Kazi ya kuajiriwa ni utumwa tu

Kwema humu?

Kama tunavyojua maisha ni magumu sana huitaji wa kazi umekua mkubwa sana mtaani

Nimeahangaika nikapata ajira kampuni flani hivi nimepewa mkataba ndio kwanza miezi mitatu lakini hii kazi inaelekea kunishinda

Kazi haina mapumziko,haina overtime kitu kidogo kazini unakatwa pesa kwenye mshahara wako, unaingia kazini saa mbili asubuhi unatoka saa tatu au nne usiku ni kazi ya kupelekeshwa tu hata mkataba haufuatwi ila watu wanafanya kwakua hawana pakwenda bosi anafoka muda wote. Mimi binafsi najiandaa kusitisha mkataba wangu

Kama kuajiriwa ndio huku nimeshindwa acha nirudi sokoni kuuza mtumba

MAISHA MAZURI NA YAFURAHA YAPO UKIJIAJIRI TU
Haina haja ya kusitisha mkataba acha tuuu...bongo hakuna cha mkataba.
 
Suala la kuacha kazi ni maamúzi binafsi ya mtu, hivyo kama unaona ni bora kujiajiri ni vyema ukafanya hivyo ila sio kuja humu kuanz kutoa mapungufu ya mwajiri wako na kuona waajiri hawafahi wakat kuna watu wanakula good time na waenjoy kazi
 
Back
Top Bottom