Kazi kubwa ya mwana chadema na mpenda tanzania mzalendo, m4c | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kazi kubwa ya mwana chadema na mpenda tanzania mzalendo, m4c

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwawa, Jun 11, 2012.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Kazi kubwa iliyeko mbele yetu wana-mapinduzi wananchi wa Tanzania kwa uwingi wetu na sehemu mbali mbali za nchi yetu nzuri yenye rutuba, maziwa, wanayama, madini na viongozi wabovu ni kuelimishana na kuelimisha umma wa nchi yetu.

  Utawala ni utamaduni, maendeleo ni fikra na kizazi. Maendeleo ni kuyapenda, kuyahitaji, kuyajua na kuyaishi. Serikali iliyoko madarakani sio kwamba tu haipendi maendeleo ya nchi yake bali hata haijui nini maana ya maendeleo.

  Propaganda zinazoendeshwa na vijana wa CCM sio hujuma tu kwa nafsi zao bali hata kwa vizazi wao. Sioni ni kitu gani CCM wanataka kulazimasha umma wa mtanzania. Kwa miaka 50 wamekuwa madarakani na walio wengi wamekuwepo tangia tunapata uhuru, wakiwa na akili zile, mawazo yale yale matendo yale yale wakitegemea tutapata majibu mapya. Mbinu za kumtoa Mtanzania kwenye lindi la umasikini wameshindwa hawawezi na hawakubali kuwa wameishiwa.

  Kinachoniumiza akili ni vijana wa CCM ambao baadhi wako juu na wamezaliwa baada ya 1975. hawa baada ya kufundwa na wazee hawa waliochoka akili, matendo na kuishi nao wanafikiri kama hawa wazee wanatenda kama hawa wazee.

  Kweli leo tatizo la Tanzania ni mtanzania kuwa chama gani cha siasa?? Kweli tatizo la maji, ubovu wa barabara, foleni ya Dar es salaam, wizi, rushwa, ufisadi, huduma mbovu za jamii zitamalizwa kwa chama tawala kufanya mikutano ya propaganda za enzi ya 1977???

  Nategemea chama chochote kikiwa madaraka kitoe suluhisho la matatizo kwa vitendo sio kuendeleza siasa za majukwaani.

  Wanachama na wapenzi wa CDM (CHADEMA) naomba tusikubali kuiga huu upuzi pindi tuingiapo ikulu 2015. Kazi kubwa ya serikali ya CDM iwe ni kutatua matatizo ya wananchi na kuwaletea maendeleo. na Viongozi wetu wakitimiza wajibu wao kutokana na sera na ilani ya uchaguzi hawatakuwa na sababu ya kupoteza muda na fedha nyingi kuuza ukweli kwa wapiga kura wao. kizuri chajiuza na kibaya......

  Mtindo huu wa siasa za kikomunisti wa kulazimisha uzuri wa maisha usiokuwepo ni ujuhu.

  Jambo lingine linalonikatisha tamaa ni hawa wasomi wetu walioko CCM, pindi wakipewa vyeo akili zao zinasimama zinashindwa kufikiri. Huwa hawana subira, tathimini na wana hamaki kupewa vyeo vile.

  Tuanze na waziri wa mambo ya barabara ambaye aliwahi kuwa waziri wa ardhi. Leo hii jiji la Dar es salaam liko shaghalabaghala hakuna mipango miji hakuna utaratibu. Sehemu zilizopimwa chini ya utawala wa Magufuli sasa Tibaijuka hazina uataratibu mzuri, hazina uangalizi wa ujenzi hivyo kujengwa hovyo na watu kuuziana viwanja hovyo kutengeneza slam mpya. Sheria hazifuatwi na wanatengeneza matatizo makubwa usoni.

  Ukiangalia foleni ya jiji la Dar linasababishwa na ukosefu wa barabara. kwanini ukiwa kibaha pasiwe na barabara unatokea mitaa ya gongo lamboto au ukonga. Ukiwa Tegeta, bunju nk na unataka kwenda kibaha kwanini uje mpaka mwenge ubungo?

  Yako wapi maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya viwanda, biashara, na ofisi nje kidogo ya jiji. Unapotenga maeneo haya na kupeleka huduma za jamii kama barabara, maji, umeme wa uhakika nk utaona wengi wakielekea huku kukwepa msongamano wa jiji. Iko wapi plan ya jiji letu ya miaka 100 ijayo au viongozi wetu ni zima moto tu??

  Tayari Dar tumeingia kwenye kitim tim cha mji usioeleweka uliokosa uthibiti wa mpango jiji, je viongozi hawa wanafanya nini sasa kuzuia miji inayokuwa isiwe kama Dar miak 25, 50, 100 ijayo??? Au wanasubiri wafe wawaachie watoto na wajukuu wajiju????

  Ukiangalia barabara zetu zinavyounganisha mikoa, wilaya, tarafa na kata utaona haya yote yanaongeza gharama za maisha na kuslow ukuaji wa uchumi kati ya mkoa kwa mkoa na wilaya kwa wilaya kwani ni sehemu nyingi sana inakubidi kuzunguka mno kabla ya kufika sehemu husika. Kwa nini wasianze hata na barabara za vumbi ili wakati wa kiangazi tuweze kupita kwa ukaribu?? Hata survey tunahitaji wafadhili.

  Tangia uhuru ni bara bara chache sana au hakuna mpya, zaidi ya kukarabati kihuni zile zile za mkoloni au Nyerere. Tuko 42-45 Milioni na hukana kitu kimeongezeka kuhudumia wananchi. Angalia chanzo cha maji cha Dar ni kile kile cha kuhudumia watu 1 Milioni leo tupo zaidi ya 4 Milioni halafu tunashangaa maji hakuna. hatuna chanzo kipya cha umeme zaidi ya Generator za kisanii.

  Mitaala yetu ni mibovu haitoi wataalamu tena inazalisha wasomi wa makaratasi halafu tunasubiria kwenda mwezini. Ndio maana kila mkata hata wa kufagia tunapigwa na wajanja. Mfumo huu wa elimu ya kukremu hauwezi kutupeleka mbali. lazima kutumia wataalamu wandani na bidhaa za ndani ili kukuza elimu ya ushindani na soko la ndani.

  Ni kazi ya viongozi walioshika dola kuleta maisha bora kwa vitendo sio kupiga tararira. CCM inabidi mjue mku madarakani, mnawajibu na kodi zetu acheni kutulaghai. Na tujue wote maendeleo ni kwa faida ya wananchi wote bila kujali vyama vyao. Uzalendo tunaouhubiri uko wapi?? Wakuishangilia mafisadi unapohitaji fedha zao au msaada wao wa kushindi kwenye siasa??? Uzalendo uko wapi wa kuwaacha mafisadi watuongozee nchi??? Uzalendo ni upi kulala gizani kisa Umeme wa dhararu kila kukicha ili wajanja wauze generator ???

  Tusemeni imetosha, imetosha kudanganywa imetusha kuibiwa.

  M4C

  Chief Mkwawa wa kalenga
  Maisha bora ni haki yangu -kulipa kodi ni uzalendo wa kweli. Kuipenda nchi yangu ni vitendo.
   
 2. M

  Mercyless JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Tupo pamoja Chief.
   
 3. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Tanzania njema ni kazi yangu na yako
   
 4. K

  KISAKA MORIS JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ucjali pamoja sana ndugu'
   
Loading...