Kazi hii ya Rais ni ya kupongezwa hata K'njaro ubambikiwaji wa kesi upo

Fred Mwakitundu

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
227
383

Naanza kwa kumpongeza Mh Rais John Magufuli kwa kazi kubwa ya kuendesha nchi na kupigania haki za wanyonge, tumeshuhudia hivi karibuni mkuu wa nchi akitembelea Gereza Kuu la Butimba Mkoani Mwanza na kusikiliza kero za wafungwa na mahabusu, alisikitishwa na kero za wafungwa na mahabusu alisikitishwa sana na wingi wa watu magereza ambapo uwezo wa gereza hilo ni kubeba watu 900 lakini walikuwa zaidi ya 1900.

Mh.Rais alishtuswa zaidi na kesi mbalimbali ambazo zinawakabili mahabusu na kusema nyingi za kubambikizwa, alimwagiza waziri wa sheria pamoja na mkurugenzi wa mashtaka (DPP)Kutembelea gereza hilo na matokeo yake ziligundulika kesi zaidi ya 300 kuwa za kubambikizwa na pamoja na wafungwa kwa ujumla ya idadi hiyo kuachiwa huru.

Akiwa Kongwa Rais aliagiza ofisi ya waziri wa sheria na DPP kuzunguka katika Magereza yote Tanzania nzima kuhakikisha kesi zisizo na mashiko kuondolewa kwani hawezi kuendesha nchi yenye machozi.

Swala limeungwa mkono na jaji mkuu wa Tanzania Prof.Ibrahim Juma, na kutoa mapendekezo kazaa juu ya kupunguza, msongamana wa mahabusu kwenye magereza. Jaji mkuu alipendekeza kuwa makosa yote yawe na dhamana lakini pia kutowakamata na kuwashtaki watu kabla ya upelelezi kukamilika, na pia sheria iweke muda wa kikomo cha upelelezi.

Jitihada za Rais ni za kupongeza na wasaidizi wake wanapaswa kufanyia kazi sawa na mawazo hayo mahiri ya Rais, huu si wakati wa kuangalia nani amekosea bali ni wakati wa kutatua tatizo na kusonga mbele kama anavyofanya Mh Rais.

Baada ya kutafakari na kupitia kwa kina nimegundua hayo mambo ya kesi zisizo na mashiko hata kilimanjaro zipo, japo si vyema kuzungumzia kesi zilizopo mahakamani lakini ipo kesi ya viongozi wa Chama KIkuu Cha Ushirika Mkoani Kilimanjaro(KNCU) wanatuhumiwa kwa uhujumu uchumi kwa kumlipa fidia mwekezaji wa Kampuni ya Ocean Link Shopping Services LTD Cyril Mushi, kiasi cha Shilingi BILIONI 2.9.

Kesi hii ni moja ya kesi zenye utata kwani kwa kupitia mikutano mikuu ya wanachama wa KNCU, ambapo waandishi wa habari huwa tunaalikwa tuliona malipo haya yanapata baraka za waziri mwenye dhamana ya ushirika Mrajis wa ushirika taifa pamoja na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, wote hawa walishirikishwa kikamilifu na kutoa ridhaa ya maandishi Cyril Mushi ambae ndie mwenye Ocean Link alipwe fedha hizo.

Kubwa zaidi fedha hizo ni uwekezaji wa Ocean Link ambapo uthaminishwaji wa mali ulifanywa na Valuer aliyeteuliwa na ofisi ya mkuu wa mkoa na kuja na thamani hiyo. Lakini pia waziri wa kilimo pamoja na Mrajis walishiriki kikao cha pamoja na kujadili fidia hiyo mpaka kufikia 2.9 bilioni alizolipwa Cyril Mushi.

Maswali mengi yanajitokeza hapa.

1. Kama mamlaka zote hizo zimehusika katika mchakato wa kumlipa Oceanlink iweje leo viongozi hawa wa KNCU watuhumiwe kwa kosa hilo?
2. Kama kumlipa Cyril Mushi, ni kosa je waliotoa ridhaa kwa maana ya Waziri na Mrajis, mbona wao hawajaunganishwa na viongozi wa KNCU kwenye kesi hiyo.
3. Lakini pia, iliyomlipa oceanlink ni bodi nzima ya KNCU, kwa nini wanaotuhumiwa ni Mwenyekiti, Makamu mwenyekiti na Menenja mkuu tuu?
4. Je aliyelipwa fedha hizo Cyril Mushi, mbona yeye ameachwa na kutanua kama kumlipa ni kosa? Au kwa kuwa yeye ni mwenyekiti wa CHama Cha mapinduzi(CCM)Wilaya ya Moshi vijijini na mbunge mtarajiwa wa Jimbo la Moshi Vijijini?
5. Sheria ya ushirika inamtaka mrajis kuchukua hatua kunapokuwa na makosa ya kiongozi lakini kwa muda wote hajawashitaki viongozi hao je yeye mrajis hakuona hilo tatizo?

Maswali haya pamoja na mengine mengi yanatufanya tuone kuwa lipo jambo nyuma ya tuhuma hizi na ni miongoni mwa kesi za kuangaliwa.

Washtakiwa hawa wanasota rumande kwa zaidi ya mwaka mmoja na mbaya zaidi wamenyimwa dhamana, lakini pia ni wagonjwa na wazee.

Hata hili Mh, Rais ni la kuangalia.

Naomba kuwasilisha
 
Nafikiri maadam Rais ameshamwagiza DPP kipitia magereza yote nchini naamini walifika gereza la Karanga watashughulikia hili pia kujua ukweli wake
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom