Kawawa kuzikwa leo jijini Dar es Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kawawa kuzikwa leo jijini Dar es Salaam

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Jan 2, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  Kawawa kuzikwa leo jijini Dar es Salaam
  [​IMG]
  Friday, January 01, 2010 1:03 PM
  MAZISHI ya marehemu yanatarajiwa kufanyika leo kuanzia majira ya saa 7 za alasiri huko nyumbani kwake Madala Kunduchi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Marehemu Kawawa alifariki jana, majira ya saa 3:20 za asubuhi, katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako juzi alifika hospitalini hapo kwa ajili ya kuangalia afya yake.

  Akiongea na waandishi wa habari kwa huzuni Ikulu, Raisi Kikwete alisema Mzee Kawawa alifika hospitalini hapo juzi kwa ajili ya kwenda kupima malaria kwa kuwa alikuwa na safari na alienda hapo ili aweze kujitambua kama angekuwa na malaria ajitibie kabla ya kwenda safari yake hiyo.

  Alisema alipofika hospitalini hapo alipima malaria na kukutwa kuwa hakuwa nayo, na alianza safari ya kurudi nyumbani kwake, kabla hajafika nyumbani kwake hali ilibadilika na waliongozana nae walimrudisha hospitalini hapo na jopo la madaktari walianza kumpima kutambua alikuwa akisumbuliwa na nini.

  Katika vipimo vya haraka haraka madaktari hao waligundua kuwa sukari yake ilikuwa imeshuka sana na kufikia 0.6 hali ambayo iliwafanya madaktari wafanye jitihada kubwa kumshughulikia kurudisha hali yake ikae sawa.

  Mbali na kumshughulikia sukari, pia waliweza kugundua kuwa vigo zote mbili zilikuwa hazifanyi kazi na pamoja na jitihada zote mwenyezi mungu alichukua uamuzi wa kumchukua majira hayo.

  Kufuatia kifo hicho Kikwete amesema wamempoteza kiongozi shupavu aliyepigania uhuru wetu wa Tanganyika enzi za mwalimu na kusema alikuwa ni kiongozi mshauri wa karibu katika kuweka hali ya nchi sawa na walikuwa wakimtegemea kwa ushauri wa hapa na pale enzi za uhai wake.

  Marehemu aliweza kushika nyadhifa nyingi enzi za uhai wake kama vile Makamu wa Kwanza wa Rais, Waziri Mkuu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi na vyeo vingine kadhaa.

  Marehemu Kawawa alizaliwa mkoani Ruvuma Wilaya na Namtumbo, Februari 27, mwaka 1926. Alifariki jana akiwa na umri wa miaka 83

  ukitaka kuona picha zaidi bonyeza hapa http://www.nifahamishe.com/album_preview.aspx?AlbumId=677797
   
 2. AlMusoma

  AlMusoma Member

  #2
  Jan 3, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 32
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Inna lillah wa inna ilaihi raajiuun. May his soul be granted a place in janna. Those who have been fortunate enough to have witnessed the political phases over the last three decades will probably agree with me that - like Julius Nyerere and a few others - Mzee Kawawa was undoubtedly a rare breed in our political habitat, an honest leader who always had the people at heart throughout his political life and in his retirement. People talk of role models - what else would one ask for other than learning from these great political figures. Unravelling the factors which transformed Tanzania's political terrain would surely form an interesting PhD title for a political science student using our first phase leaders as cases. How I wish I were a political science don. My condolences to all Tanzanians and particularly to his family - Fatuma, Zalia, Vita, Zamaradi, Farida and others. Again, inna lillahi wa inna ilaihi raajiuun.
   
Loading...