Dr shukuru kawambwa akihojiwa na Seleman mtangazaji wa ITV Katika kipindi cha Dkk 45 leo, kasema wazazi ndo Wenye Jukumu la kuwasomesha watoto wao, hata hivyo serikali itajivua gamba kwa mzigo inayobebeshwa katika Swala la Elimu Kwa watoto wao. Ameongeza kwamba Ghana ni 1% tu inahusika katika swala la Elimu nchini mwake, na Tanzania mzigo wa Elimu ni mkubwa 68.% ukilinganisha na nchi za kusini mwa Jangwa la sahara kama Kenya, Uganda,Malawi,Burundi na Rwanda. Hata hivyo amedadavua kwamba Idadi ya wanafunzi waliokopeshwa na serikali kugharimia Elimu yao ya Juu imepanda hadi kufikia wanafunzi 92,000 kwa mwaka huu ikilinganishwa na Miaka iliyopita ambayo ilikuwa pungufu ya hapo. Huu nauita UmbayuWaYu na Ukong'ota kwa asilimia 100%. Je Tanzania imewekeza vyakutosha katika Elimu?