Kaya 15,000 wanajisaidia vichakani wilayani Mbogwe, Geita

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Kaya 15,000 kati ya kaya 37,000 hazina vyoo wilayani Mbogwe mkoani Geita zikiacha wananchi wengi wakijisaidia milimani na vichakani hali inayohatarisha afya na kusababisha uwepo wa magonjwa ya kuambukiza yanayosababishwa na uchafu. Afisa afya wilaya ya Mbogwe ndg Ezekiel amesema hawawezi kupona magonjwa, lazima waugue magonjwa ya kuharisha damu na kipindupindu.

Kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Mbongwe, afisa tarafa wa wilaya ya Mbogwe amesema pesa zimetengwa kiasi cha milioni 83 kuendesha kampeni ya usafi wa mazingira kwa mwaka wa fedha 2015/16.
 
Back
Top Bottom