Kazi ipo kweli, inamaana CAG na ripoti ya Jairo haaminiki?

Ng`wanakidiku

JF-Expert Member
Apr 18, 2009
1,195
232
Kwa nini watanzania wengi wameshindwa kuamini maamuzi ya serikali (kupitia Ikulu) juu ya suala la Jairo, je ofisi ya CAG haiaminiki tena?
 
CAG kateuliwa na nani?na ana report kwa nani?hapo kuna imani tena iwapo huyo bosi wake wananchi hawana imani tena
 
Huyu vp tena? Hapo jibu ni ndiyo hyo ripot haiaminik! Huyu ni kati ya wale wasukuma gari la jairo anakooonda!
 
Kwa mtazamo wangu CAG kafanyakazi aliyotumwa na wakubwa wake.kwenye maelezo ya ripoti yake amegunda pesa ZIMECHANGWA na zimeingia kwenye akaunti husika ila yeye hana mamlaka ya kisheria kumchukulia hatua mtumishi kazi ambayo alimwachia LUHANJO atolee maamuzi. Kwa makusudi CAG hakutoa mapendekezo kwenye ripoti yake akawa ametega tego kwa jamaa nae akategeka bila ya kumtuhumu JAIRO na kufuatia hatua nyingine ya RUSHWA(TAKUKURU).
CAG big kwa kazi nzuri kugundua pesa zilichangwa.
 
Inachekesha kumpa kazi mkaguzi mkuu kazi ya kukagua fedha zilizokusanywa kifisadi kwa ajili ya mtumizi y kifisadi. Anaeyejua accounting atakwambia CAG atatoa ripoti kwamba fedha zimetumika kwa kusudio sawa! Hii haina maana Jairo hakua na makosa, kimaadili Jairo ni fisadi aliyekusanya fedha kifisadi, kwa rukhsa ya wakuu wake mafisadi na kuitumia kifisadi, na huu ni ufisadi! Kwa hili Jairo, Malima, Ngeleja wangekua kwenye serikali makini yenye maadili wangekua jela hivi sasa! Lakini kwa serikali ya mzee wa kufuturisha, yeye yuko busy kujikusanyia thawabu kwa kufuturisha!
 
Kwa nini watanzania wengi wameshindwa kuamini maamuzi ya serikali (kupitia Ikulu) juu ya suala la Jairo, je ofisi ya CAG haiaminiki tena?

KATIBA MPYA ndio suluhisho la haya maovu yooote. Ndiyo haaaminiki huyo CAG kwa kuwa analinda kibarua chake. CAG inatakiwa watu wa apply wapitishwe na bunge kupata mtu competent, ili wawajibike kwa bunge na sio kwa Rais, haya yameonekana ukiwa na Rais kama wa kwetu, tupo matatani sana. Angalia Kenya sasa hivi, hakuna hiyo power, CJ kapitishwa na bunge. AG na Budget Contoler nao watapitishwa hivyo hivyo.
 
Unajua watanzania ni hatari sana CAG mzuri kama ripoti imetoa kile watakacho akitoa tofauti na walivyotaka basi CAG mbaya. Mimi nakubaliana kabisa na ripoti ya CAG . Sasa Jairo keshakuwa Newsmaker tumeisha sahau maendeleo na mijadala mingine
 
Kwa nini watanzania wengi wameshindwa kuamini maamuzi ya serikali (kupitia Ikulu) juu ya suala la Jairo, je ofisi ya CAG haiaminiki tena?

Nchi inaongozwa na watu wenye kutanguliza masilahi binafsi na kulindana. Serikali yetu haijui maana ya Public trust, nchi zinazojua kuwajiba ni kwamba Jairo hakustahili kuruishwa kazini hata kama hana hatia ili kulinda masilahi ya umma na uaminifu kwa vyombo vya umma. Kitendo cha kumtumia Utoh kumsafisha Jairo, maana yake ni kwamba Utoh na taasisi yake wanabakia na uchafu mikononi. Ofisi ya CAG imeshakuwa contaminated. Wangeliona hilo, Jairo angeachwa na nafasi yake kuchukuliwa na mtu mwingine.
 
Yaani kumbe mlikuwa mnamwamini CAG huyuhuyu nyie kweli kiboko CAG yupo na anakagua daily lkn pesa zinaendelea kuliwa hana jipya mwizi tu
 
Duh! imani yangu imeisha kabisa hasa kwenu nyie mnaojiita great thinkers mnaofanya maamuzi kabla ya kufikiri.
 
Kwa mtazamo wangu CAG kafanyakazi aliyotumwa na wakubwa wake.kwenye maelezo ya ripoti yake amegunda pesa ZIMECHANGWA na zimeingia kwenye akaunti husika ila yeye hana mamlaka ya kisheria kumchukulia hatua mtumishi kazi ambayo alimwachia LUHANJO atolee maamuzi. Kwa makusudi CAG hakutoa mapendekezo kwenye ripoti yake akawa ametega tego kwa jamaa nae akategeka bila ya kumtuhumu JAIRO na kufuatia hatua nyingine ya RUSHWA(TAKUKURU).
CAG big kwa kazi nzuri kugundua pesa zilichangwa.

Inanitia shaka hiyo ripoti. Riport gani ya auditor inakosa mapendekezo? Labda sijui vizuri mambo ya auditing. Tusubiri uchunguzi wa tume teule ya bunge mkuu...
 
Ndio maaana Tundu Lissu anasema, Tanzania tuna "Urais wa Kifalme" na ameuchanana vibaya sana ktk hotuba yake jana. Na bila kufanya mabadiliko hayo, hatutoki ktk hali hii.
 
Kwa nini watanzania wengi wameshindwa kuamini maamuzi ya serikali (kupitia Ikulu) juu ya suala la Jairo, je ofisi ya CAG haiaminiki tena?

Tuanze na wewe ndugu yangu. Je umeamini maamuzi ya serikali kupitia ikulu juu ya suala la Jairo? Je unaiamini ofisi ya CAG katika suala hili?
 
  1. CAG kateuliwa na nani?na ana report kwa nani?hapo kuna imani tena iwapo huyo bosi wake wananchi hawana imani tena
CAG ameteuliwa na anaripoti kwa Rais. Amepewa kazi na Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ameteuliwa na anaripoti kwa rais. Amemchunguza Jairo ambaye naye ameteuliwa na Rais.

Hii ni kesi ya Gorilla kumkabidhi Sokwe mtu.
 
Back
Top Bottom