Kazi ya kuandika katiba mpya ni kazi muhimu kuliko zote katika Taifa lolote( kazi takatifu) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kazi ya kuandika katiba mpya ni kazi muhimu kuliko zote katika Taifa lolote( kazi takatifu)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by HISIA KALI, Nov 29, 2011.

 1. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimesoma kwa makini mapendekezo ya CHADEMA. Kusema ukweli yamenikuna sana. Yamenikuna kwani yameweka masilahi ya Taifa la Tanzania mbele.

  Ni kweli suala la kutanga katiba mpya linahitaji uangalifu mkubwa na hekima ya kutosha. Kikubwa zaidi hili zoezi la kutunga katiba mpya linatakiwa liwekwe kwenye mikono ya wananchi wa Tanzania wenyewe.

  Ninajua pia hata kama tukisema utungaji wa katiba mpya ni wa wananchi wenyewe, si kweli kuwa kila mwananchi atashiriki kwa asilimia mia moja katika hili. Ila kuna baadhi ya wananchi ambao watapata nafasi kubwa ya kushiriki kikamilifu katika zoezi ili kama wawakilishi wa wananchi wengine.

  Hao wawakilishi watatakiwa kutambua kuwa wamepewa kazi kubwa na yenye dhamani kuliko kazi nyingine yeyote hapa nchini. Kwa kifupi wajue kwamba watakuwa wanafanya kazi ya kuandika msahafu wa Taifa la Tanzania ( Kitabu kitakatifu cha Taifa letu), Hivyo watatakiwa kuwa ni watu waadilifu na wazalendo wa kweli kweli, watu ambao watatakiwa kujitoa muunga kwa ajili ya Taifa lao. Masilahi mapana ya Taifa la Tanzania yatawekwe mbele kuliko kitu kingine chochote.

  Katiba mpya ndio itakuwa dira ya Taifa letu kwa miaka mingi ijayo. Hivyo mimi sioni haja ya kufanya haraka katika hili jambo. Viongozi wetu wa kisiasa na kijamii watakiwa kutumia hekima na ikibidi waombe miungu yao wapate hekima zaidi ili hili zoezi liendeshwe kwa umakini mkubwa.

  Masilahi ya Taifa yawekwe mbele kuliko wakati mwingine wowote ule.
   
Loading...