Kazi ya BOT ni nini? Shilingi yazidi kuporomoka, sasa $1=Tsh. 1,500 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kazi ya BOT ni nini? Shilingi yazidi kuporomoka, sasa $1=Tsh. 1,500

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Brooklyn, May 20, 2010.

 1. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Hivi jamani BOT wameshindwa ku intervene forex market?

  Ndani ya siku 26 tu, shilingi imeporomoka kutoka Tsh 1360/US$ kufikia Tsh1492/US$.

  Katika hili kazi ya BOT ni nini?

  Mbona wenzetu wa Kenya shilingi yao imekuwa stable sana for the past 7 years.

  Tatizo nini hapa kwetu? Je turudi kwenye mfumo wa ku control unnecessary importations ili tuweze kusave vidola vichache tunavyovipata kutokana na exports?

  Wadau na wataalamu wa masuala ya uchumi tusaidiane katika ili!!
   
 2. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mfumo mzima wa fedha hapa kwetu ni mbovu!

  Unaweza kununua na kuuza dollar kadri unavyotaka na hamna mtu atakae kuuliza. CBA pekee ndio nimeona wanacontrol haya mambo.

  Wafanyabiashara wanaweka bei za bidhaa zao interms of USD unategemea nn?! Yaani mtalii akitoka kwao haitaji kununua shilling coz atanunua kila kitu kwa USD na serikali imeridhika kabisa na huu utaratibu, mpaka TRA wanacharge interms of USD. Kwao ni sawa tu!

  Katika mazingira kama hayo usitegemee shillingi kuwa strong, it'll always be weak.
   
 3. d

  damn JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tatizo BOT ni kiota cha mbayuwayu!!!
   
 4. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  inatisha na tusipoangalia tutakuwa kama\ zimbabwe
   
 5. L

  Losemo Senior Member

  #5
  May 20, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijui kama wizara ya fedha ina viongozi. Hali hii inatisha. Tuna viongozi vipofu wasioona kinachtokea. Mungu ibariki TZ
   
 6. B

  Bobby JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Viongozi wako kwenye kampeni mkuu. By the way mimi wala sishituki kwani ninamfahamu vizuri mkullo so sikutarajia miujiza kutoka kwake. Na huyo profesa wa BOT yeye anachojuwa ni kudemand nyumba yenye swimming pool tena ya bilioni mbili . Hiyo shilingi ikiporomoka hata ikawa kama zim dollar si issue kwake. Unajuwa bado mimi napata tabu sana kwamba kitu gani tulimkosea Mungu kiasi cha kutupa adhabu kubwa kiasi hiki cha kukosa serikali? Kila kitu kiko kwenye auto pilot jamani Mungu tuonee huruma tunaangamia kwa kweli.
   
 7. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Inasikitisha sana...juzi nimeingia kiji restaurant kimoja pale Mbezi, kuangalia Menu naona bei zote ziko in terms of Dollar!!

  - Nyumba za kupanga zinapangishwa kwa Dollar
  - Mikopo benki inatolewa kwa dollar
  -Madada poa wana quote bei zao kwa dollar
  -TRA wanacharge kwa dollar
  .....bado kidogo tu hata mikate ya bakharesa tutanunua kwa dollar.....

  Wapi Mkullo na Prof Ndullu???
   
 8. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Iiii...a-a-a...hii..aaah..ah..ah... Hiki ni kilio tu wandugu...
  Kuna wimbo mmoja tuliimba Primary..
  >>Tanzania..Tanzania...
  >>Nakupenda kwa moyo wote..
  >>Nchi yangu Tanzania
  >> Jina Lako ni tamu sana...

  >Nilalapo nakuota wewe.
  >Niamkapo ni heri mama wee..!
  >Tanzania Tanzania
  >Nakupenda kwa moyo wote..

  Kwanza nikiufikiria huu wimbo namkumbuka Mwalimu Nyerere na Uzalendo wake.
  Pili najiuliza..'' HIVI HUU WIMBO BADO UNAWEZA KUIMBIKA SASA??...

  Labda uimbike Hivi;

  Tanzania Tanzania
  Wakuponda kwa Moyo wote
  Nchi yangu Tanzania
  Jina lako ni chafu kwao

  Nilalapo wakuchota wewe
  Niamkapo ni feki sio wee
  Tanzania Tanzania
  Wakuponda kwa moyo wote
   
 9. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ulishamsikia Mkullo akijadili masuala ya taaluma? Jamaa ni mweupe kinoma kama boss wake... Smart people surround themselves with smart people.. Mkulu yeye kuzoazoa tu mradi uwe Mr yes man kwake.. kuna watu wengi tu kwenye baraza letu ambao reasoning yao na discussion of serious issues ni questionable..mfano yupo rafiki yangu (profesa wa miti shamba) Maghembe, sijui ukiwa profesa ndo unakuwa mchovu vile au alitoa mrungula kuupata? mwingine yupo profesa kapuya --- mimi sijui. kwenye timu ya kikwete watu ambao wanaweza kuanalyse issues ni wa kuhesabu na wote ukiangalia siyo wana mtandao (JPM, MKPP,Magreth Sita, yule mama aliye enda UN, basi) wengine wote wachovu
   
 10. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Sikubaliani na wewe kuhusu huyo Magreth Sita; huyu mama nae ni mchovu!! Huyo MKPP ndio nani tena ?? Kama ni Pinda basi nae nina question mark juu ya utendaji wake kwani ni mwoga, anawaogopa mafisadi!! Unakumbuka utumbo anaosemekana alisema kule Igumga kumsifia Rostam; sikutegemea waziri mkuu aliyejitosheleza angezungumza maneno ya kumsifia fisadi kama aliyoyatoa Pinda kule Igunga mbele ya wananchi kummwagia sifa fisadi papa!!
   
 11. M

  Magezi JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kwani Beno ndulu anafanya nini?? Yeye si professor??
   
 12. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Mimi siyo mchumi lakini ukweli haufichiki.

  Athari za utandawazi zinajidhirisha zaidi katika hali ambayo tumejikuta. Kuanguka kwa uchumi wa ugiriki kumesababisha EURO kuanguka vibaya sana na hali hii imeifanya USD$ BP£ kupanda thamani sana hivyo kusababisha wale ambao wana reserve kubwa ya pesa hizo[$$/£ kufaidika lakini wale ambao hawana reserve kubwa na wanategemea kununua bidhaa toka nje kwa kutumia pesa hizo ni lazima waumie.

  Sasa tunapoilaumu na kuiponda BOT ni kweli mnaitendea haki?????? au ndiyo ile hulka yetu ya kuponda kila kitu chetu tunapodhani [bila utafiti wa kutosha] vyombo vyetu havifanyi kazi??? kama mkiangalia mitandao mtakubaliana nami kuwa hali hii ni universal na kama juhudi za kuamsha uchumi wa ugiriki zisipofanikiwa ni kwamba ulaya yote na sisi wanyonge pia [isipokuwa uingereza] itaathirika vibaya kwani karibu wote wako kwenye Euro zone.
   
 13. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu tuko pamoja. Tatizo hili la kushuka kwa thamani ya shilingi tunapashwa kuliangalia kwa mapana yake kwani hata Euro imepoteza thamani yake mbele ya dola. Kuna sababu nyingi za msingi kuhusu hili, na tatizo sio ubovu wa Mkullo na Prof. pale BOT. Wachumi njoo na analysis yenye akili juu ya tatizo hili.

  Tiba
   
 14. B

  Bobby JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  OMG ina maana Abunwasi na Tiba hamjuwi sababu ya kushuka kwa Euro? If that is the case then we have a long way to go kama nchi.

  By the way, sisi hatuzungumzii kushuka au kupanda kwa USD kwenye global market sisi tunazungumzia kushuka kwa tsh against USD kitu ambacho kiko ndani ya uwezo wetu kama nchi meaning huwezi kumuondoa kwenye hili waziri wa fedha na gavana wa BOT otherwise yatakuwa ni makosa makubwa. Tumeeleza hapo juu system ya transactions zetu ndio inayopelekea mahitaji makubwa ya dola.

  Kila kitu sasa hivi kinauzwa kwa USD what do you expect kama sio demand kubwa ya USD? Guys basi someni kidogo issue ya demand na supply huenda mtaelewa kwanini mkullo na benno ndulu wakoresponsible moja kwa moja kwenye hili. Kama nilivyosema, kila kitu humu nchini kwa sasa kinanunuliwa au kuuzwa kwa USD as a result mahitaji ya USD ni makubwa sana kuliko supply yake kwani sisi hatuzalishi hizo USD.

  So basically hiyo ndio sababu ya kupaa kwa USD against Tsh. Na hii yote ni kwasababu hatuna serious government ambayo imepelekea kuwa na Finance Ministry na BOT zisizo serious pia. Sijuwi ni nani amemuambia Mkullo kwamba kazi yake ni kusoma budget peke yake huku akiacha uchumi unayumba pasipo kuchukua hatua zozote. Nilisema jana kila kitu Tanzania kwa sasa kiko kwenye auto pilot so lolote linaweza kutokea kwani serikali imeamua kwa makusudi kwenda likizo.

  Kwa kuwasaidia Euro imeshuka against USD kutokana na hofu iliyopo Euro zone yote kutokana na kuyumba kwa uchumi wa Greece. Ikumbukwe kwamba Greece kama zilivyo nchi nyingi za ulaya zinatumia Euro.
   
 15. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #15
  May 21, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Abunwasi kwani uchumi wa ugiriki umeanguka lini????

  Ukijibu hilo swali, naomba ujibu na hili pia;

  shilingi yetu imeanza kuporomoka toka lini??

  Tukitaka kutafuta sababu (external factors) za kuporomoka kwa shilingi yetu hatuwezi kukosa kabisa. Lakini je nini role ya central bank? Huko kudondoka kunatuathiri sisi tu? Mbona majirani zetu sarafu yao imekuwa stable kwa kipindi kirefu???
   
 16. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Pengine watu wa PR BOT hawafanyi kazi yao vizuri lakini ninavyoelewa mimi kwa sasa BOT lazimia itakuwa inauza reserve yake ya gold ili ijaribu kustabilize uchumi wetu na kwa vile sisi tuna import sana matumizi yataongezeka na kwa zile bidhaa tunazo uza nje bei itashuka Ukweli ni kwamba kwa hivi sasa ni taabu kwa wenye nazo na sisi tusionazo.

  Tutarajie thamani ya misaada kupungua, thamani ya export kupungua na kama hatucontrol matumizi yetu ya pesa za kigeni kama nchi tunaweza kujikuta kama ugiriki
   
 17. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #17
  May 21, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Brooklyn,

  Why is Greece in so much trouble?

  In recent years, Greece has been living beyond its means. , Its rising level of debt has placed a huge strain on the country's economy.

  The Greek govt borrowed heavily and went on something of a spending spree due this, public spending increased and public sector wages was doubled due cool down strikes.

  While this was going on, the money flowed out of the government's coffers, tax income was hit because of widespread tax evasion.

  Greece's budget deficit increase [the govt spent more than its revenues from taxation. [ last year was 13.6% of its gross domestic product (GDP)].
  Greece's high levels of debt means investors became wary of lending it more money and therefore, and demanded a higher premium for doing so.[This year the govt must refinance more than 50bn euros in debt..

  Why is this a worry outside Greece?
  Everyone in the euro zone - and anyone who trades with the euro zone - is affected because of the impact on the common European currency.

  The most immediate impact is on the 15 other euro zone economies who have agreed to help out Greece. The taxpayers of these countries will effectively share a part of Greece's burden.

  The impact of the crisis to other country [China for example]
  THE pain of the European debt crisis is spreading as the plummeting euro makes Chinese companies less competitive in Europe, their largest market, and complicates any move to break the Chinese currency's peg to the US dollar. Uncoupling the yen would make American goods more competitive against Chinese products.

  For various reasons, China has not yet put that policy into place and the euro's nosedive could make such a move even more difficult. Letting the yuan rise against the $US would also mean a further increase in the yuan's value against the euro, creating even more problems for Chinese exporters.
   
 18. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #18
  May 21, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Brooklyn
  Kama tukitaka kustabilize uwezo wetu basi la muhimu ni kuhakikisha tunauza zaidi kuliko tunavyotumia nakisi itokanayo na tofauti ya uagizaji na uuzaji zinasaidia sana kustabilize currency [ingawa kuna mambo mengi mengine]
   
 19. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #19
  May 21, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Brooklyn
  Kama tukitaka kustabilize uwezo wetu basi la muhimu ni kuhakikisha tunauza zaidi kuliko tunavyotumia nakisi itokanayo na tofauti ya uagizaji na uuzaji zinasaidia sana kustabilize currency [ingawa kuna mambo mengi mengine]
   
 20. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #20
  May 21, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu Bobby,

  Asante kwa maelezo ya ziada. Kwa taarifa yako najua sana hiyo demand and suppy theory zaidi ya unavyofikiria. Nilichojaribu kusema hapo juu ni kwamba tusikimbilie kuwalaumu Mkullo na Ndulu bila kwanza kuangalia some basic reasons behind kushuka kwa thamani ya shillingi. Kwa ufahamu wangu na kama kumbukumbu zangu ni sahihi shilingi imekuwa stable a bit for the past one year. Imekuwa ikicheza kwenye 1,300 mpaka 1,340. Ni wiki iliyopita tu imeshuka ghafula mpaka kufikia karibu 1,500. Sasa kushuka huku kwa ghafula kumetokana na nini? Ndio maelezo ninayotaka. Haitoshi kuniambia ni suala la demand and supply tu. Ndio maana nikaomba wataalamu wa uchumi watupatie mwongozo/maelezo ya kina.

  Nakubaliana na wewe kwamba BOT/Wizara ya fedha inabidi wafanye kazi ya ziada kuzuia uchumi wa Tanzania kuwa dollarized kwani hii ni hatari. Unashangaa unakwenda kupanga nyumba ya mtu anakwambia ulipie kodi kwa dola. Kwa nini? Kuna haja ya kuthibiti hali hii.
   
Loading...