Kawawa ashangaa viongozi kumiliki mabilioni ya fedha

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,047
Posted Date::4/17/2008
Kawawa ashangaa viongozi kumiliki mabilioni ya fedha
Na Muhibu Said
Mwananchi

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Rashidi Mfaume Kawawa, ameitaka serikali kuwasaka viongozi wanaojihusisha na vitendo vya ufisadi nchini na kuwabana waeleze fedha wanazozimiliki namna walivyozipata.

Kawawa ambaye ni mmoja wa waasisi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kiongozi anayeheshimika kutokana na kushika nyadhifa mbalimbali za kitaifa, alitoa kauli hiyo katika mahojiano maalum na waandishi wa habari, muda mfupi baada ya kuzindua kitabu kiitwacho: 'CCM na Mustakbali wa Nchi Yetu', katika hoteli ya Courtyard, jijini Dar es Salaam jana.

Alisema yeye pamoja na watu wengine waadilifu, hawapendi tabia ya kujilimbikizia mali isivyo halali inayoendekezwa na baadhi ya viongozi nchini, ambayo haikuwahi kufanywa na waasisi wa taifa hili, wakiongozwa na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere.

"Hatupendi ulimbikizaji mali wa haramu, hivyo wote wanaojilimbikizia mali kwa njia hiyo, wafuatiliwe, waulizwe, waseme walizipataje," alisema Kawawa ambaye alipata pia kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema Mwalimu Nyerere ambaye ni kielelezo cha uadilifu na uaminifu kati ya viongozi wachache duniani, hakuwahi hata siku moja kujipatia mali kwa njia zisizo za halali.

"JKT (Jeshi la Kujenga Taifa) walimjengea nyumba, alikubali kwa sababu alihitaji nyumba. Sijui kama alikuwa na uwezo au alikuwa hana wa kujenga hiyo nyumba, ila hakuwahi kujipatia mali kwa njia za haramu," alisema Kawawa ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Mstaafu.

Alisema mbali na Mwalimu Nyerere, hata yeye (Kawawa) hadi anastaafu kazi serikalini na katika chama, hajawahi kujipatia mali kwa njia za haramu.

"Ningeyapata wapi hayo mabilioni ya shilingi?," alihoji Kawawa ambaye ni Katibu Mkuu wa kwanza wa CCM.

Kuhusu Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge ya kuyaita mabilioni ya shilingi anayotuhumiwa kuyahifadhi katika akaunti ndani na nje ya nchi kuwa ni "vijisenti", Kawawa alisema: "Hayo ni maoni ya mtu, kila mtu ana maoni yake".

Alipoulizwa, ni hatari gani inayoweza kukikumba chama baadaye kutokana na ufisadi, alisema kwa ufupi: "si jambo zuri".

Kauli hiyo ya Kawawa inatokana na kuibuliwa tuhuma za ufisadi na ulimbikizaji wa mabilioni ya shilingi kwa njia za haramu, kunakodaiwa kufanywa na baadhi ya vigogo, wakiwamo viongozi wa serikali na kulisababishia taifa hasara kubwa.

Zaidi ya Sh133 bilioni zilithibitishwa na serikali kupotea katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika mazingira yanayosadikiwa kuwa ni ya kifisadi.

Mbali na hilo, Waziri Chenge, ambaye juzi alikiri kuchunguzwa na vyombo mbalimbali vya kitaifa na kimataifa, anatuhumiwa kumiliki dola 1 milioni (Sh1.2 bilioni) katika akaunti iliyoko katika kisiwa cha Jersey, nchini Uingereza katika mazingira ya kutantanisha, yanayohusishwa rushwa ya ununuzi wa rada ya kijeshi miaka iliyopita.

Awali, akitoa nasaha katika uzinduzi wa kitabu hicho, Makwaia wa Kuhenga, Mhadhiri Mwandamizi Mstaafu wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Issa Shivji alionyesha kushangazwa kwake na mabadiliko ya uongozi nchini, kutoka kwenye utumishi wa umma kuwa mradi kwa baadhi ya watu.

"Kila siku hivi sasa, kwenye magazeti utasikia ufisadi. Lazima tuhoji, kwa nini uongozi umekuwa mradi badala ya utumishi wa umma?," alihoji Profesa Shivji.

Kawawa ambaye amewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), pia alitoa ushauri kwa wana CCM kudumisha utamaduni wa kujikosoa na kukosoana ili kuleta mabadiliko katika chama na taifa kwa jumla.

Kawawa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa kwanza wa chama hicho, alisema tangu enzi za TANU na ASP hadi sasa, CCM imekuwa na utamaduni wa kuwa na mijadala katika mambo mazito yanayohusu chama na taifa na kwamba, hakiogopi kukosolewa kwa kuwa Mwongozo wa chama hicho wa mwaka 1981 umetamka bayana kwamba kujikosoa na kukosoana ni silaha ya mapinduzi.
 
Indeed, all ministers must now state as clear as possible who got what where when and why, and what does it mean. Tumechoka sasa.
programming.gif
 
kama na mzee nae kamuua Chenge kisiasa ni bora aachie ngazi maana kitachofuata hapo ni aibu ya mpaka kufa..
 
Huyu pimbi sijui naye kaibukia wapi,hawa ndio misingi waliyojenga imetufikisha hapa...anyamaze tuu maana hana jipya kabisa!
 
Huyu mzee naomba akae kando, ujinga huu waliuanzisha wenyewe kwa siasa zao za Kiimla.

Huu muziki ni sisi tu tunao weza kuucheza kwa minenguo yote bila kujikanyaga.
Wao wazee wa CCM wameanza sisi tutamalizia na kuwamaliza wote, ni suala la muda tu.

Siasa za kina Kawawa na Kingunge na vishahibu vingine vyote hazina nafasi tena kwenye hili Rumba kali.

Kizazi cha akina Chenge kimeanzisha Soo hili, kizazi chetu kitajibu mapigo vizuri sana na kwa usahihi.

Ombi langu ni moja tu, tukianza kujibu mapigo watu wasianze kutuita maharamia na kusema tumekosa Uzalendo.

Jino kwa Jino.
Moto kwa Moto.
Fedha kwa Fedha.
 
Yaani all this time watu wanapiga makelele ndio sasa anaongea?
Tena ni mtu ambaye era ya nyerere ambaye tulitegemea angejitokeza mapema kama butiku kuwasema hawa....huyu lazima walimlisha hawa watu.
 
CCM ni lazima imeguke na zaidi imeguliwe kwenye madaraka ndipo hapo kisanga kitapopata uhai ,hivi ni nani ambae unafikiri ufisadi hajaufanya ,hawa mawaziri wangapi wamepita tuanzie na Mwinyi ambae yeye kama utayachunguza haya mambo basi ndie mhusika mkuu ndipo kwenye utawala wake mambo yalipoanzia kuharibika ,huyu si ndie wakimwita mzee rukhsa ,hiyo ndio picha halisi haya mawaziri wake wangapi wamepita unaijua ni ruhusa gani walichukua ,wangapi wapo nchini ,baadae alitua Mkapa yeye ndio huna la kusema ,aliifanya Ikulu kama Tandika magengeni yaani Mkapa ndio nae alifurahia kwa mara ya kwanza kuona faida ya kufungua biashara ya genge na kuigeuza ikulu sehemu yake ya kuuzia genge ,yeye na mawaziri wake ndio hao leo wamebaki kwenye nyavu za Kikwete wakiruka ruka ,kila mmoja anamshinda mwenziwe kwa kusanya feza wakati wa Mkapa ,wamesoma kwa mkapa na kuweza kufaulu ni namna gani wataanzisha makampuni na kuchota feza yote ya benki bila ya kukamatwa au kuwepo ushahidi maana hayo makampuni hivi sasa hayajulikani hata yalipo ,tumebaki kupapasa na kwa ufundi mkubwa wameunda takukuru na Pcb wakijua ni yao wenyewe Kikwete amedandia tu na hataweza kuibua mitandao iliyomo ndani,ila waliokwama na biashara hii ni hawa mawaziri wa Kikwete maana mambo yamechafuka bado serikali inayumba.
 
kwi..kwi..kwiiii! Sasa yeye mwenyewe mbona haongelei yale maeneo matatu ya kuwindia aliyopewa na BM...hehheheheh!
CCM kiboko,wakiwa nazo wanatumia wanakuwa washkaji,likibumbuluka,eti kila mtu anashangaa! Sasa cha kujiuliza ni kwamba inakuwaje Chenge apate kura nyingi kuliko wagombea wote kwenye uchaguzi wa NEC kama haikumaanisha yeye ndio alitumia pesa nying1 kuliko wote? Sasa wanashangaana nini sasa hivi! Hypocrites
 
Ama kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni ! pamoja na watu kushangaa jamaa bado anadai hivyo ni vijisenti tu namhurumia sana JK amefuga mbwa ili wazuie wezi kwenye mji wake Instead mbwa hao wameanza kuuma kila mgeni aingia kwake hana la ziada ila ni kuua mbwa wote na kutafuta ulinzi mwingine vinginevyo atajikuta alone mwaka mzima bila kupata wageni
 
Mzee Kawawa anashangaa na kushutumu jambo hili kwa sababu alifuatwa na kuombwa atoe maoni yake, vinginevyo angekaa kimya. Kwa sasa yeye naye kama alivyo kingunge ni watu wanaofaidika na mtindo wa sasa wa uongozi hasa tangu era ya 3 na hii ya sasa ambapo mwenye sauti ni yule mwenye pesa na kwamba muhimu si wananchi bali kina nani wana maslahi katika uongozi wangu na wapate nini. Kawawa tulia.

Kuna wengine wanafikiria kwa kutumia matumbo, they are dead from the neck above
 
...... inakuwaje Chenge apate kura nyingi kuliko wagombea wote kwenye uchaguzi wa NEC kama haikumaanisha yeye ndio alitumia pesa nying1 kuliko wote? Sasa wanashangaana nini sasa hivi! Hypocrites[/QUOTE]

Hii ndio aibu kubwa kwa CCM na wanachama wake,yaani imebaki kununua na kununuliwa basi. Mwenye pesa anawanunua wajumbe kama anavyonunua perege sokoni na kuhakikisha kicheko cha mjumbe lazima aone jino la mwisho,Mjumbe naye badala ya kutumia fursa aliyoipata ya kupiga kura kumweka kiongozi bora anageuza kichwa chake kuwa box tupu kwa kununuliwa kama kondoo mnadani bila ya kujali heshima yake wala wale waliomtuma kuwawakilisha kupiga kura.
Ndio maana pamoja na dharau na majivuno na kauli zake chafu bado alipata kura kibao uchaguzi wa NEC,shauri ya "visenti" alivyotoa.
Ukweli ni kuwa sasa hivi CCM INANUKA KABISAkwa uozo uliopo. Wazee walisema "La kuvunda halina....."
 
ukweli ni kuwa ukifuatilia wanaoweka viongozi wabovu ni wanachama wa CCM ambao njaa zao hutulizwa kwa muda ifikapo kipindi cha uchaguzi.

viongozi wa CCM na wanachama wake ni uozo mtupu, na hayo ndo matokeo aliyoyataka nyerere kuwa watu wasisome ili wasione mbali. sasa leo mtu mzima anahongwa flana na kofia au doti ya kanga kisha anakubali kumchagua mtu awe mbuge kisha mwenzie anakwenda kula mamilioni ya shilingi bila kukumbuka kile alichoagizwa na mpiga kura wake je hii ni akili?
 
..sitaki kabisa kusikia viongozi ambao hawana cha kuonyesha bali "umasikini" wao.

..sikubaliani na wizi wa waziwazi unaoendelea, lakini CCM wametuchukua msukule kiasi kwamba umasikini umekuwa ni sifa ya uongozi.

..If Kawawa is for real, aanze na kurudisha hekalu alilojengewa na JKT. huyu Mzee ana nyumba madale, kiluvya,dodoma,bomba mbili-- songea, halafu anajidai kuwa ni maskini mwenzetu.

..hii tabia ya kuwajengea mahekalu viongozi wastaafu ndiyo iliyosababisha hawa wa sasa wajiuzie nyumba za serikali kwa bei poa.
 
Mzee Kawawa anashangaa na kushutumu jambo hili kwa sababu alifuatwa na kuombwa atoe maoni yake, vinginevyo angekaa kimya. Kwa sasa yeye naye kama alivyo kingunge ni watu wanaofaidika na mtindo wa sasa wa uongozi hasa tangu era ya 3 na hii ya sasa ambapo mwenye sauti ni yule mwenye pesa na kwamba muhimu si wananchi bali kina nani wana maslahi katika uongozi wangu na wapate nini. Kawawa tulia.

Huyu ndiye aliyetumika kuhitimisha kupewa madaraka mtandao na Mkapa, wakampa nafasi ya mwisho kuzungumza, sasa hivi anachana mihela tu ya bure ya serikali, huku akiwa na mke saizi ya mjukuu wake kama sio kilembwe, hiki kimama kilipoingia tu kikasema hakitaki nyumba ya Kawawa ya zamani maana ina nuksi,

guess what? serikali ikajenga nyingine mpya mara moja, kwa hela za nani? Sisi walipa kodi maana wajinga ndio wali wetu.

Mungu Ibariki Tanzania!
 
Tatizo kubwa la hawa wazee ni kwamba wamefika mahali na kuamini kuwa Tanzania can't be any better than it is now. Kwa hiyo wanataka mabo yaendelee tui kuwa kama yalivyo mpaka watakapokufa. It is a pity!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom