Kazi gani nzuri.

Mbangubangu

Senior Member
May 6, 2013
188
69
wadau naomba kuuliza kazi gani nzuri na yenye mafanikio katika maisha ya sasa.Coz kuna wazee wetu walifanya kazi ktk mashirika makubwa bt hali zao sasa sio nzuri.
 
Wizi wa mifukoni, haina interview kinachohitajika sanasana ni mbio tu na kujua vichochoro
 
wadau naomba kuuliza kazi gani nzuri na yenye mafanikio katika maisha ya sasa.coz kuna wazee wetu walifanya kazi ktk mashirika makubwa bt hali zao sasa sio nzuri.

kuzibua vyoo kuna dili kubwa sana halafu hakuna ushindani kule.

 
Kuzoa taka mtaani dili sana kama vp ongea na masha akupe mchongo wa kuzoa taka za mbagala
 
Last edited by a moderator:
Binafsi ninavyofahamu kazi nzuri ni ile ambayo wewe mwenyewe unaipenda toka rohoni, unaifanya kwa moyo mkunjufu bila kunung'unika kwa mtu yoyote. Hii ni pamoja na kuridhika na kipato unacho kipata kutokana na kazi husika. Vilevile, kazi nzuri ni ile ambayo itakuepushia 'risks' wakati ukiwa katika utekelezaji. Kwa mfano, kazi ambayo ina asilimia kubwa ya kukusababishia ajali, maradhi, chuki na watu unaowahudumia na mateso; mara nyingi huwa si nzuri, wengi huzifanya wakati wakiangalia kazi nyingine ambyo itawafaa. Kwa upande wa hawa wazee wetu, wengi wao walikua wakifanya kazi bila malengo na wengi wao walikua waki 'create' vyanzo vingi vya kutolea pesa zao bila wao kujijua na kupunguza kipato ambacho kingewawezesha kufanyia maendeleo. Kwa mfano, kuwa na familia kubwa, kupenda starehe au kutumia pesa kwenye matumizi yasiyo ya lazima.

Note: hii ni kutokana na uzoefu wangu katika maisha ya kibongo bongo!
 
Kazi yoyote halali ni nzuri, busara ya matumizi yako binafsi ndo inapasa kukuongoza ili utambue kiasi gani usave!
 
Kazi nzuri ni ile ambayo mazngra hayana rsk...pia kuwa na pesa si kulpwa mshahara mkubwa ni plan/mipango na kuheshmu matumizi na kuwa na vpaumbele ustake kufanya kila ktu at the same time
 
Back
Top Bottom