Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 15,202
- 10,938
Mbunge ataka vitabu vichomwe moto
MBUNGE JIMBO LA CHWAKA
na Irene Mark na Rahel Chizoza, Dodoma
MBUNGE wa Chwaka, Yahya Kassim Issa (CCM) ameitaka serikali kuviteketeza kwa moto vitabu vilivyoandikwa kimakosa mikoa ya Zanzibar kwa kuwa vinapotosha jamii.
Akiuliza swali bungeni jana, mbunge huyo aliitaka serikali kutoa sababu za kuiorodhesha Zanzibar katika mikoa ya Tanzania Bara wakati ni nchi yenye mikoa yake mitano.
Serikali haioni kwamba inapaswa kuitaja mikoa husika ya Zanzibar kwa jambo lolote linalohusu mikoa hiyo badala ya kuitaja Zanzibar kwa kuiunganisha na mikoa ya Tanzania Bara? alihoji mbunge huyo.
Akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Dk. Husein Mwinyi, alisema serikali haiijumuishi Zanzibar katika mikoa ya Tanzania Bara kwa kutambua kuwa Zanzibar ina mikoa yake inayojitegemea.
Alisema iwapo jambo hilo limetokea katika vitabu mbalimbali vilivyowahi kuchapishwa, limefanyika kimakosa na litafanyiwa marekebisho ili kuondoa utata uliopo kupitia vitabu hivyo.
Kuhusu mikoa ya Zanzibar kutajwa katika mikoa inayounganisha Tanzania, Dk. Mwinyi alisema hufanyika hivyo katika masuala ya Muungano na kutoa mfano wa uteuzi wa makamanda wa polisi.
Alifafanua kuwa Serikali Kuu ni ya Muungano wakati Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) si suala la Muungano kwani Zanzibar wana Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Aidha, Dk. Mwinyi alibainisha kuwa Serikali ya Muungano inatambua uwepo wa mikoa 26, yaani mitano Tanzania Zanzibar na 21 Tanzania Bara.
Chanzo: Tanzania Daima, 1/11/2007
Tuambiwe, vitabu hivi vilichapwa wapi? Na kampuni gani?
Iwapo vitachapwa upya, kwa gharama za nani?