Kazi serikalini na fao la PSPF

Stv Mkn

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
328
273
Wakuu naomba mnisaidie kufahamu, mimi nimeacha kazi rasmi November mwaka jana. Ni serikalini.

Niliandika barua ya kuresign ila mpaka sasa sijajibiwa, ila mshahara umesitishwa.

Nachoomba kueleweshwa ni je naweza kupata pension yangu niliyochangia kwa miaka minne kazini? Nilikuwa mfuko wa Pspf.

Na process zao ziko vipi?
 
ulamua kufanya maamuzmagumu, baki huko ulikoona kunafaa, miaka minne ni sawa na miezi 48 ni sawa na average ya sh 1.3 mil
 
ulamua kufanya maamuzmagumu, baki huko ulikoona kunafaa, miaka minne ni sawa na miezi 48 ni sawa na average ya sh 1.3 mil

Wabongo tuna roho mbaya sana ndio maana hatuendelei,unijui sikujui ila umeshaanza kunifanyia choyo...sasa nibaki wapi na ninataka kurudi wapi? na hiyo calculation umeitoa wapi?
 
Wabongo tuna roho mbaya sana ndio maana hatuendelei,unijui sikujui ila umeshaanza kunifanyia choyo...sasa nibaki wapi na ninataka kurudi wapi? na hiyo calculation umeitoa wapi?

Ahaaaa labda anajua wafanyakzi wote wa serikali wanalipwa laki mbili.
 
Ukweli ni kuwa ukiacha kazi unalipwa fao la kujitoa na si pensheni.. Labda watu wameshindwa kujua nn mana ya pensheni

hvyo basi unachotakiwa kufanya mara baada ya mwajiri wako kuthibitisha kuwa ww si mfanyakaz tena... Unachotakiwa kufanya ni kujaza Form namba 6 inayopatikaNa ofisi zote za pspf mikoa yote.... Then utaambatanisha barua ya ajira.. Barua ya kuthibitishwa kazin kama ipo.... barua ya kuacha/kufukuzwa kazi.. Nakala ya kadi ya bank na salary slip ya hv karibuni (most recent)
baada ya kukamilisha utarejeshewa michango yako yote na ile ya mwajiri... Ila huwezi liowa penshen ya kila mwezi kwa sababu dheria inataka uchangie angalau miaka 15 ndo uwe na sifa ya kulipwa penshen ya kila mwezi

NB. KWA MAKOSA YA KINIDHAMU (MISSCONDUCT), kuachishwa au kuacha kazi kunakunyima fursa ya kulipwa pensheni ya kila mwezi badala yake unapata kiinua mgongo

TIP

1. Ukiacha/kufukuzwa kazi wakat umechangia miaka 15 au zaidi utalipwa kiinua mgongo bila penshen ya kila mwezi
2. ukiacha/kufukuzwa kazi na hujatimiza miaka 15 ya kuchangia... Unarejeshewa michango yako yote.. Na ya mwajiri pia....

HATA HIVYO.. UKIACHA KAZI NA UNATAKA KUBADILISHA MWAJIRI.. IPO FURSA YA KUWASILIANA NA PSPF.. ILI UENDELEZE MICHANGO YAKO PALE ULIPOISHIA ILI USPOTEZE SIFA YA KULIPWA PENSHEN.....
 
Na mimi niulize hapa, nasikia wanatoa mkopo wa elimu kwa wanachama wake...je makato yake watakata kwenye salary kila mwezi au watakata kwenye mafao yako ya mwisho?
 
MwanaJF Stv Mkn, km ukiacha kaz na mwanachama wa PSPF unarudishiwa michango yako yote na ya mwajiri kwa muda uliofanya kaz kama Mdau hapo juu alyefafanua vzr.

Nenda ofs ya PSPF iliyo jiran na ww ili upate maelezo zaid. Kwa sasa PSPF wamebadilika/wamebadili sheria zao nadhan sababu ya ushindan wa mifuko mingi ya penshen iliyopo sasa.

MwanaJF Mmasihiya, niliwah kwenda ofs ya pspf takriban wiki 2 zilzopita kuulzia khs mkopo wa elimu, nikaambiwa wanakata ktk Mshahara wa mfnykz km mkopo wa benki na sio ktk penshen.

Kwa maelezo zaidi unaweza kwenda ofsn au omba kijarida kina maelezo yote au ingia ktk tovuti yao.
 
Kifupi mifumo mingi duniani imeanzishwa kwa ajili ya kumnyonya mfanyakaz na sio kumsaidia (mifumo ya kibepari)

Ndio maana siku zote wafanyakaz ni kulalamika kunakotokana na kukandamizwa na mamlaka zilizipo eneo husika.

Mifuko ya penshen (mfn: PSPF) wanakusanya hela nyng za wafanyakaz na kuwekeza ktk mirad mbalimbali na kutengeneza faida kubwa sana (super profit) lakn penshen/mafao ya mchangiaji hiyo hela (yaan mfanyakaz) inachakachuliwa ili apate kidogo....it pains much!
 
Wakuu naomba mnisaidie kufahamu, mimi nimeacha kazi rasmi November mwaka jana. Ni serikalini.

Niliandika barua ya kuresign ila mpaka sasa sijajibiwa, ila mshahara umesitishwa.

Nachoomba kueleweshwa ni je naweza kupata pension yangu niliyochangia kwa miaka minne kazini? Nilikuwa mfuko wa Pspf.

Na process zao ziko vipi?

heee kumbe watu wanaachaga kazi serikalini...c nlickia hawaachagi...okaaay
 
Na mimi niulize hapa, nasikia wanatoa mkopo wa elimu kwa wanachama wake...je makato yake watakata kwenye salary kila mwezi au watakata kwenye mafao yako ya mwisho?

Michango haiwezi kukatwa kwa namna yoyote ile.. Michango inasimama kama security kwa ajili ya uwekezaji na ulipaji mafao

mkopo wa elimu na wa kujikimu hukatwa ktk mshahara wako wa kila mwezi kwa riba ya 1.17 kila mwezi mpk deni litakapoisha
 
Kifupi mifumo mingi duniani imeanzishwa kwa ajili ya kumnyonya mfanyakaz na sio kumsaidia (mifumo ya kibepari)

Ndio maana siku zote wafanyakaz ni kulalamika kunakotokana na kukandamizwa na mamlaka zilizipo eneo husika.

Mifuko ya penshen (mfn: PSPF) wanakusanya hela nyng za wafanyakaz na kuwekeza ktk mirad mbalimbali na kutengeneza faida kubwa sana (super profit) lakn penshen/mafao ya mchangiaji hiyo hela (yaan mfanyakaz) inachakachuliwa ili apate kidogo....it pains much!

Hii kauli haina ukweli...... Hakuna mfuko unaolipa vzuri.zaidi penshen na viinua mgongo kuliko pspf... Na hakuna mfuko unaolipa penshen za wastaafu ila pspf pekee
 
Michango haiwezi kukatwa kwa namna yoyote ile.. Michango inasimama kama security kwa ajili ya uwekezaji na ulipaji mafao

mkopo wa elimu na wa kujikimu hukatwa ktk mshahara wako wa kila mwezi kwa riba ya 1.17 kila mwezi mpk deni litakapoisha

Ahsante kwa taarifa mkuu
 
Back
Top Bottom