Kazi ya CHADEMA kanda ya ziwa imenibariki sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kazi ya CHADEMA kanda ya ziwa imenibariki sana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kweleakwelea, Feb 28, 2011.

 1. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,419
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  Frederick Katulanda, Butiama
  MJANE wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, jana aliwaombea dua njema kwa Mungu, viongozi wakuu wa Chadema huku mtoto wake, Madaraka Nyerere, akikitabiria chama hicho kupata ushindi wa kura milioni sita dhidi ya kura milioni nne za CCM, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 .

  Hatua hiyo inakuja wakati viongozi wa chama hicho cha upinzani, wakiwa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, kuendesha maandamano ya kuishinikiza serikali, isilipe tuzo ya Sh94 bilioni kwa Kampuni wa Dowans.

  Tuzo hiyo imetolewa na Mahakama ya Kimatafa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara, baada ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuvunja mkataba kati yake na Dowans.
  Maandamano ya Chadema katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, yamekuwa yakiungwa mkono na maelefu ya wananchi.

  Jana maandamano hayo yalifanyika katika Kijijni cha Butiama, Musoma Vijijini alikozaliwa na kuzikwa mwasisi wa taifa la Tanzania Mwalimu Julius Nyerere.Viongozi wa chama hicho na baadhi ya wananchi, walikwenda kwenye kaburi la kiongozi huyo, ili kuomba dunia.

  Akizungumza mbele ya kaburi hilo, Mama Maria aliomba akisema "mtumishi wa Mungu, tazama hawa viongozi wanaokuja mbele yako, wanafanya kazi, tunakuomba kila mmoja wao umwezeshe kutambua kuwa yeye ni mtumishi wa watu tu."


  Hata hivyo, jukumu la kuzungumza alipewa Madaraka ambaye alisema aliposikia habari kuhusu maandamano, hakuelewa vizuri, lakini sasa ametambua na kuamini kuwa hilo ni jambo jema.

  Madaraka alisema kwa muda mrefu amekuwa akikitambua chama tawala na kwamba alikuwa hawajui Makongoro na Mbowe akimaanisha kuwa taifa halikuwa na ubaguzi wa dini wala ukabila.Alisema hata hiyo sasa ameanza kutambua na kuona tofauti.

  "Kazi ya upinzani ni kusaka kura. Nilisikia katika uchaguzi uliopita kuwa watu walipiga kura na wengine hawakupiga kura. Sasa nadhahi mwaka 2015 watakaopiga kura watakuwa milioni 12 na CCM watapata kura milioni sita lakini, Chadema wao watapata kura milioni sita. Hizi nyingine milioni mbili zitakuwa za watu ambao hawatapiga kura," alisema Madaraka.

  Madaraka pia ni mume wa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chadema, Leticia Nyerere.

  Kabla ya kuchaguliwa mbunge wa viti maalumu, Leticia aligombea ubunge katika Jimbo la Kwimba, lakini alibagwa Shanif Mansoor wa CCM.

  Mbali na Leticia Nyerere, Chadema ina mbunge mwingine kutoka katika familia ya Baba wa Taifa, anayejulikana kwa jina la Vicent Nyerere. Vicent ni mbunge wa kuchaguliwa katika Jimbo la Musoma Mjini.

  Madaraka alisema kwa sasa hana shaka na Chadema kwa sababu chama kinakubalika kwa wananchi na kwamba hiyo inatokana na jinsi viongozi wanavyojipanga.


  Alisema kujipanga huko ni pamoja na kupita mikoani wakitetea wananchi na kunadi sera.

  Madaraka alisema wakati fulani hakuelewa mantiki ya wabunge wa Chadema, kususia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, lakini sasa anajua.

  "Lengo lenu ni zuri, unaweza kuwa na lengo zuri sana lakini likapotoshwa kwa makusudi. Kwa hiyo mkipita kuwapambanulia wananchi, wataelewa tu," alisema Madaraka.

  Katika Kijiji cha Butiama, wabunge hao na viongozi wa Chadema, walikaribishwa na mtoto mwingine wa hayati baba wa taifa Makongoro Nyerere, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara.

  Baada ya kupokewa na Madaraka Nyerere, walisalimiana na Mama Maria Nyerere na baadaye Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alimshukuru kwa kuwakaribisha Butiama.

  "Tunakutakia mema, tunakuomba utuombea, tunaomba utuunge mkono pale panapotakiwa, taifa letu bado linaitegemea familia yenu," aliomba dua Mbowe.

  Akizungumza baada ya kumalizika kwa sala katika kaburi la Baba wa Taifa, Katibu Mkuu wa chama hicho,Dk Willbroad Slaa, alisema kwa sasa kanisa liko katika mchakato wa kumtangaza Nyerere kuwa Mtakatifu.

  Dk Slaa alitilia mkazo mchakato huo akiwataka Watanzania kuombea suala hilo ili likamilishwe kwa wakati uliopangwa.

  Leo maandamano hayo yaliyoanza jjini Mwanza juzi, yataelekea katika Mkoa wa Kagera.


  Familia ya Nyerere yawapongeza CHADEMA

  Na Suleiman Abeid, Butiama

  VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana walitembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambako walipewa
  matumaini kuwa wanaweza kuibuka na ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 na kuongoza nchi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 50 ya uhuru.

  Ubashiri huo umetolewa jana kijijini Butiama na mmoja wa watoto wa hayati baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Bw. Magige Kambarage alipokuwa akitoa shukrani zake kwa viongozi wa CHADEMA waliokuwa wamekwenda kijijini Butiama kuzuru kaburi la hayati baba wa Taifa na kumjulia hali mjane wake, Mama Maria Nyerere.

  Msafara wa viongozi wa CHADEMA ukiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa uliwasili kijijini Butiama saa 6.00 mchana jana na kupokewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mara, Bw. Makongoro Nyerere ambaye pia ni mmoja wa watoto wa hayati baba wa taifa.

  Akiukaribisha msafara huo uliojumuisha wabunge mbalimbali wa chama hicho, Bw. Makongoro aliupongeza ujumbe huo kwa kuona umuhimu wa kufika Butihama, na hasa nyumbani kwao, kuwajulia hali na kutembelea kaburi la marehemu baba yao, kwa kuwa siasa si uadui.

  Baada ya kutembelea kaburi hilo na kuweka mashada ya maua, Bw. Kambarage aliwapongeza viongozi wa CHADEMA kwa uamuzi wao wa kuendesha maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima ili kuzungumzia mstakabali wa Taifa la Tanzania.

  Kugombana ndani ya siasa ni ujinga tu ndiyo unaotusumbua, mimi nasema kitendo hiki cha maandamano mlichokifanya ni kitendo kizuri sana, pamoja na kwamba mimi ni mwanachama wa CCM, lakini nakupongezeni,[FONT=&quot]�[/FONT] alisema.

  Hizi safari za kutembea kwa miguu na kushirikiana na wananchi ni kitu muhimu, eleweni kwamba mna dhamana kubwa hivi sasa mbele ya umma wa Tanzania, kwani ninyi ndiyo kambi kuu ya upinzani hapa nchini, fanyeni kazi msije mkapoteza dhamana mliyokabidhiwa na wananchi, umma umeishawakubali,â€[FONT=&quot]�[/FONT] alieleza Bw. Kambarage.

  Alisema katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana, watu wengi hawakujitokeza kupiga kura, lakini wapo zaidi ya milioni 20 wenye haki ya kupiga kura, ambapo aliwataka viongozi hao wa CHADEMA wafanye kazi kubwa ya kuwatafuta waliko ili ifikapo mwaka 2015 waweze kupiga kura.

  Mimi nasema hawa ambao hawakupiga kura wapo wengi sana, watafuteni waliko, 2010 CCM tulipata kura milioni tano za urais, lakini naamini mkiwatafuta hawa waliopotea, katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015 CHADEMA mtazoa zaidi ya kura milioni sita na CCM tutaambulia kura milioni nne, naamini hivyo,[FONT=&quot]�[/FONT] alieleza Bw. Kambarage.

  Alisema moja ya kazi wa vyama vya upinzani nchini ni kuwainua watanzania katika mambo ambayo serikali iliyoko madarakani imeshindwa kuwatekelezea na kwamba hivi sasa Watanzania wameishakikubali chama cha CHADEMA na ndiyo maana wanakiunga mkono badala ya CCM," nakuombeeni Mungu aibariki kazi yenu,[FONT=&quot]�[/FONT] alisema.

  Awali, mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe alimweleza mama Maria Nyerere kuwa lengo la ziara yao hiyo ni kumjulia hali yeye na familia yake, kudhuru kaburi la hayati baba wa Taifa na kuomba dua katika kaburi lake ikiwa ni katika kuenzi heshima aliyokuwa nayo katika Taifa la Tanzania.

  Nachukua fursa hii kukushukuru kwa heshima kubwa uliyotupatia ya kukubali kuja kukujulia hali pamoja na kutembelea kaburi la hayati baba wa Taifa, tunasema hii ni heshima kubwa kwetu sisi CHADEMA wakati tukiwa katika mkoa wa Mara kuendesha maandamano ya amani na mikutano ya hadhara kuzungumzia mstakabali wa taifa letu,

  Tunaomba utuombee kwa Mungu ili tuweze kufanya kazi zetu vizuri na ikibidi kutuunga mkono, basi utuunge katika lolote lile ambalo tutahitaji kuungwa mkono na wewe, lengo letu ni moja tu kuwatumikia Watanzania ili waweze na kufaidi matunda ya uhuru wa nchi yetu,[FONT=&quot]�[/FONT] alieleza Bw. Mbowe.

  Kwa upande wake mama Maria Nyerere aliwashukuru viongozi hao wa CHADEMA kwa uamuzi wa kumtembelea ili kumjulia hali ambapo aliwaombea kwa Mungu aweze kuwapa afya njema na waendelee kuwatumikia wananchi kwa haki bila ya upendeleo wowote.

  Akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Musoma na vitongoji vyake katika viwanja vya Shule ya Msingi Mukendo juzi, Bw. Mbowe alisema chama hicho hakina mpango wa kumchukulia hatua Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi mkoani Shinyanga, Bw. John Shibuda kwa vile kinaamini hakijawa na mgogoro naye.

  Bw. Mbowe alilazimika kutoa ufafanuzi huo wa kuhusiana na Bw. Shibuda baada ya kutakiwa na wananchi aeleze nini hatma ya mbunge huyo ambaye amekuwa akionesha dalili za kupingana na maelekezo ya chama mara kwa mara.

  Mwenyekiti huyo alijikuta akiulizwa swali hilo mara baada ya yeye kutoa ufafanuzi wa kitendo cha spika kubadili kanuni za bunge na kutaka kuilazimisha CHADEMA kuungana na vyama vingine kuunda kambi ya upinzani bungeni, wananchi hao walipiga kelele wakisema, na Shibuda, Shibudaaaa.

  Kutokana na kelele hizo, Bw. Mbowe alilazimika kuwauliza wananchi hao iwapo walikuwa wakimtaka Bw. Shibuda aongee nao, nao walijibu kwamba wanachohitaji ni yeye kutoa ufafanuzi kuhusiana na madai ya kutaka kupingana na viongozi wake ndani ya CHADEMA.

  Bw. Mbowe aliwaeleza wananchi kwamba Bw. Shibuda hana tatizo lolote ndani ya chama na kwama mambo yaliyokuwa yamejitokeza ni mambo madogo madogo ambayo hayawezi kusababisha mbunge huyo kufukuzwa ndani ya Chama.

  Ndugu zangu napenda nikufahamisheni wazi kuwa tupo humu ndani ya vyama vya siasa kwa sura na tabia tofauti, inaweza kutokea Bw. Shibuda akashindwa kuelewana lugha na Bw. Wenje, huu huwezi kuuita kuwa ni ugomvi, ni kutofautiana kwa lugha tu ni suala la kibanadamu, ninachowaomba, tuvumiliane, Bw. Shibuda bado ni mwenzetu,[FONT=&quot]�[/FONT] alieleza Bw. Mbowe.

  Bw. Mbowe aliwaeleza wananchi hao kuhusiana na suala la msimamo wa CHADEMA kukataa kushirikiana na vyama vingine vya upinzani ndani ya bunge kwa vile baadhi ya vyama hivyo havina msimamo kutokana na vingine kufunga ndoa na Chama cha Mapinduzi (CCM).

  Aidha alieleza kushangazwa kwake na huruma ya machozi ya mamba kwa binadamu iliyooneshwa na Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda ndani ya bunge kwa kuvitaka vyama vya upinzani kushirikiana kwa lengo la kuwa na nguvu imara, kitendo ambacho alisema si huruma ya kweli.

  Ndugu zangu haiwezi kutokea hata siku moja, adui yako akakupa ushauri wa jinsi ya kupata nguvu ili uweze kumteketeza kama alivyojaribu kufanya spika wetu wa bunge. Huyo anadai wapinzani tuungane ili tuwe na nguvu bungeni, si kweli maana tukiwa na nguvu zaidi tutakishinda chama chake.

  Hizi zilikuwa ni mbinu tu za CCM katika kujaribu kusambaratisha upinzani hapa nchini, lakini sisi CHADEMA tumekataa na kubaki na msimamo wetu, hata mawaziri vivuli wote wanatokana CHADEMA, bado tunawapima hawa wenzetu ili tuone kama kweli wana dhati ya kuwa wapinzani dhidi ya CCM, alieleza Bw. Mbowe.

  DK SLAA ATIBUA MAMBO KWA WASSIRA

  Anthony Mayunga, Bunda na Frederick Katulanda, Butiama  [​IMG]
  ALIYEKUWA mgombea ubunge wa ubunge kwa tiketi ya Chadema jimbo la Bunda Elias Maarugu ametimuliwa kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho uliohutubiwa na katibu mkuu Dk Wilbroad Slaa baada ya kukataliwa
  na wananchi kwa madai kuwa alihongwa na kumwachia Stephen Wasira.

  Dalili za kumkataa Maarugu zilianza mapema mara baada ya kuitwa asalimie wananchi mjini Bunda, umati mkubwa wa wananchi ulipiga kelele na kudai hawataki kumsikiliza kwa kuwa aliwasaliti na kuuza haki zao.

  Wananchi hao walipiga kelele wakisema hawako tayari kumsikiliza huku wakimtaka atoke jukwaani kwa kuwa hafai, "hatumtaki huyo mtoeni hapo aliuza kura, alihongwa msaliti hafai mtoeni hatutaki kumsikiliza.”

  Kelele hizo zilisikika sauti kwa nguvu za wananchi waliojaza uwanja wa stendi ya zamani.

  Licha ya Maarugu kujikakamua na kusema Peoples, wananchi walipaza sauti na kumtaka atoke haraka sana," hatutaki kumsikiliza huyo mtoeni huyo hafai msaliti alikuwa wapi kwanini amekuja leo siku zote alikuwa wapi?”walihoji.

  Kutokana na kelele na wananchi kugoma kumsikiliza Dk Slaa alilazimika kuingilia kati na kusema kuwa, "sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, hivyo kama umma wote huu unakukataa ndugu yangu Maalugu kuna kitu naomba utueleze kwa nini watu hawa wanakukataa.”

  Hata hivyo katibu mkuu huyo kuwataka wananchi wawe na subira wananchi waliendelea kugoma na kusema kuwa hawako tayari kumwona wala kumsikiliza hivyo wakamtaka atoke eneo hilo.

  “Maarugu Chadema inapinga ufisadi ndani na nje ya chama kama unatuhumiwa wewe ni mtu mzima na kuheshimu sana nakuomba uamke taratibu uage uende kwako na sisi tunakuchunguza, natamka kuanzia sasa kuwa nakufutia ugombea wa miaka mitano ijayo kwa kuwa hufai maana nakataliwa na wananchi, nitatoa taarifa kwenye kamati tendaji ya chama,”alisema.

  Kutokana na kauli hiyo Maarugu ambaye aliwahi kuwa mkuu wa wilaya ya Magu na Misenyi alilazimika kushuka taratibu huku akizomewa na maelfu ya wananchi waliokuwa wamefurika hapo,huku Dk Slaa akiwasihi wananchi wasimpige,kumtukana kwa kuwa suala lake bado linachunguzwa na wananchi watapewa majibu.

  Aliagiza kamati tendaji ya chama wilaya kuketi haraka kujadili kisha kutoa taarifa kwake ndani ya wiki mbili, na kama wataridhika nayo wataifanyia kazi,vinginevyo watalazimika kuunda kamati maalumya kufuatilia kwa kuwahoji wananchi wa jimbo hilo.

  Mapema Mkurugenzi wa mambo ya Bunge na halmashauri wa chama hicho John Mrema alisema kitendo hicho hakipaswi kuvumiliwa hata kwa viongozi wengine wa chama hicho na kuwa chadema mambo yao yako wazi.

  Wakati huo huo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amekataa madai ya wakazi wa Tarime kudai kuwa kura zao zilichakachuliwa na CCM kushinda Ubunge katika jimbo hilo.

  Akizungumza jana katika uwanja wa mpira wa barabara ya Nyamwaga, mwenyekiti wa Chadema, alisema hakubaliani na hoja za watu kusingizia chama chake kilishindwa uchaguzi kutokana na kuchakachuliwa kura bali mgawanyiko wa ndani.

  Alisema katika kipindi cha uchaguzi alifika Tarime na kukaa kikao na viongozi wa chama chake Tarime na kubainisha kuwa katika kikao hicho aliwaeleza wazi kama hawajui kushindwa uchaguzi na kama wamesahau kutawaliwa na CCM basi wajue kuwa watajifunza pale ambapo kiti cha ubunge kitakapo ondoka.

  “Niliwaeleza katika kikao cha ndani kama hawajui hathari za ubinafsi basi watajifunza pale watakapopoteza kiti cha Ubunge, niliwaeleza kuwa mtajifunza pale mtakapotawaliwa na CCM. Sasa kuniambia kuwa kura zilichakachuliwa nakataa…sababu naijua,” alieleza Mbowe ambaye alionekana kukasirika.

  Mwenyekiti huyo ambaye ni kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, alisema ingawa alitambua mpasuko huo, yeye akiwa kiongozi wa chama mwenye dhamana ya kupitisha majina ya wagombea, walipoletwa waliogombea waliwapima kwa vigezo na kuamua kulirudisha jina la Waitara Chacha.

  “Leo nalisema hili ili mjue kuwa pale ubinafsi unapotawala katika harakati za ukombozi ni hatari sana…, Mwera alikuwa anataka kuwa mbunge, Waitara, Heche na Matage, wote hawa waliutaka ubunge lakini hawawezi kuwa wote ni lazima ashinde mmoja,” alifafanua.

  Alisema kuwa kila mmoja anayo haki ya kugombea ubunge lakini inapofikia kila mmoja anataka kushinda hapo ndipo inapokuwa ngoma.  SLAA ALIPUA MABOMU​
  Frederick Katulanda na Anthony Mayunga, Musoma

  [​IMG]  Katibu mkuu wa Chadema Dk Willibroad Slaa akihutubia umati wa watu waliofurika katika uwanja wa Mkendo mjini msoma jana katika muendelezo wa maandamano ya chama hicho nchi nzima yalioanzia mkoani Mwanza alhamisi wiki hii.
  MAANDAMANO ya Chadema yameingia mkoani Mara na kuuteka mji wa Musoma huku Katibu mkuu wa chama hicho, Dk Wilibroad Slaa, akitoboa siri ya kulipuka kwa mabomu ya Gongo la Mboto na Mbagala.

  Naye Mwenyekiti Chadema taifa, Freeman Mbowe aliitahadharisha Serikali kuwa taifa litaingia kubaya iwapo mchakato wa mabadiliko ya katiba utachakachuliwa kwa maslai ya mafisadi.

  Akizingumza jana katika Uwanjwa wa Mukendo mjini Musoma baada ya maandamano ya kilomita 15 kutoka Bweri hadi mjini, Dk Slaa alisema kulipuka kwa mabomu hayo kumetokana na Serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete kupuuza ombi la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuwapa fedha kwa ajili ya kuteketeza mabomu yaliyokwisha muda wake.

  Alisema kazi ya jeshi ni kulinda uhai wa watu wake nchini, lakini kupitia jeshi taifa limeweza kupoteza watu zaidi ya 40 kutokana na serikali kugoma kutoa fedha hizo ambazo ziliombwa na JWTZ.

  “Tunataka Kikwete atueleze kwa kina kama ni kweli, maana tunaambiwa kabla ya mabomu kulipuka mwaka 2009 JWTZ (Mbagala) waliomba fedha kwa ajili ya kuteketeza mabomu, lakini kutokana na serikali kutothamini maisha ya watu wake ilikataa kuwa hakuna fedha.

  "Tunaambiwa tena kuwa kabla ya mabomu haya ya mwisho kulipuka wanajeshi waliomba fedha serikalini kwa ajili ya kuteketeza mabomu hayo, lakini pia serikali hiyohiyo haikutoa kwa madai kuwa hakuna fedha,” alieleza Dk. Slaa.

  Kwa sababu hiyo akamtaka
  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi alijiuzulu.

  Dk Slaa alisema kuwa Watanzania wanataka Waziri Mwinyi afuate nyayo za baba yake kama ambavyo alijiuzulu kwa mauaji ya polisi mkoani Shinyanga na kwamba asipofanya hivyo baada ya siku tisa kuisha Chadema watatangaza hatua ya pili kwa ajili ya kumshinikiza ajiuzulu.

  Onyo kuhusu Katiba

  Akizungumza katika mkutano huo uliokuwa umefurika watu, Mweyekiti wa chama hicho, Mbowe alitahadharisha kuwa serikali ya CCM itaingilia na kuvuruga mchakato wa katiba kwa maslai yake binafisi, basi "Tanzania patachimbika kama Tunisia na Misri."

  Hata hivyo, Mbowe alisema kwa muda sasa amekuwa akishangazwa na kauli za Rais Kikwete ambazo zimekuwa zikidai kuwa nchini kuna udini akisema hizo ni propaganda zake.

  Alisema kama kweli Kikwete anauhakika juu ua jambo hilo basi anapaswa kuwachukulia hatua wahusika.

  Kabla ya mkutano huo viongozi hao waliwaongoza wananchi wa Musoma kuandamana umbali wa kilomita 15 wakitembea kupinga ugumu wa maisha na kulipwa kwa Dowans.


  “Tutaendelea kuandamana mpaka maskini wa Tanzania asikilizwe. Tutaandamana mpaka vijana wa kitanzania wapate ajira na hatutalala mpaka kieleweke,” alisema Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia.

  Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje alisema vijana wengi wanafanya kazi za umachinga kwa sababu ya mfumo mbovu uliowekwa na serikali unaowafanya wakose ajira.

  “Musoma kulikuwa na kiwanda kizuri sana cha Mutex kilichokuwa kinatoa ajira kwa vijana, lakini kwa uzembe na ujanja wakawapa watu kwa madai ya kubinafsisha. Sasa kimefungwa hakuna ajira kwa vijana na matokeo yake ndiyo wamachinga ambao wanapigwa mabomu kila wakati,” alisema Wenje na kuongeza.

  “Kuna kila sababu ya kutafuta haki kwa njia mbalimbali. Andamaneni mpaka haki yenu ipatikane."


  Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi alisema Wamarekani wana msemo kuwa anayehifadhi magaidi naye ni gaidi, hivyo wasanii wanazunguka na CCM na kuimba kuwa nchi hii ina amani nao ni wasaliti.

  Mbunge wa Kawe, Halima Mdee alisema pamoja na kuwa jimbo lake linakaliwa na vigogo wote wa nchi hii, lakini mwaka jana walifikia hatua ya kuikataa CCM.

  “Kama Kawe wamesema CCM baibai inakuwaje ninyi watu wa Mara. Nawaambieni kuwa mwaka 2015 majimbo yote saba yanatakiwa yachukuliwe na Chadema na kuingia Ikulu, maana sisi tumewaahidi kupambana na ufisadi mpaka mwisho," alisema.

  Utetezi wa Mbunge Lema

  Dk Slaa alizungumzia pia kitendo cha Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kutakiwa kuwasilisha ushahidi kwa madai yakuwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alidanganya bungeni hivi karibuni.

  Dk Salaa alisema kuwa tayari amewasilisha ushahidi na kwamba unaonyesha wazi kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alidanganya mara 23 bungeni kuhusiana na suala la mauaji ya Arusha.

  “Spika aliomba ushahidi Lema kapeleka, lakini kwa sababu alitaka kumlinda Pinda akasema kuwa ushahidi huo upelekwe kwake.

  "Lema ameitwa muongo hadharani na ushahidi aliowasilisha umebainisha Pinda ndiye alidanganya mara 23, sasa tunataka apewe nafasi hadharani bungeni auseme ushahidi wake katika kikao cha bunge lijalo Aprili,” alidai Slaa.

  MY TAKE:


  1. CHADEMA SASA NDIYO KIMBILIO LA KIZAZI HIKI NA KIJACHO! KIMSINGI CHAMA KIMEKUBALIKA.


  1. CHADEMA SASA IMEKUWA TAASISI IMARA NA YENYE KUHESHIMIKA. NI VYEMA TUKAWAPONGEZA VIONGOZI NA WANACHAMA WAKE WOTE KUWEZA KUHIMILI MISUKO SUKO INAYOTOKANA NA RAPID EXPANSION!


  1. FAMILIA YA NYERERE IMEENDELEA KUONYESHA UWEZO WAKE WA KUWA THE LEADING FAMILY (ROYAL) KWA TAIFA. IMETEKELEZA WAJIBU WAKE KWA USAHIHI. SALA YA MAMA YETU MARIA KWA BABA NYERERE IMEONYESHA UCHAJI WA HALI YA JUU, USAHIHI WA HALI YA JUU NA WAKILISHI HALISI WA MAWAZO YA MTANZANIA CHANYA.


  1. RESPONSE YA MBOWE NA CHADEMA INAONYESHA UNYENYEKEVU WA HALI YA JUU KWA BABA YETU, WACHILIA MBALI CCM WANAOKWENDA KUZURU KABURI NA KUMSANIFU MAREHEMU BABA WA TAIFA. HAKIKA NINA WASIWASI MKUBWA KILA VISIT YA VIONGOZI WA CCM AMBAO WANATENDA KINYUME KABISA NA FIKRA NA NJOZI ZA MWALIMU HUWA WANAMKERA SANA HUKO ALIPO NA PENGINE MAMA NYERERE HUKOSA USINGIZI NA KUPATA MAJINAMIZI THEREAFTER. USINGIZI ALIOUPATA JANA UTASIMULIWA KATIKA HISTORIA!


  1. MIMI BINAFSI NAISHUKURU SANA CHADEMA KWA PROGRAMU HII. IMEHUISHA SANA UMMA WA WATANZANIA NA KUWAKATA NGEBE NA KIBURI WENZETU WA CCM. BINAFSI AMANI NILIYOIPATA LEO INANIWEZESHA KUFANYA KAZI ZANGU KWA UFANISI BAADA YA KUSTAGNATE KWA MUDA MREFU! – SINCE GENERAL ELECTION


  1. INAWEZA TUSIJUE KILICHOTOKEA LAKINI KUZURU KABURI LA BABA WA TAIFA KUMETIA SANA LEGITIMACY NA BARAKA KWA CHAMA –KIIMANI NA KIUTAMADUNI!


  1. MUNGU IBARIKI CHADEMA! MUNGU IBARIKI TANZANIA!
   
 2. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kuwa maelezo ni marefu lakini ni matamu sana. Ukilinganisha maelezo haya na hotuba ya JK,maneno ya Wassira,Sophia Simba,Mrema,Cheyo na blabla zingine kuhusu maandamano ya wananchi (sio Chadema) utaona utofauti wa uelewa wa watu (viongozi) juu ya nchi yetu. Chadema mwendo mdundo mpaka kieleweke.
   
Loading...