Kazi kuu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nini?

Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
5,023
2,553
Nimekuwa nafuatilia kampeni za ubunge arumeru kwa muda sasa, nilichogundua kutoka kwa wagombea wote wawili ni ahadi ambazo kimsingi itamlazimu mbunge husika atoe hela ya kwake kwa ajili ya kutumiza ahadi husika, ninachojua ni kwamba kazi kuu ya bunge ni kutunga sheria za nchi na si vinginevyo.
 
Najua kazi za mbunge tu,so unaweza ukatohoa hapo:

•Kutunga sheria
•kusimamia serikali
•kuwakilisha wananchi
 
kazi za ubunge inategemea na chama:kama upo chama cha magamba kazi nikudai posho kwa nguvu zote,kusinzia mjengoni,kugonga meza huku ukizomea kwa nguvu zote nk...kama upo Chadema kazi kubwa ni kutunga sheria,kuisimamia serikali,kuwasilisha matatizo ya watanzania na wananchi unaowawakilisha hizi ndo kazi za wabunge.
 
Nimekuwa nafuatilia kampeni za ubunge arumeru kwa muda sasa, nilichogundua kutoka kwa wagombea wote wawili ni ahadi ambazo kimsingi itamlazimu mbunge husika atoe hela ya kwake kwa ajili ya kutumiza ahadi husika, ninachojua ni kwamba kazi kuu ya bunge ni kutunga sheria za nchi.na si vinginevyo

Bado wanaweza kushirikiana na wananchi katika kujiletea maendeleo jimboni na ndio maana kuna Mfuko wa Jimbo wa Maendeleo. Apart from huo mfuko wa maendeleo, bado wabunge ni wajumbe Baraza la Madiwani, mara nyingi vikao hivyo ndio huamua namna ya kukusanya mapato na namna ya kutumia. Kwa hiyo kama Baraza la Madiwani linafanya kazi kwa manufaa ya wananchi, unaweza kuta jimbo lina mipango mingi ya maendeleo na serikali kuu huachiwa mambo makubwa ambayo bajeti yake hutoka serikali kuu.
 
Bado
wanaweza kushirikiana na wananchi katika kujiletea maendeleo jimboni na
ndio maana kuna Mfuko wa Jimbo wa Maendeleo. Apart from huo mfuko wa
maendeleo, bado wabunge ni wajumbe Baraza la Madiwani, mara nyingi
vikao hivyo ndio huamua namna ya kukusanya mapato na namna ya kutumia.
Kwa hiyo kama Baraza la Madiwani linafanya kazi kwa manufaa ya
wananchi, unaweza kuta jimbo lina mipango mingi ya maendeleo na
serikali kuu huachiwa mambo makubwa ambayo bajeti yake hutoka serikali
kuu.

kwa kutumia mfuko wa jimbo wanaweza kuibua miradi ambayo serikali itawaunga mkono kuifanikisha.
 
1. Serikali inaleta muswada bungeni ili ujadiliwe na kuboreshwa (kupitia michango ya wabunge) na baadaye upitishwe (kutunga sheria).
2. Kinachofanyika ni kwamba serikali inaleta muswada, unajadiliwa na wabunge wanapochangia ili uboreshwe waziri aliyeuleta anakuwa very defensive na anasema kwa nini serikali inataka vifungu fulani (vyote au karibu vyote) vibaki kama vilivyo na hatimaye hupitishwa kwa kura ya majority hata kama hoja zenye mashiko zimetolewa na wabunge kutoka vyama vya upinzani.
3. Kupitisha sheria kwa namna hii ya No 2 kwa maoni yangu ni kupitisha sheria na siyo kutunga sheria.
4. Wadau mnalionaje hili? Tuelimishane.
 
Mkuu uko sahihi kabisa kama ammbavyo bunge huwa halituingi bajeti linaletewa bajeti iliyokwisha tungwa kisha wajadilli kidogo.

Kazi ya kutunga sheria sio mchezo mbunge kama mnyika ambaye hata chuo kikuu hajawahi fika hawezi tunga sheria yule hata Lissu hawezi. Wanachoweza ni kujadili miswada ya sheria ILIYOLETWA NA SERIKALI si kutunga.

Hata bajeti hawawezi tengeneza ukisoma bajeti ya upinzani huwa imejaa vituko.Haiwi bajeti mbadala inayoonyesha mapato na matumizi huwa imekaa kimbeya mbeya tu ikielezea jujuu tu sehemu za kuelekeza matumizi bila kujikita kuonyesha kwa undani hizo bla bla zao pesa ya ku-finance ipatikane wapi kwa mchanganuo upi.

Upinzani hawajui kutengeneza bajeti mbadala wanajua kutengeneza bajeti kipande ya kubishia bungeni tu
 
Kutunga sheria maana yake ni 1) muswada kuletwa bungeni 2) wabunge kuujadili kwa nia ya kuuboresha 3) kuupitisha au kutoupitisha 4) kufanya hivi ndiyo kutunga sheria kwa maoni yangu. Lakini 1) muswada kuletwa 2) kuujadili kwa ushabiki ili upite jinsi ulivyo na 3) kuupitisha bila kwangu huku ni kuwa rubber stamp na siyo kutunga sheria.
 
Back
Top Bottom