Kazi wanazofanya mabolozi wa marekani katika nchi za kigeni,ni sawa za mabalozi wa Tz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kazi wanazofanya mabolozi wa marekani katika nchi za kigeni,ni sawa za mabalozi wa Tz

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mathias Byabato, Dec 21, 2010.

 1. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #1
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 905
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Kwa wanaofuatilia siri zinazoendelea kufichuliwa na mtandao wa wikileaks hasa zikionesha ripoti zinazotumwa na mabalozi wa marekani waliopo katika nchi za kigeni kwa nchi yao,wataklubalina na mimi kuwa mbali na kuwa baadhi ya siri ni ukweli,uongo au nyingine kuwa za chumvi lakini zinaacha funzo MOJA KUBWA kuwa mabalozi hao wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha nchi yao inaielewa vilivyo nchi mabalozi hao walipo.

  SWALI:Je kazi kama hiyo inagfanya pia na mabalozi wetu walioko katika nchi za kigeni? au waop wanafanya diplomasia tu.TUJADILI
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mabalozi wetu wapo kwenye shopping spree, utalii na networking, zaidi ya hapo ni kumpokea mhishimiwa endapo atafanya ziara huko. Nothing more. Hata hivyo, the writing is on the wall, the contents of cables speak for themselves.
   
 3. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kazi zinazofanywa na barozi za nchi iliyoko katika ngazi ya mtawala wa dunia haiwezi kuwa sawa na ile inayofanywa na barozi zinazowakilisha nchi zenye hadhi ya kutembeza bakuri duniani kote. Kwa nchi tawala za dunia, zinataka zifahamu kwa undani uwezo na misimamo ya viongozi wote wanao ongoza nchi na wasaidizi wao wakuu. Kwa nchi masikini habari kama hizo uenda zisiwe na maana yeyote.
   
 4. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2010
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,873
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  Byendangwero, nafikiri ni balozi na siyo barozi !
   
 5. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kufanya hayo wanayofanya wanabalozi wa marekani katika nchi za kigeni ni alama kwamba wana mitendao mikubwa sana katika kila sekta ya serikali/nchi husika: kila mahali wana watu wao. Ni ishara ya nguvu ya kipesa na kiinteligentia. Sasa mabalozi wetu wanaweza kuwa na mitandao ya aina hiyo nchi za kigeni? Siyo rahisi hata kidogo! Tuko maskini na uwezo mdogo wa kiinteligentia: hatuwezi kufanya hayo wanayofanya marekani. Kwanza ukijaribu tu wanakukamata kirahisi kwani hizo ni mbinu za kijasusi.
   
 6. Chifunanga

  Chifunanga JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2010
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Kwa marekani ni rahisi kwenda kwa kiongozi wa tanzania na kumuambia ampe story fulani na asipofanya hivyo marekani inaweza kupunguza misaada.....sasa balozi wa tanzania atatoa sababu gani ya kukutana na kiongozi wa marekani, na atamtishia nini ili apate taarifa ya siri?

  marekani wanaweza kupata hizi info zote kwa sababu ni matajiri na wana nguvu (jeshi n.k.) ya kushawishi.
   
 7. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  jamani 2natofauti kubwa sana sisi wakwetu wakienda uko unaandaliwa namna yakwenda kuwa omba omba maarufu kupita matonya
   
Loading...