Uchaguzi 2020 Kawe, Dar: Yaliyojiri mkutano wa Dkt. Magufuli katika viwanja vya Tanganyika Packers

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,966
Jua linachomoza, madimbwi yamekauka kwa Upendo wa Mungu na watu kwa maelfu wanaelekea viwanja vya Kawe Tanganyika packers kumsindikiza kipenzi cha watanzania Dr Magufuli.

Karibuni nyote.

Rip Mwalimu Nyerere

Up dates;

DKT. BASHIRU: SIFA YA MAENDELEO YA WATU NI KUJITAWALA WENYEWE

Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru amesema Rais Magufuli ambaye pia ni mgombea urais kwa tiketi ya CCM ameleta maendeleo ya watu kwa kuwa maendeleo ya watu huanza kwanza kwa uwezo wa kujitawala

Dkt. Bashiru pia amesema maendeleo ya watu ni kuchapa kazi, na amemsifu Dkt. Magufuli kuchapa kazi hata akafanikiwa kupata gawio la Tsh Bilioni 100 la dhahabu alilopokea Oktoba 13

Aidha amesema mahusiano ya watu pia ni sehemu ya maendelo ya watu ambayo amesema ni Dkt. Magufuli aliyeyaleta kwa kusema kuwa maendeleo hayana chama na kuwajali wanyonge

Ameyasema hayo katika mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe


DKT. MAGUFULI: ALIYESHINDA KURA ZA MAONI KAWE NI MTOTO WA DADA YANGU LAKINI SIKUMRUDISHA
Aliyeongoza kwenye kura za maoni ni mtoto wangu, mtoto wa dada yangu. Anaitwa Furaha. Lakini nikasema hapana. Aliyefuatia aliwahi kuwa Mbunge wa East Africa, nikasema hapana. Nimewaletea Gwajima aje afufue maendeleo ya Kawe.


DKT. MAGUFULI: ALIYEKUWA MBUNGE WA HAPA HAKUWAHI KUNIOMBA
Mgombea urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Magufuli amesema Oktoba 13, alipigiwa simu na Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM kuhusu adha za wananchi wa Basihaya

"Ningeweza kutoka Ikulu na kwenda moja kwa moja kwenda Tanganyika Packers. Lakini jana Gwajima pamoja na Diwani waliniambia kuwa kuna sehemu za Kawe zimeharibika kutokana na mvua, nikasema nitapita kuona."

Amesema aliyekuwa mbunge wa Kawe, jimbo ambalo Bashaya ni sehemu yake, hakuwahi kumuomba kuhusu shida ya mitaro ambayo ilifanya makazi waingiliwe na maji kwa mvua iliyonyesha jana

"Na mimi nafahamu hapa huwa kunakuwa na maji mengi. Watu wanapata shida. Lakini sijawahi kuombwa hata siku moja kwamba wananchi wa hapa wanapata shida."

Aidha amemtaja Gwajima kuwa aliwatembelea wananchi hao na kusaidia kuokoa vitu vyao vilivyokuwa vikichukuliwa na maji

Magufuli amesema serikali imetenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa mitaro mkoani Dar es Salaam

"Tumetenga bilioni 32 kwaajili ya kushughulikia mitaro [jijini Dar Es Salaam]. Bilioni 5 nitazileta kuja kushughulikia hapa. Lakini tukubaliane, musinichanganyie [na viongozi wa Upinzani]. Huwa naumia sana. Miaka 10 bado hamuelewagi tu?"


DKT: MAGUFULI: VYAMA VYENYE BENDERA VYENYE RANGI NYEKUNDU VINAASHIRIA MABAYA
Katika Mkutano wa kampeni wa mgombea wa urais wa kupitia CCM, Dkt. Magufuli amesema baba wa Tiafa mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipata uhuru wa nchi hii bila kumwaga damu

Leo tunaadhimisha miaka 21 tangu kifo chake. Lakini anakumbukwa kwa kulipatia uhuru taifa la Tanzania bila mtu yoyote kufa katika harakati za kuutafuta uhuru

Amesema hiyo ndio sababu bendera ya nchi yetu haina rangi nyekundu, tofauti na nchi nyingi za Afrika ambazo zina rangi nyekundu

Amesema kuna baadhi ya vyama vya siasa vina rangi nyekundu, ambavyo haviashirii dalili nzuri. Dkt. Magufuli ameyasema hayo alipokuwa Tegeta kwa Ndevu akielekea Kawe kufanya mkutano wa Kampeni.


DKT. MAGUFULI: BABA WA TAIFA ALITUACHIA UHURU, MUUNGANO, UMOJA NA MSIKAMANO. TUVIDUMISHE
Kufuatia kuibuka kwa ugonjwa wa Corona, yalitolewa maelekezo kila nchi kufunga mipaka yake na iwazuie raia wake kutoka nje. Sisi tukasema hapana. Nilifanya haya kwa kuzingatia misingi tuliyoachiwa na Baba wa Taifa katika kulinda uhuru wa Taifa letu

Baba wa Taifa alituachia Amani na Utulivu Hii ni tunu kubwa. Baba wa taifa alipigania amani ndani na nje ya mipaka…amani ni msingi wa maendeleo ya Kiuchumi wa Taifa letu.

Baba wa Taifa alituachia Umoja na mshikamano. Watanzania tunaishi bila kubaguana kwa makabila yetu. Muungano unajenga undugu, Muungano unajenga biashara.

Tuna mashirikiano katika nchi za EAC, zaidi ya watu milioni 165 na SADC zaidi ya watu milioni 400. Muungano huleta faida.

Jambo linguine alilotuachia Baba wa Taifa ni kujenga Taifa lenye kujitegemea. Baba wa taifa alianzisha mipango ya kuiwezesha nchi kujitegema kwa kuanzisha viwanda na mashirika mbalimbali.


DKT. MAGUFULI: BARABARA JIMBO LA KAWE TULIZIJENGA WENYEWE ‘KWA NGUVU’, HATUKUOMBWA
Nilipokuwa nawauliza Waziri wa Ujenzi ni miradi ipi ya barabara hata za mitaa zilizoombwa katika jimbo la Kawe, kwasababu maendeleo hyana chama, mimi nataka kuwatumikia Wana Kawe, ninaambiwa hakuna aliyewasumbua

Ilibidi miradi mingine tuifanye kwa nguvu, kwa kutambua jiografia ya Kawe. Ile barabara kutoka Tangi Bovu kuunganisha Mbezi ilibidi niifanye kwa nguvu zangu mwenyewe. Ile barabara ya kutoka kona ya Wazo Hill kwenda kutokea hadi kwa akina Kawawa kule, tuliifanya wenyewe kwa nguvu zetu. Hata hii barabara ya Ununio na barabara nyingine za kwenda baharini tuliamua kuzifanya kwa nguvu kama serikali kuu.


DKT. MAGUFULI: MBUNGE USIPOJENGA MAHUSIANO NA WAZIRI HUWEZI KUPATA MIRADI
Nimekuwa Mbunge kwa miaka 20, na miaka 20 nimekuwa Waziri. Kazi ya Mbunge huwa ni kujenga mahusiano na mawaziri wa wizara husika. Usipojenga mahusiano huwezi ukapata miradi. Usipojenga mahusiano na Waziri wa Maji, huwezi ukapata miradi ya maji; watapata wenzako wanaowahi. Usipojenga mahusiano na Waziri wa Afya, huwezi ukapata vituo vya afya, huwezi kupata hospitali – utapata vya mwisho mwisho.

Muliowachagua Kawe hawakujenga mahusiano na Mawaziri ndiyo maana Jimbo la Kawe lenye watu mamilioni halina hata hospitali kubwa ya kufanya operesheni. Wilaya ya kigamboni ni mpya, ilianzishwa mwaka 2016, lakini ina hospitali kubwa mbili za kufanya operesheni.

DKT. MAGUFULI: NINGEPENDA KUPITA KILA MAHALI LAKINI NITATUMA VIONGOZI WENGINE
Nilipenda sana kupita maeneo mbalimbali. Nilipenda nifike Mbagala; nitamtuma Mheshimiwa Jakaya Kikwete. Nilipanga niende mpaka Ukonga mwisho, napo nitamtuma Mh. Jakaya Kikwete na viongozi wengine.

Nilipanga kupita kila eneo, lakini mimi ni binadamu. Ningependa hata nifike Katavi na Rukwa lakini ilibidi nimtume Makamu wangu wa Rais, Mama Samia.

Ningependa nifike Mtwara na Lindi lkini nitamtuma kule Waziri Mkuu wangu, Ndugu Kassim Majaliwa.

Ningependa nifike Morogoro; ningependa nifike Pwani; ningependa nifike Pemba na maeneo mengine. Mimi ni binadamu, siwezi kuwa kila mahali na wakati huohuo nifanye kazi za serikali. Kwasababu serikali lazima iendelee kwenda, wafanyakazi wapate mishahara yao. Madawa lazima yapatikane hospitali. Na mengine mengi. Wakulima lazima wapate pembejeo. Hatya yote unayasimamia wakati ukifanya kampeni.


DKT. MAGUFULI: SIKU YA KUPIGA KURA HAITOFUNGANA NA SIKU ZA IBADA. NITATANGAZA MAPUMZIKO
Tarehe 28 tukafanye yaliyo ya kweli. Musidangwanywe mukaambiwa Magufuli tayari ameshinda. Siwezi nikashinda bila kupigiwa kura.

Tarehe 28 hata kama mtu anaumwa, mpeleke akapige kura.

Uchaguzi wa mwaka huu tumeufanya usiingiliwe na siku ya ibada. Hautafanyika Ijumaa, Jumamosi wala Jumapili – itakuwa Jumatano. Na siku hiyo nitaitangaza kuwa ya mapumziko. Lakini ukapige kura kwanza.


DKT. MAGUFULI: WASANII HAWA NI WANA CCM, WAMEKUJA KWENYE CHAMA CHAO
Wapo wagombea wenzangu wanaojua lazima watashindwa…We mkutano kama huu utaulinganisha na vimkutano vyao huko?

Ati wanasema watu wanahudhuria wengi kwasababu ya muziki. Kwani Mwamposa anacheza muziki hapa wa Ndombolo? Kwani Sheikh Mussa amekuja kucheza muziki hapa? Wanamuziki hawa ni wanaCCM, kwani wameambiwa wanamuziki hawatakiwi kuwa CCM? Wamekuja kwenye chama chao, wamekuja kusherehekea na wanachama wenzao. Wamekuja kusherehekea dalili za ushindi.

Na tena tutashinda vibaya mwaka huu!

0196358B-B910-4B2B-AE5F-52B593BECAAB.jpeg
 
Vipi leo mnasomba watu kama ng'ombe kutoka wapi, juzi hapa kinyerezi walilazimisha kila mwenyekiti wa mtaa alazimishe watu 30 na makosta yanabeba,kama mnapendwa watu watakuja wenyewe kwanini mnaforce watu?yaani mnajitekenya aibu gani hii kwa chama tawala ,mmekosa mvuto
 
Vipi leo mnasomba watu kama ng'ombe kutoka wapi, juzi hapa kinyerezi walilazimisha kila mwenyekiti wa mtaa alazimishe watu 30 na makosta yanabeba,kama mnapendwa watu watakuja wenyewe kwanini mnaforce watu?yaani mnajitekenya aibu gani hii mwa chama tawala .mmekosa mvuto
Tunaanzia safari kwenye office za CCM mtaa, Kila mtaa una coasta za kutosha watu wake tayari na magari binafsi pia.
Sema wewe uko mtaa gani nikupitie

johnthebaptist wakaribishe wanaotaka kujiunga CCM leo
 
Back
Top Bottom