Kazi Tunayo Mbona! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kazi Tunayo Mbona!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eliaona, Jun 25, 2009.

 1. Eliaona

  Eliaona Member

  #1
  Jun 25, 2009
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 25
  Mwl. JK Nyerere aliandika kijitabu kidogo kiitwacho "Uongozi na Hatima ya Tanzania".
  Juzi juzi hapa habari ya Zimbabwe ikiwa joto juu Mzee Mandela akiwa huko London kwenye Birthday yake alisema hivyo hivyo juu ya Zimbabwe..
  Sasa hapa kwetu tunasikia kila siku sakata juu ya sakata sio ndani ya CCM sio ndani ya Chadema sio CUF. Kweli tunaenda wapi, kwani tumeshindwa kabisa kuandaa viongozi wa nchi yetu hii?
   
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Nyerere alikuwa hana jipya

  anaendelea kututawala toka kaburini na la kufanya hatuna
   
 3. Eliaona

  Eliaona Member

  #3
  Jun 25, 2009
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 25
  Namthamini mchango wake walau ulitupatia direction kidogo, lakini sasa mambo yanavyoenda, Mungu atuepushe tu...
   
 4. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  sikatai direction yenyewe ilikuwa ni ya kurudi nyuma gizani
   
 5. Eliaona

  Eliaona Member

  #5
  Jun 25, 2009
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 25
  Sasa hii ya hawa wenzetu wa sasa inaenda wapi?
   
 6. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Kama ingekuwa hivyo basi kusingekuwa na hata harufu ya Rushwa. Kila siku najiuliza kama angekuwepo EL saa hizi angekuwa wapi. Au viongozi wa Chama wanaokumbatia ufisadi wangekuwa wapi. Yeye aliweza kuwatolea uvivu hata PM Malecela na Secretary General Kolimba enzi hizo. Sidhani kama angeshindwa kufanya hivyo leo, hata kama angetembelea mkongojo.

  Mkuu yule Mzee alikuwa na mabaya yake lakini la ufisadi au kuutetea hakuwepo. Let him have a good rest.
   
 7. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  ahera
   
 8. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  haina dira wala mwelekeo
   
 9. K

  Kyatsvapi JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 316
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  Nadhani ishu siyo chama. Anayepewa madaraka ndani ya chama, ndiyo tatizo. Kwani hata dini; japokuwa zinahubiri wema, lakini wengine, miongoni mwao wanafanya mambo ambayo hata shetani mwenyewe huwa haamini kama yanaweza kufanywa na wanadamu. Nikupe mifano. Ni kwa nini pope wa Roma alinusurika kupigwa risasi mwaka 1982? Sababu gani zilisababisha hata Kennedy, F (rais wa Marekani) kuuawa?

  Majibu ya maswali haya na mengine yanaonyesha ni kwa jinsi gani dini zetu zinatumika kufanya mambo ya siasa na kusahau lengo lake kuu la kuhubiri ufalme wa Mbinguni.

  Kwa hiyo, sishangai chama kikiwa kinavurugwa na watu wachache wanaokuwa wanakitumia vibaya na wengine wengi kukubali kufuata na hata kusifia matendo yao hata kama ni mabaya. Haya ni matokeo ya kutokutumia vizuri akili zetu na kuwaacha wengine wazitumie badala yetu. Hivi, tukubadilishana nchi; Watanzania wote wakahamia Marekani na Wamarekani wakaja Tanzania (kila watu waende kama walivyo, bila kuchukua kitu chochote), maisha ya Watanzania hawa wakiwa Marekani, yatakuwa endelevu kimaendeleo (sustainable)?

  Think critically.
   
Loading...