Kazi nimeiomba na ninaitaka, lakini interview siko tayari?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kazi nimeiomba na ninaitaka, lakini interview siko tayari?!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Baija Bolobi, Oct 9, 2010.

 1. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Waheshimiwa nisaidie kitendawili hiki:

  Tangazo la kazi limetolewa. Sifa za nafasi hiyo ninazo. Barua ya maombi na CV nimeandaa na kuomba kazi hiyo. Sasa wameniita kwenda kwenye interview pamoja na wengine walioomba na kuwa-short listed. Mimi sitaki kwenda kwenye interview hiyo kwa sababu nahisi kuna njama za kuniuliza maswali "mabaya" ili nikose kazi hiyo, lakini kazi naitaka sana. Je niipateje kazi hiyo bila kwenda interview. Je CV yangu itatosha kuwashawishi waajiri wanipe kazi hiyo na kuwaacha waliofika kwenye interview hiyo?

  Hii ina tofauti gani na CCM? Udiwani, Ubunge na Urais wanautaka. maombi wamepeleka. CV zao (Ilani) wamepeleka. Waajiri ni Watanzania. Wamewaalika waombaji kwenye interview (Midahalo), lakini CCM hawataki kwenda, lakini wanasisitiza kuwa kazi wanaitaka. Je kazi wapewe?
   
 2. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2010
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Sambaza katika sms! Ni ujumbe mzuri sana!:hand:
   
 3. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2010
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  imekaa vizuri sana
   
 4. D

  Dopas JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kazi wasipewe. Tutajuaje kama CV ni zao kweli au wamefoji? Uwezo wao wa kujibu maswali ya papo kwa hapo katika interview ungetupa nafasi ya kufahamu uwezo wao zaidi, na kuamua kuwapa kazi au la. Kwa vile wameogopa interview nasi tuogope kuwaajiri, hasa kiongozi wao mkuu JK
   
 5. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Mwajiri anaweza kuamua kukuajiri kwa kuulizia habari zako kwa mwajiriri wa zamani (Bado ni sisi wananchi) na akijiridhisha atakupa ajiri. CCM wananchi tunao kwa miaka 50 sasa tukijiridhisha na utendaji wao wa huko nyuma tutawapa kura, lau hutujaridhika tutaangalia miongoni mwa wale tulio wa interview. Lakini kwenye kazi kuna kitu kinaitwa "LEARNING CURVE" kama tutakao wainterview IQ yao ni ndogo kuweza kuleta majibu ya haraka kwa matatizo ya wananchi, bado yule wa zamani angalau anafahamu nini cha kufanya na kama atakuwa tayari kurekebisha yale wananchi tusiyoyapenda tutaendelea kumpa kazi.
   
 6. P

  Paul S.S Verified User

  #6
  Oct 9, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Acha uvivu wa kufikiri mkuu, mfano wako ni mfu kabisa, aliekwambia mdahalo ni lazima kama usaili ni nani.
  na hata hivyo mkuu mbona usaili anahojiwa mmoja mmoja si kikundi kama mdahalo?
  kama kweli ni usaili basi unafanywa mbele ya wanaotakiwa kufanyiwa kazi na si lazima tufanyiwe pamoja kwa wakati mmoja.
   
 7. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  imekaa vizuri sana awajamaa awafai ata kidogo utaombaje kazi alafu upewe kinyemele ila aishangazi kwani walishaozea kuchakachua so kila kitu wao ni kuchakachua tu
   
 8. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #8
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  bravo Slaa, nimeipenda hiyo, HAKUNA INTERVIEW HAKUNA KAZI, HAKUNA MDAHALO HAKUNA KURA.
   
 9. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  :mad::mad::mad:
   
 10. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Hakuna mdahalo hakuna kura.
   
 11. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #11
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280

  wataisoma namba mwaka huu.
   
 12. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Huu mfano umekaa vizuri wewe p.u.s.s.y, wewe ndio mvivu wa kufikiri, kama mtu hataki interview hataki kazi, tuachane nae.
   
 13. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #13
  Oct 9, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hapo sijaona uvivu wa kufikiri mkuu ila naona kama wewe ndiyo hujatanua mawazo zaidi kutafakari
   
 14. P

  Paul S.S Verified User

  #14
  Oct 9, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  kapotolo ndugu yangu karibu sana janvini
  hapa tunakubaliana kutokukubaliana kwetu kwa hoja na si matusi.
  jaribu kutunza motto ya janvi try to be the great thinker
   
 15. P

  Paul S.S Verified User

  #15
  Oct 9, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  lakini hata tukikubaliana issue hii kuwa usaili, j usaili utakuwa mdahalo au mikutano ya kampeni?
  kama wangegoma na kampeni ambapo wanakutana na maswali pia ningekubaliana na wewe
  naita uvivu wa kufikiri sababu interview ni lazima katika kazi kama ilivyo kampeni ktk chaguzi, lakini mdahalo si lazima mkuu
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Oct 9, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Naelewa unachosema, CCM wamechemsha kichizi kusema hawataki midahalo kwa sababu hii ni njia nzuri sana ya kuweza kuwahabarisha wananchi kuhusu mipango yao.

  Lakini ukisema hawataki interview, CCM ( pamoja na wasiofungamana na upande wowote kama mimi) wanaweza kukwambia kwamba katika utetezi wa CCM, CCM wanasema sio kwamba hawataki interview, wanataka (na wanafanya kwa mujibu wao) interview moja kwa moja na wananchi. Wanasema hawataki "phone interview" (TV debates) kwa sababu inaweza kutumiwa vibaya, wanataka kuongea na wananchi moja kwa moja.

  If you ask me this is pure baloney, kwa sababu kama wanataka sana kuongea na wananchi moja kwa moja kwa nini rais anahutubia kwa kutumia TV na redio ? Na kama hotuba za rais zinafaa kutumwa kwa matangazo ya TV na redio kwa nini midahalo ya kampeni isifanyike kwa jinsi hii ?

  Kusema CCM haitaki interview si sahihi, kitu sahihi zaidi kingekuwa kulinganisha CCM na muomba kazi anayesisitiza interview iwe jinsi anavyotaka yeye tu. Hatuwezi kukubali chama kipange jinsi gani kinataka kuwa wazi kwa wananchi, wananchi ni lazima wavilazimishe vyama kuwa wazi.

  Tatizo ninaloliona hapa ni kwamba, CCM hawahofii kwamba kutotaka mijadala kutawapotezea kura, inahofia kwamba kuingia katika mijadala kutawapotezea kura. Chama gani kinaogopa kuingia katika mjadala? Obviously ni chama ambacho hakijatekeleza ahadi zake na wala hakina uwezo wa kujieleza kwa wananchi.

  Watanzania wakiendelea kukichagua CCM watakuwa wamekipa leseni ya kuendelea kuongoza bila kuwa wazi, na wasitegemee uwazi wowote kutoka CCM siku za mbeleni. Kwa nini CCM waongeze uwazi wakati wanashinda chaguzi bila hata kukubali kuwa wawazi?

  Hivi zile kelele za Benjamin Mkapa kuhusu "Ukweli na Uwazi" zimeishia wapi ? Ndio uwazi huu tunaouona kwa kukataa midahalo? Au zilikuwa propaganda za nguvu ya soda tu ?
   
 17. M

  Mnyalu wa Kweli JF-Expert Member

  #17
  Oct 9, 2010
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 233
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Huyu jamaa anayeupinga mhadalo inaonesha hata elimu yake in ya kufoji vyeti. Na hiyo ndiyo tabia ya viongozi na wanachama wengi wa CCM. Msemakweli alikuja na orodha ya wenye doctorate feki kibao ndani ya baraza la mawaziri. kuna aliyekanusha?
   
 18. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #18
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Asante, nimekaribia, try not to be much provocative
   
 19. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #19
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,266
  Trophy Points: 280
  Huwezi kumwajiri mtu ambaye haji kwenye zoezi la kusailiwa. Huo ndiyo ukweli wao CCM na hakuna mwingine.
   
Loading...