Kazi gani ya kufanya ndani ya kazi nyingine

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,219
Hallo wakuu, nna shost yangu wa ukweli kaniomba ushauri huu hapa chini,

Yeye kazi yake anayofanya haimbani sanaa na anakaa ofisini kwa muda wa masaa Kumi hadi kumi na Moja kila siku.

Sasa anatafuta shughuli ya kumwingizia kipato anayoweza kufanya akiwa hapo hapo ofisini kwake.

Nikaona bora nije huku kwenye wazoefu mbali mbali na wa fani tofauti tofauti nimpatie ushauri wenu.

Asante
 
Ofisi nyingi za serikali hazina water fountain, (ingawa kwa sheria za Health and Safety ni lazima). Shost anaweza kununua maji na kuyauza ofisini.
Yeye kajiajiri kwenye kiofisi chake kidogo tu na kulingana na Huduma anayotoa anatikiwa kuwepo hapo kwa muda wa hayo masaa tajwa hapo juu
 
Kuna ofisi za jirani? Au ni mtaa uliochangamka?
Anaweza kununua microwave, apike pilau usiku mchana akiwa kazini akauzia watu take away iliyopashwa moto
Ni wazo zuri ijapo hiyo sehemu alipo migahawa pia ipo, na pia ni sehemu zenye maduka ya jumla na reja reja
 
Yeye kajiajiri kwenye kiofisi chake kidogo tu na kulingana na Huduma anayotoa anatikiwa kuwepo hapo kwa muda wa hayo masaa tajwa hapo juu
kumbe kajiajiri tayari,nilijua ni muajiriwa ofisi flani..

kama kajiajiri basi aseme ni biashara gani anayofanya au aliojiajiri nayo kisha tumshauri biashara ya kufanya ndani ya biashara yake hiyo hiyo.

huwezi mshauri muuza mkaa au pumba za kuku auze chakula hapo hapo ofisini HAIWEZEKANI lazima ushauri ataopewa uendane au ukaribiane na biashara hiyo hiyo anayoifanya sasa hivi.
 
Akikujibu naomba unitag
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom