Kazi kubwa ya Serikali ni kurudisha Imani ya Wananchi kwa Serikali yao

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,298
12,598
Ilifikia wakati Wananchi akiwemo mimi nilianza kupoteza imani kwa Viongozi wa Serikali kutokana na kutofautiana sana kati ya kauli na matendo yao, na kati ya mambo yalivyo na yanavyotakiwa kuwa.

Mfano:
1. Wafanyakazi wanaambiwa warudi nchini lakini wanaporudi wanafikia TAKUKURU na mahabusu.

2. Serikali inasema maendeleo hayana chama lakini hapohapo unasikia kionhozi akisema hajajenga barabara kwakuwa wananchi walichagua mpinzani.

3. Wanasema tumtangulize Mungu kwa kila jambo lakini kuna watu wanaopotea kwa visasi na chuki.

4. Tutaboresha maisha ya wafanyakazi lakini maisha ya mfanyakazi ni ya kipato kisichokidhi uhalisia wa maisha na kodi kubwa.

5. Wamachinga wanaharibu mazingira na kuziba njia, nafasi za wazi zote na kuonheza uhalifu lakini utamsikia kionhozi akisema hao ndio wapiga kura wangu waachwe. Na wengine wanasema waondolewe mitaani. Nani yuko sahihi?

6. Ahadi nyingi wakati wa uchaguzi tu na namna washindi wanavyopatkina, wanavyochaguliwa na kutangazwa kila mtu anakakaa kimya tu kwakuwa sio kwakuwa hajui lakini kwakuwa hana LA kufanya.

7. Mgawanyo wa miradi mikubwa kikanda, mikoa, wilaya, tarafa, kata, vjijiji na vitongoji vina harufu ya ubaguzi wa kanda, mkoa, wilaya, tarafa, kata, kijiji na kitongoji na familia IPI imetoa kiongozi wa umma.

8. Mwananchi hana uhakika na haki yake mikononi mwa polisi, mahakama, na ofisi ya umma.

Hii ni mifano tu ya imani zilizopotea ambazo serikali yetu ya sasa haina budi kuzirejesha kwa watu wake. Hivi utawezaje kumuita MTU arudi halafu akija anafikia kwenye mikono ya vyombo vya dola eti uliharibu hiki na kile. Huku ni kufukua makaburi kunakoweza kusababisha wafanyabiashara wengine wasirudi haraka nchini.

Nadhani serikali kwenye hili ingekuwa kufungua ukurasa mpya wa uwekezaji na ukusunyaji kodi kwa 100% kwa kila mwekezaji mpya, wazamani na anayerejea baada ya kuikimbia nchi.
 
Nataka kuamini kwamba hajashikiliwa kwa ubaya, kama hesabu zake zipo vizuri na wala hakuwa na hila kwenye mambo ya kodi bila shaka watamuachia au watayajenga mambo yaishe na kauli ya mama ibaki na heshima yake, tusubiri matokeo angalau Takukuru na TRA ya wakati huu sio ile ya Shujaa.
 
Si misema Jiwe ndio ana bifu naye? Leo je?
Juzi juzi nilipita kule Kigamboni mtaa wa Dege nikaona magorofa lukuki ambayo yametelekezwa hayajamaliziwa ujenzi. Nikaambiwa eti ni mali ya NSSF na Manji kwa ubia.

Hata kama kulikuwa na ufisadi kwenye ule mradi lakini kutelekeza mradi mkubwa ambao ungetoa ajira na makazi kwa watanzania sio sawa wala hekima. Kwenye mradi ule maana yake TRA ingepata kodi, tannesco ingeuza umeme, Dawasa wangeuza maji, makampuni ya simu na mabenki yangepata faida nk.

Napenda tuimarishe mifumo yetu ya Kofi ili kila MTU alipe.
 
Back
Top Bottom