Kazi ya kuajiriwa ni utumwa tu

bitebo7

JF-Expert Member
May 1, 2015
858
593
Kwema humu?

Kama tunavyojua maisha ni magumu sana huitaji wa kazi umekua mkubwa sana mtaani

Nimeahangaika nikapata ajira kampuni flani hivi nimepewa mkataba ndio kwanza miezi mitatu lakini hii kazi inaelekea kunishinda

Kazi haina mapumziko,haina overtime kitu kidogo kazini unakatwa pesa kwenye mshahara wako, unaingia kazini saa mbili asubuhi unatoka saa tatu au nne usiku ni kazi ya kupelekeshwa tu hata mkataba haufuatwi ila watu wanafanya kwakua hawana pakwenda bosi anafoka muda wote. Mimi binafsi najiandaa kusitisha mkataba wangu

Kama kuajiriwa ndio huku nimeshindwa 🙌 acha nirudi sokoni kuuza mtumba

MAISHA MAZURI NA YAFURAHA YAPO UKIJIAJIRI TU
 
Pole mkuu! Lakini sio kazi zote zipo hivyo kuna wengine wanarelax sana tu! We kuwa mvumilivu uitumie hiyo kazi kama gazi ya kupata kazi nyingine!

Watu husema kama unaona kazi kufanya kazi, Acha kazi uone ilivo kazi kupata kazi!

Uamuzi wa kuacha kazi usiuchukue kala ya kupiga hesau zuri za kujiajiri, vinginevyo utakujajutia!
 
Ni soko gani ilo unaenda mkuu. kumbuka kuna zoezi la wamachinga kupangiwa maeneo ya biashara nalo linaendelea
 
Una uhakika gani ,Mara nyingi mkikosa ajira ndo mnaanza vimaneno maneno acha watu walitumikie taifa lao
 
Una uhakika gani ,Mara nyingi mkikosa ajira ndo mnaanza vimaneno maneno acha watu walitumikie taifa lao
Uko sahihi kabisa sio kila mwajiri anatumikisha kama yeye anavyotymikishwa huko aliko bhana hizo n chuki binafsi kwa walioajiliwa
 
Sio ajira zote zipo hivyo ingawa ni kweli kwamba ukishakuwa mwajiriwa sehemu yoyote basi uhuru wako (freedom) unapunguzwa na muda wako wa kuwa kazini huwezi kufanya jambo jingine au kwenda kokote unakotaka wewe

Tafuta kitu kingine cha kufanya kama hiyo ya kuingia saa 2 asubuhi na kutoka nne usiku imekushinda. Bila shaka wote hapo hakuna anayefurahia hiyo ila ni kwamba hawaoni/hawana/hawajaamua choice nyingine kwa sasa
 
Back
Top Bottom