Kazi na majukumu ya Meya hapa Tanzania ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kazi na majukumu ya Meya hapa Tanzania ni nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Massenberg, Feb 10, 2012.

 1. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Utafiti wa haraka haraka usiohitaji utaalamu utakuonyesha kuwa katika nchi nyingi meya wa mji au jiji ni mtu mwenye madaraka na majukumu yanayofahamika na kuonekana wazi. Haya ni pamoja na masuala ya uchumi na uwekezaji katika mji, afya, miundombinu, mazingira, makazi, usalama, usafiri, n.k.
  Katika hali ya kushangaza mameya wa miji ya Tanzania ni watu ambao wapowapo tu na wengi wao hata hawajulikani. Mara nyingi mambo ambayo ni majukumu ya meya utakuta mkuu wa mkoa anayafanya. Kwa mfano, katika maafa ya mafuriko ya hivi karibuni mameya walitakiwa kuwa wahusika wa kwanza lakini hakuna kitu zaidi ya kupiga porojo za siasa tu.
  Swali ni kwamba je, mameya wa Tanzania wana kazi tofauti na mameya wengine duniani?
   
 2. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  wamejipa kazi ya kuhodhi na kugawa viwanja...
   
 3. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Kwa hapa Tanzania hakuna ilipoainishwa kwa maandishi kwamba Meya anapaswa kuwa mtu wa namna gani? Uwepo wao ni kutokana na kuchaguliwa na madiwani wenzake, madiwani wenyewe nao pia upatikanaji wao ni wa kisiasa tu - wanachaguliwa na wananchi waliochoka kimaisha - ambao wakipewa chumvi kidogo tu wanachekelea kama zuzu. Kwa kuwa kuna uwezekano wa kuwa na Meya Mbumbumbu ambaye anapendwa na raia pamoja na madiwani wenzake, tusitegemee kuwabana sana hawa mameya hadi hapo tutakapoweka sheria ndogo za uchaguzi zitakazowabana wagombea kuwa na professionals.
  Madiwani wengi ni form foour failer, Std VII na wengine records zao haziko wazi.
   
 4. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Na kinachowapunguzia uwezo wa maamuzi ni uwepo wa Mkurugenzi wa jiji kwani maamuzi mengi ya Halmashauri yanatolewa na Mkurugenzi ambaye ni Chaguo la Rais. Wakurugenzi wengi ndo wanarudisha maendeleo ya miji / majiji nyuma kwa kuwa wengi hawatekelezi mapendekezo ya madiwadi wa kata za mji husika; bali hutekeleza amri toka kwa Bwana wao.
   
 5. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #5
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  MEYA=Mega keki na Epuka Anayekuja kama ni mwizi,hata mkurugenzi wa wilaya na mkuu wa wilaya sioni haja ya wote kuwepo ni bora awepo mmoja afanye majukumu yote
   
Loading...