KAZI kubwa ya madiwani wa Manispaa ya Arusha kupitia Chama cha Demokrasia na Maendel

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
KAZI kubwa ya madiwani wa Manispaa ya Arusha kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo ni ukusanyaji na kudhibiti watu wanaotafuna mapato ya halmashauri na
kukwamisha ya maendeleo ya wananchi.

Akizungumza Majira Arusha juzi, Diwani wa Kata ya Kimandolu, Bw. Estomih Malla alisema yeye pamoja na wenzake watahakikisha fedha zote zinazokusanywa kutoka vyanzo vyote vya mapato ya halmashauri zinatumika kwa miradi iliyokusudiwa na lazima thamani ya mradi huusika ilingane na kiasi kilichotumika.

“Sisi tunaingia pale halmashauri tukiwa na tabia kama ya paka. Tunakwenda kukamata panya walioko pale wanaotafuna fedha ambazo zingeenda kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi. Kwa kipindi cha miaka mitano ya uhai wa baraza hili tunataka wananchi waone umuhimu wa kuwepo madiwani wengi kutoka vyama vya upinzani,” alisema Bw. Malla.

Alisema kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato na kudhibiti ubadhirifu, fedha za miradi ya maendeleo itapatikana na hivyo huduma za kijamii zitaboreka tofauti na hali ilivyo sasa ambapo licha ya mapato kutokusanywa ipasavyo, hata kiasi kidogo kinachokusanywa kinafujwa na watendaji wasio waaminifu kwa matumizi yasiyolenga maendeleo ya wananchi.

Bw. Malla aliyekuwa mgombea wa nafasi ya umeya katika uchaguzi uliogubikwa na utata kamwe hawatatumika kama muhuri kupitisha mambo yasiyozingatia maslahi ya wananchi, badala yake watasimama imara kupinga na kudhibiti mambo yote yanayolenga maslahi binafsi au kundi fulani ya watu.

Kambi mbili za madiwani wa Manispaa ya Arusha wamejitangazia mameya, mmoja kutoka CHADEMA ambaye ni Bw. Malla na mwingine ambaye ndiye anatambuliwa na uongozi wa Manispaa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Gaudance Lyimo, diwani wa Kata Olorien.

Bw. Malla alitaja kazi nyingine ya kudumu ya madiwani wa CHADEMA kuwa ni kusimamia ugawaji mzuri wa viwanja na kuchunguza viwanja vyote vya wazi vilivyoporwa au kuuzwa kwa matajiri ili kuhakikisha vinarejeshwa kwenye umiliki wa umma.

Kwa muda mrefu, baraza la madiwani wa Manispaa ya Arusha kwa vipindi tofauti limekuwa likituhumiwa kujihusisha na ugawaji na uuzaji holela wa viwanja vya wazi ambapo baadhi ya madiwani akiwemo meya waliwahi kuvuliwa madaraka yao baada ya kuhutuhumiwa kuhusika kwenye uuzaji wa viwanja vya wazi eneo la Kilombero na Makao Mapya.
 
Back
Top Bottom