Kazi 10 hatari zaidi Duniani

Kazi ya uchimbaji madini hususani dhahabu na kwa niliyoyashuhudia ina hatari kubwa sana kuliko hata huo uvuvi

Unakuta mtu kachimba shimo refu kushuka chini halafu huko chini kaanza kuchimba fonka inayopita chini kwa chini kama handaki. Mtu huyu mara zote yuko jirani na kifo kwasababu hilo likifusi likimfukia habari yake huishia hapo

Kuna watu walifukiwa na kifusi (kule wanaita gema) lilikua ni shimo refu lililotrmbea umbali mrefu ilikua ni ngumu kuwafukua kulingana na zana hazikua za kisasa, tulichofanya sisi nikuenda kuweka msalaba juu tu

Wapo waliokufa kwa mlipuko wa baruti. Sometimes unakuta mwamba unadhahabu nyingi na umekua mgumu hauvunjiki mpaka utumie baruti.

Ulipuaji wa baruti una risk sana kwasababu unakuta umetega baruti na kila uki detonate hali respond sasa hapo itakubidi uende ukakague huwenda nyaya hazikua combined vizuri hivyo baruti haikua armed.

Lakini ghafla tu unakuta umeenda ile unafika tu nayo inalipuka, sasa wengi wamelipukiwa na kupoteza maisha kwa staili hiyo.
 
Mkuu bandiko lako bila kuweka kazi ya ulinzi basi bandiko lako ni fake..

Mlinzi ni target number moja ktk uhalifu wowote ule duniani.

Ila nakubaliana nawewe no 7 ktk uchimbaji wa mafuta.
Ni ya hatari sana..
Tunafanya sababu ya njaa tu.

Licha ya kuchimbwa baharini,,,licha ya risk ya rough sea,,
maana mafuta huchimbwa deep sea,, pia kuna gesi ya H2S ambayo ikilipuka na bila kuwa na vifaa vya oxygen ya kupumulia basi tutakutana mawinguni..
 
10. Kuendesha Malori

Kazi hii ni hatari kwasababu kuu mbili, kwanza ni umbali ambao madereva hawa hulazimika kuendesha gari na la pili ni aina za barabara wanazokutana nazo, nyingi zikiwa ni za hatari sana ikiwemo miteremko na milima mikali.

Kwa hapa nchini Tanzania, maeneo kama Kitonga na Sekenke kwa miaka ya nyuma yalikuwa yakichukua roho za madereva wengi kutokana na mazingira yalivyokuwa hatarishi.

Takwimu zilizokusanywa 2014 zinasema zaidi ya madereva wa malori 700 duniani walipoteza maisha mwaka huo.

09. Askari Magereza

Unaweza kushangaa lakini ukweli ndio huo, hii ni kazi ambayo usipokuwa makini kwa 100% unaweza kupoteza maisha kwa haraka sana.

Asilimia kubwa ya wafungwa ni watu hatari, baadhi yao wamehukumiwa kifungo cha maisha hivyo hawana cha kupoteza, wanaweza kukudhuru bila kuhofia chochote.

Gereza kama la Gldani lililopo Georgia linatumika kuhifadhi wafungwa waliohukumiwa kwa makosa makubwa na ya hatari. Katika gereza hili askari wa zamu hawezi kuwa mmoja. Matukio ya kupigana na ubakaji ni kitu cha kawaida na askari hulazimika kuwa waangalifu wakati wa kushughulika na mambo hayo.

08. Wafanyakazi Kwenye Mitambo ya Nyuklia

Mwaka 2011 kulitokea tukio la nyuklia kuvuja na kusababisha kiasi kikubwa cha mionzi kusambaa. Ili kuzuia isilete madhara ilikuwa ni lazima wataalamu wasogee eneo hilo na kuziba kurudisha katika hali ya kawaida.

Hatari ya kusogea eneo hilo ilikuwa kubwa sana kwavile mionzi hiyo ilikuwa na sumu kali kwa mwili wa binadamu ambapo watu wengine waliaswa kukaa umbali wa kilomita nyingi kutoka eneo la tukio.

Lakini wafanyakazi walilazimika kuendelea kuwepo jirani ili kufunga hali iliyopelekea wengi wapoteze maisha. Hii ni kazi ya hatari hasa.

07. Uchimbaji Mafuta

Wafanyakazi katika machimbo ya mafuta hulazimika kufanya kazi kwa masaa hadi 16 kwa siku. Wakati wakiendelea na kazi wanapaswa kuwa makini mno na mashine zinazozunguka ambapo kosa moja tu linaweza kupelekea ajali mbaya.

Kwavile uchimbaji huu hufanyika baharini, wafanyakazi hawa wanapaswa pia kuwa makini na mawimbi ya bahari huku mafuta yenyewe yakiwa ni hatari namba moja.

Mwaka 2010 wafanyakazi 11 walipoteza maisha katika machimbo ya mafuta nchini Mexico baada ya kutokea kwa mlipuko mkubwa.

06. Mafundi Wanaojenga 'Line' za Umeme

Umeme wa Volti 50 tu unatosha kuondoa uhai wa binadamu, gridi ya umeme huweza kubeba hadi Volti 800,000 unadhani unaweza kuua watu wangapi?.

Fikiria fundi anapanda juu a nguzo kubwa umbali wa takribani mita 50 na kulazimika kuwa makini na vitu viwili;
1. Asianguke chini
2. Asikosee kugusa umeme

Kosa lolote kati ya hayo yanaweza kuuondoa uhai wako ndani ya sekunde chache tu.

05. Mwandishi wa Habari za Kivita

Mwandishi wa habari hulazimika kuingia katikati ya uwanja wa vita ili apate picha na taarifa za matukio zenye ubora zaidi.

Anachoweza kufanya ili kujitetea ni kuwaa kivazi chenye logo ya 'PRESS' kifuani na mgongoni akitumaini hilo tu litamsaidia asipigwe risasi, hii ni kazi inayohitaji moyo wa ujasiri.

04. Wachimbaji Makaa ya Mawe

Mfanyakazi katika migodi ya makaa ya mawe hulazimika kufanya kazi kwa wastani wa masaa 12 kila siku na katika mazingira hatarishi ambayo nafasi ni finyu na unaweza kupata shida ya kupumua kutokana na vumbi la makaa hayo.

Kupumua katika vumbi hili ni hatari sana lakini endapo mfanyakazi atazimia basi tambua kuwa yupo chini ya ardhi kwa umbali wa zaidi ya mita 100. Kama ana bahati basi atakufa muda huo huo, lakini kama hana bahati basi anaweza kunasa huko ardhini na akafa taratibu kutokana na njaa.

03. Upasuaji wa Mbao

Unaweza kudhani msumeno wa umeme ndio kitu pekee cha hatari katika kazi hii, unajidanganya kwavile watu wengi hupoteza maisha kwa kutojua tu ni upande upi mti utaangukia baada ya kuukata.

Ukiangukiwa na mti mkubwa kama huo hapo pichani kunakuwa hakuna namna ya kukuokoa na huo unakuwa mwisho wa maisha yako.

02. Wanaanga

Siku utakayoamua kuwa Mwanaanga basi tambua tayari una asilimia saba za kupoteza maisha ukiwa katika kazi zako.

Kosa moja tu wakati wa kurusha roketi linaweza kusababisha kwenda uelekeo usio sahihi na kupotea, roketi kulipuka, hewa safi ya Oxygen ambayo husafiri nayo kwa matumizi ya huko angani huweza kuvuja au mtu akapotelea angani moja kwa moja.

01. Uvuvi

Kazi hii imeshika namba moja katika orodha ya kazi 10 za hatari zaidi duniani. Utamu wa samaki kwenye migahawa unatufanya wengi tusahau hata mchakato wa upatikanaji wake.

Hii ni kazi ngumu na ya hatari sana wala si masihara. Mfanyakazi hulazimika kufanya kazi kwa masaa hadi 24 kila siku akipambana kumwaga maji nje ya boti, kunyanyua vitu vizito na kuwa makini na mawimbi ambayo yanaweza kumuondoa mtu yeyote kwenye boti.

Ukimuuliza mkongwe yeyote wa kazi hii kama aliwahi kunusurika na kifo majini basi atakuambia 'NDIO'.View attachment 1766905
Mkuu tuheshimishe na sisi.
Hata uandishi wa nyuzi JF ni kazi ngumu (unaandika kwa dakika 10, harafu uzi unafutwa)
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Kipindi kama hiki cha pandemic, ungeongeza na wahudumu wa afya (manesi, madaktari n.k)...

Pia sijaona wajeda, wale wenye wako mstari wa mbele kwenye mapigano...

Halafu kuna bomb squad, hawa ni wale wategua mabomu yawe ni ya ardhini, au yaliyotegwa kwenye majengo, watu n.k. Kosa moja tu uhai unakuwa ni juu ya maulana kuulinda
 
Hili andiko halijafanyiwa research hata kidogo. Mwandishi ameelezea kazi anazohisi ni hatari tu. Yaani kazi ya uandishi wa habari za vita ni hatari kuliko kazi yenyewe ya wanajeshi wanaopigana hiyo vita? Au hao sio kazi wanafanya?
Huyu mtu anaweza kunishawishi kuwa kuendesha lori ni hatari zaidi ya kuendesha bodaboda? Au anaongelea ulaya tu?
Au kuna kazi ya hatari zaidi ya kuwa mwanasiasa wa upinzani Afrika?
 
Mimi naona kua mpinzani Hasa wa siasa ni kazi hatari zaidi wakati wa jiwe kuliko hizo kazi ulizozitaja
 
Source ?


Umekaa ndo ukafikiria hicho
me naomba nikuulize swali zipi ni kazi salamaa?
Mkuu just relax kazi zote zina changamoto zake! lakini kuna zingine zina changamoto zaidi baadhi nimejaribu kuzielezea na zingine wadau wanajazia. Kuna kazi mtu anaweza kufanya na mwingine asiweze kwa sababu kazi hiyo ni pasua kichwa.

Imagine unaambiwa ukafanye kazi maalum mshahara mnono wale wahalifu wanaopewa hukumu ya kifo yaani ananyongwa mpaka kifo wewe ndo unapewa kazi hiyo ukatekeleze utaweza? na mafunzo utapewa utaweza? lakini kuna watu wanaweza!
 
50. Ualimu
Kumchapa mtoto muhuni au wa tajiri ndo utajua hujui
49. Ujangili
Kuua wanyama wenye hasira kali ni shughuli alaf jangili anawindwa na serikali na wanyama wenyewe
48. Ugaidi
Mda wowote unapewa bomu ukajitoee muhanga.
47. Snitches
Hii inaeleweka
46. Wizi
Anytime arubaini yako itafika ndo utaona cha mtema kuni
45. Ushabiki
Unaweza ukakaa uwanjani ukapigwa mpira wa pua au unaweza ukabet na mtu kuhus timu yako then result ndo utajua hujui
44. Kwenda disko
Siku umetoka disko mida ya saa 8 ukakutana na sungusungu ndo utajua hujui
43. Music
Huku mnaweza mkaekeana mabifu mpaka mtaanza kupigana hiyo yote mwishowe kuuana
42......1
List ni ndefu saana.
 
Back
Top Bottom