watamchafua kiongozi huyu mahiri ktk anga la siasa.

Inasikitisha vyombo vya habari vikiwemo magazeti ,na mitandao ya kijamii kusikiliza upande mmoja tu bila kujua upande wa pili.

Ni kichaa tu ndio atakaeamini huu upuuzi na ufinyu wa fikra.
 
kamanda amebanwa, mkuu naona unalialia tu, waje watuambie hayo majumba ya Dubai ni haki yao wao kua nayo lakini wengine wakiwa nayo ni wezi...haya sasa..halafu cash mkuu, its is cash..au labda ule mfumo wa hawala ndio umetumika hapa...

Ndiyo Mfanyabiashara msafi anayelipa kodi ni haki yake kumiliki na ndiyo maana sera ya CHADEMA ni kuruhusu individual creativity na serikali inaweka mazingira mazuri bila intervention kubwa ili creativity ya mtu iwe rewarded.Hao walioiba usiwafananishe na wafanyabiashara safi

Ndiyo maana Pinda aliwatambua mentality zenu akawatangazia kuwa anazo shilingi milioni 25 tu kwenye akaunti kama vile ni ufahari sana kuishi maisha ya kimaskini huku ukiwa kazini kwa miaka zaidi 35.

CHADEMA kinaamini kama tungeweka sera sahihi basi Tanzania kingekua na Mamilionea na mabilionea wetu wa kutosha.Tunaamini katika matumizi ya raslimali zetu kwa ajili ya kuboresha maisha yetu na kujivunia aendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Tuachane na hizi mentality dwarf.Umaskini si kitu cha kuona kama vile ni pride ya jamii.Unaweza kuwa wewe ni mwizi na mroho uliyekubuhu lakini mchumia tumbo tu hivyo unakua maskini wa kudumu au ukawa jizi linalojua kuwekeza (Nyote ni wezi) na pia unaweza ukawa mfanyabiashara anayefuata kanuni na sheria zote za nchi kibiashara na kijamii.

Sasa kuna chaguzi ndani ya CHADEMA mambo kama haya ni lazima yaibuke ba mengine zaidi.Kuna sakata la fedha zilizotoroshwa nje na kuna njama za ku-dilute case hii kwa kuwatoa kafara political figure wa Upinzani.Ni lazima tuukatae uhuni na mchezo huu wa kishamba kabisa.
 
ukanda ule unashida kwenye mambo ya pesa waliowengi ni wezi na tapeli huyu mbowe hela za chama anafuja kumbe upande wa pili fisadi.
kumbe upande mwema upande mnafiki atimuliwe kwenye chama amwachie zito hatumtaki tena.
mind you, it is a cash transaction, that means haikutakiwa kufahamika sources za hiyo pesa, if it was a clean transaction , mbona tu kuna bank to bank transactions...maswali tunayo sisi majibu wanayo wenyewe..
 
Ndiyo Mfanyabiashara msafi anayelipa kodi ni haki yake kumiliki na ndiyo maana sera ya CHADEMA ni kuruhusu individual creativity na serikali inaweka mazingira mazuri bila intervention kubwa ili creativity ya mtu iwe rewarded.Hao walioiba usiwafananishe na wafanyabiashara safi

Ndiyo maana Pinda aliwatambua mentality zenu akawatangazia kuwa anazo shilingi milioni 25 tu kwenye akaunti kama vile ni ufahari sana kuishi maisha ya kimaskini huku ukiwa kazini kwa miaka zaidi 35.

CHADEMA kinaamini kama tungeweka sera sahihi basi Tanzania kingekua na Mamilionea na mabilionea wetu wa kutosha.Tunaamini katika matumizi ya raslimali zetu kwa ajili ya kuboresha maisha yetu na kujivunia aendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Tuachane na hizi mentality dwarf.Umaskini si kitu cha kuona kama vile ni pride ya jamii.Unaweza kuwa wewe ni mwizi na mroho uliyekubuhu lakini mchumia tumbo tu hivyo unakua maskini wa kudumu au ukawa jizi linalojua kuwekeza (Nyote ni wezi) na pia unaweza ukawa mfanyabiashara anayefuata kanuni na sheria zote za nchi kibiashara na kijamii.

Sasa kuna chaguzi ndani ya CHADEMA mambo kama haya ni lazima yaibuke ba mengine zaidi.Kuna sakata la fedha zilizotoroshwa nje na kuna njama za ku-dilute case hii kwa kuwatoa kafara political figure wa Upinzani.Ni lazima tuukatae uhuni na mchezo huu wa kishamba kabisa.
simply explain to me and i know that you don't have answers right now, kwanini ikawa a cash transaction na sio bank to bank, nini kilikua kinafichwa??? nadhani inajua when it comes to deal being handled in cash wahusika wanataka kuficha nini..watu wawazi katika biashara hutumia bank to bank payments!!!
 
kwahiyo upatikanaji haramu wa mali kwa chadema ni RUKSA!!! kama ni RUKSA mnatupa wasiwasi kuwapa nchi watu wanaohalalisha uharamu from the beginning..hamtufai simply as that...

Wapi imerukhsiwa kupata mali kwa haramu? Kwani CCM viongozi wake ni wepi wamepata mali kwa halali?
 
Back
Top Bottom