Kazi ya Kikwete ni kuhudhuria kila msiba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kazi ya Kikwete ni kuhudhuria kila msiba?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Phillemon Mikael, Feb 10, 2010.

 1. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #1
  Feb 10, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 9,248
  Likes Received: 2,937
  Trophy Points: 280
  mazishi

  [​IMG]
  waombolezaji kinamama msibani
  [​IMG]
  Wakuu wa wilaya za Kilimanjaro wakiwa msibani
  [​IMG]

  baadhi ya waombolezaji​

  Habari na picha na
  Dixon Busagaga,
  Same
  RAIS Jakaya Kikwete jana ameongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa mnikulu marehemu Rajabu Kianda aliyefariki dunia Februari 7 mwaka huu kwa ugonjwa wa shinikizo la damu.

  Akizungumza baada ya mazishi yaliyofanyika kijiji cha Kangokoro kata ya Kihuria wilayani Same,Rais Kikwete aliitaka familia ya marehemu kuwa wavumilivu na moyo wa subira hasa katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

  Naye katibu mkuu wa Ikulu Bw Michael Mwanda akisoma wasifu wa wa marehemu Kianda alimtaja marehemu kuwa alikuwa ni mchapa kazi hodari na kwamba ni mfano wa kuigwa..

  Kwa upande wake baba mdogo wa marehemu ,Bw Said Nyika akitoa neno la familia ameishukuru serikali kwa msaada iliyotoa wakati wa matibabu ya ndugu yao hadi mauti yalipomfika.

  Mazishi hayo pia yalihudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo wakuu wa wilaya,wabunge, viongozi wa vyama vya siasa, taasisi mbali mbali za serikali na zisizo za serikali.

  Marehemu Kianda aliyefariki dunia Februari 7 katika hospitali ya Muhimbili ,amezikwa katika makaburi ya familia yaliyopo eneo la Mashine kata ya Kihurio na ameacha mjane na watoto sita.


  SOURCE: Michuzi Blog
   
 2. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2010
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Mbona umetoa habari kwa Michuzi bila ku acknowledge
   
 3. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  yes me nadhani ni moja ya jukumu kubwa la rais....sio misiba tu kuwajulia hali wagonjwa pia katika hospitali mbalimbali
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  Feb 10, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  pamoja na madhaifu aliyoyasema Semenya, kweli Kikwete ni Bigwa wa kuudhulia misiba, anajitahidi, sijui ni sifa ama ni ujiko.
   
 5. B

  Bull JF-Expert Member

  #5
  Feb 10, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rais lazima awe karibu na watu ni sehemu ya majukumu yake, kama kuhudhuria kwa raisi msibani wewe kumekukweza, waliofiwa, jamaa na marafiki wanafarajika
   
 6. M

  Mundu JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,720
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sio kila msiba ndugu! mingine kama kweli ameguswa, basi awatume viongozi wake wasaidizi kama vile DC, RC n.k wamwakilishe. Anatuletea adha kubwa sana ya foleni hasa wakazi wa Dar.

  Wajua tena msafara wa raisi ukipita, magari mengine yote husibiri kwa masaa zaidi mawili kwenye foleni. Madhara yake hata kiuchumi ni makubwa pia!
   
 7. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #7
  Feb 10, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 9,248
  Likes Received: 2,937
  Trophy Points: 280

  rais hakuwa na sababu ya kwenda kuzika same kwa huyu afisa usalama aliyefariki..kwani kitendo cha rais na mkewe kufika pale mikocheni nyumbani siku ya kuaga mwili wa marehemu...na kwakuwa inajulikana rais ni mtu mwenye mamlaka na kazi nyingi....kile kitendo pekee kilitosha kuonesha upendo wake kwa maafisa wake wanaomlinda na kumsaidia kazi......lakini bado tena amesafiri na kutumia siku nyingine nzima kwenda kuzika same......urais ni cheo kikuu sana ....ingetosha kumtuma mkuu wa mkoa au waziri wa utawala bora ..amuwakilishe kama kweli aliona ...inafaa.....

  the president wants to win peoples emmotions at all time....that may not be possibe!!
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,541
  Likes Received: 1,529
  Trophy Points: 280
  ulitegemea nini kuwa na raisi mkwere
   
 9. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,143
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Watu bwana!!! Kweli uongozi kazi, hivi Rais kuhudhuria msiba ni kutaka sifa? Kwakweli unachekesha. Rais ni kama mtanzania mwingine yeyote ambaye anaguswa na kifo cha mtu ambaye ama alikuwa anafahamiana naye kwa karibu au ni ndugu au rafiki wa karibu bila kujali nafasi yake serikalini. Kama ambavyo wewe huwa unaomba Ruhusa ili kwenda kwenye msiba na yeye ana nafasi ya kufanya hivyo. Mbona tupo hivyo watanzania?? Tunaacha kuangalia mambo ya msingi tunaanza kujadili mambo ambayo ni too personal!! Wewe unafahamu Kikwete na huyo bwana wanamahusiano gani? Tuache ushabiki unaopitiliza kiasi. hata kama ni kumchukia lakini siyo kihivyo.
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,541
  Likes Received: 1,529
  Trophy Points: 280
  yaani huyu anaona aibu tu kwenda ngomani lakini ingekuwa amri yake aaaah ..ngomanai kama kawaaa
   
 11. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #11
  Feb 10, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kuna rafiki yangu ni bingwa wa hesabu na siku moja nilikuwa nae ktk porojo zake akaanza kukokotoa mambo yanavyofanyika pale ikulu na Mh wetu, akasema tufanye pale ikulu kuna masomo 5 na kama yeye angekuwa mwalimu angetowa marks hizi, sijui mimi na wewe tungetowa zipi?
  1. Kuhudhuria misiba na mazishi - 86%
  2.Safari za Nje -89%
  3. Safari za Ndani- 61%
  4.Kukaa ofisini- 15%
  5. Msimamo katika vita ya ufisadi- 05%
   
 12. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #12
  Feb 10, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,541
  Likes Received: 1,529
  Trophy Points: 280
  hakuwa na sababu ya msingi kusafiri kwenda same kuhudhuria msiba ambao angeweza kumtuma mwakilishi na yeye akatulia ofisini kufanya kazi.ndo shida ya kula miguu ya kuku wakati wa utoto madhara yake ndo hayo sasa yanaonekana ukubwani..
   
 13. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #13
  Feb 10, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,301
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Jamani chaguo la Mungu huyo vile vile ni mtu wa watu!
   
 14. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #14
  Feb 10, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,541
  Likes Received: 1,529
  Trophy Points: 280
  kukaa ofisini ni 1.2%
  safari za nje 98.7
  kuhudhuria mazishi ni 100%
   
 15. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #15
  Feb 10, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  umesahau kukaribisha watu dinner IKULU 100%
   
 16. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #16
  Feb 10, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 9,248
  Likes Received: 2,937
  Trophy Points: 280
  juzi alitumia masaa mawili kwenda kuaga marehemu mikocheni ....jana siku nzima hajafanya kazi...kisa anazika....,ukishakuwa rais kuna vitu unapoteza...kimoja ni kuwa hata muda wa rais ni mali yetu!..asiufisadi muda wetu tuliompa! alaaa!
   
 17. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #17
  Feb 10, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Kuhudhuria misiba hakudetermine ubora au ubaya wa kiongozi,hiyo ni culture ya kawaida kabisa,hata kama angeudhuria kila msiba wa wilaya ya Ilala sisi tunachojali anaifanyia nini Tanzania.Sometimes muwe mnapunguza kauli za kubeza.
   
 18. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #18
  Feb 10, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,456
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kikwete: Tumaini Lililopotea
   
 19. M

  Magehema JF-Expert Member

  #19
  Feb 10, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 449
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Staha kwa Mheshimiwa Rais tafadhali!
   
 20. bht

  bht JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  jamani nisaidieni mnikulu ni cheo gani??
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...