KAWAMBWA, JuKUMU LA KUWASOMESHA WATOTO NI La WazaZi na sio Serikali.

NIMIMI

Senior Member
Apr 2, 2011
170
16
Dr shukuru kawambwa akihojiwa na Seleman mtangazaji wa ITV Katika kipindi cha Dkk 45 leo, kasema wazazi ndo Wenye Jukumu la kuwasomesha watoto wao, hata hivyo serikali itajivua gamba kwa mzigo inayobebeshwa katika Swala la Elimu Kwa watoto wao. Ameongeza kwamba Ghana ni 1% tu inahusika katika swala la Elimu nchini mwake, na Tanzania mzigo wa Elimu ni mkubwa 68.% ukilinganisha na nchi za kusini mwa Jangwa la sahara kama Kenya, Uganda,Malawi,Burundi na Rwanda. Hata hivyo amedadavua kwamba Idadi ya wanafunzi waliokopeshwa na serikali kugharimia Elimu yao ya Juu imepanda hadi kufikia wanafunzi 92,000 kwa mwaka huu ikilinganishwa na Miaka iliyopita ambayo ilikuwa pungufu ya hapo. Huu nauita UmbayuWaYu na Ukong'ota kwa asilimia 100%. Je Tanzania imewekeza vyakutosha katika Elimu?

Sasa hajiulizi ni kwa nini watz hawawezi kumudu kuwasomesha watototo wao kwa elimu ya chuo?

mnh naingia mashaka na uwezo wa waziri katika kuchambua mambo......................sijui ka kafatilia historia ya nchi yake

ndo kama ivo siku izi kila m2 ni MC (msema chochote) kama uonavyo uchambuzi wa Dr. kawambwa kama sio kukatishana tamaa ni nn?

mkubwa kujieleza F coz swali la mikopo kalizunguka...sasa nazidi kupata shaka na uteuzi wa mawaziri wa jk...kawambwa hafai amechanganya maji..!

Dr Slaa alisema elimu bure inawezeka.hamkumpa kura,sasa angalia tunavyo haha na wadogo zetu.

... serikali kugharimia Elimu yao ya Juu imepanda hadi kufikia wanafunzi 92,000 kwa mwaka huu ...

Ina maana serikali inatumia karibu Tsh millioni 700 (i.e., 92,000 x 7,000) kila siku kulipa posho tu (au mikopo feki) .. achilia mbali direct costs zingine (mishahara, umeme, matengenezo, etc.). Kweli ni mzigo mkubwa kwa walipa kodi. Ndiyo maana hospitali hazina dawa, tunaendesha magari kwenye makorongo, n.k. Ningekuwa policy maker ( .. na wana bahati sitapewa nafasi ..) ningefuta posho na kutoa elimu bure bila tuition fee (kama iliyo kwa elimu ya msingi) ili kupunguza gharama.

.... I know students will HATE me for this post ....

Bora real Dr(Slaa) angechukua nch ila kura yangu ilichakachuliwa ni kwel elimu bure inawezekana,sasa uyo fek Dr(Kawambwa) anatueleza upuuuuz 2...... Oooooh ****

Alichonishangaza ni pale aliposema swala la mikopo mwaka huu nimeangalia vigezo vilivyotolewa na Tume Ya Mh. Jk kwamba 1. Uhitaji na 2. Vipaumbele yaani UaLIMU, UHANDISI na UdAKTARI na aliongezea kwa msisitizo kwamba ambaye alikuwa kwenye vigezo tajwa alinufaika hata kama hakufaulu kwa daraja la 1 & 2 kwani kigezo cha kufaulu kwa viwango vya 1 na 2 hakikuwa kigezo kupatiwa mkopo. Na aliyekopeshwa kugharimia fani ya UDAKTARI ile ni kama RUZUKU kwani hatadaiwa. Pamoja na haya alidai serikali inabebeshwa jukumu ambalo lilipaswa kubebwa na Wazazi wa WANAFUNZI. Uko wapi Uzalendo wa Tanzania kwa wananchi wake?

Mie namuunga mkono maana kwa sasa kila mzazi inabidi apange kulimbikiza hela ya kuwasomasha watoto wake hasa elimu ya juu. Pia uzazi wa mpango ni muhimu sana, utakuta mtu leo anahela za kutosha na miradi kazi yake ni kuzaa tu na mkewe mpaka watoto hata 4 hadi 6 utafikiri ana mkataba na hizo hela kwamba hazitapungua ama kwisha kabisa na anasahau hata kuwawekea akiba watoto kwenye akaunti zao, wakifika Elimu za juu wanaanza kugombana na serikali utafikiri serikali ilimshikia kiboko azae watoto lundo. Mambo mengine hata sisi wananchi tunaweza tukayafanya siyo kila kitu kuitupia serikali. Kaa chini na mwenzi wako panga maisha na yataenda tu

Inatia aibu kweli naye anajivunia kuwa ni waziri,mbona vituko awamu hii ya nne mauzauza matupu kuanzia mwenye nchi mpaka vibaraka wake kasoro wawili watatu

Namuunga mkono shukuru. Hongera Waziri. Wazazi wakati wanazaa watoto hawakupanga na serikali. Mzigo wa kusomesha mtoto ni wa mzazi.

Dr shukuru kawambwa akihojiwa na Seleman mtangazaji wa ITV Katika kipindi cha Dkk 45 leo, kasema wazazi ndo Wenye Jukumu la kuwasomesha watoto wao, hata hivyo serikali itajivua gamba kwa mzigo inayobebeshwa katika Swala la Elimu Kwa watoto wao. Ameongeza kwamba Ghana ni 1% tu inahusika katika swala la Elimu nchini mwake, na Tanzania mzigo wa Elimu ni mkubwa 68.% ukilinganisha na nchi za kusini mwa Jangwa la sahara kama Kenya, Uganda,Malawi,Burundi na Rwanda. Hata hivyo amedadavua kwamba Idadi ya wanafunzi waliokopeshwa na serikali kugharimia Elimu yao ya Juu imepanda hadi kufikia wanafunzi 92,000 kwa mwaka huu ikilinganishwa na Miaka iliyopita ambayo ilikuwa pungufu ya hapo. Huu nauita UmbayuWaYu na Ukong'ota kwa asilimia 100%. Je Tanzania imewekeza vyakutosha katika Elimu?

thubutu wawekeze kwenye elimu kwani watoto wao wanasoma Tanzania hii?.Kwenye budget serikali nadhani huwa wanatenga kabisa hela kwa ajili ya watoto wao kwenda kusoma nje.NANGOJEA MWAKA WATAKAPOSEMA MWAKA HUU MIKOPO HAKUNA IMEIBIWA YOTE,we ngoja tu! Kama washaanza kusema Ghana serikali inakuwa involved kwenye elimu for 1% kuna siku watasema haya mwaka huu sayansi watapata 0.9% ya mkopo na walimu 0.1% tena kwenye ada tu! Fuculty recquirement,meal&accomdation,stationery daily expenditure watajiju.HALAFU huko kwingine 0%.MUNGU SAIDIA MAANA sijui nani kairoga inji hii.

Dr Slaa alisema elimu bure inawezeka.hamkumpa kura,sasa angalia tunavyo haha na wadogo zetu.

ndugu yangu we acha tu! Kufa hatufi cha moto tunakiona na bado na hizo kauli zao we ngoja tu!

Mie namuunga mkono maana kwa sasa kila mzazi inabidi apange kulimbikiza hela ya kuwasomasha watoto wake hasa elimu ya juu. Pia uzazi wa mpango ni muhimu sana, utakuta mtu leo anahela za kutosha na miradi kazi yake ni kuzaa tu na mkewe mpaka watoto hata 4 hadi 6 utafikiri ana mkataba na hizo hela kwamba hazitapungua ama kwisha kabisa na anasahau hata kuwawekea akiba watoto kwenye akaunti zao, wakifika Elimu za juu wanaanza kugombana na serikali utafikiri serikali ilimshikia kiboko azae watoto lundo. Mambo mengine hata sisi wananchi tunaweza tukayafanya siyo kila kitu kuitupia serikali. Kaa chini na mwenzi wako panga maisha na yataenda tu

we kweli kibweka! Hebu assume mama ni muuza maandazi,baba mlinzi pale mint masters mshahara Tshs.90,000/= per month, chumba cha kupanga labda huyu binti/kijana wao kapata hifadhi kwa rafiki yake,mjini hata kijijini kila kitu ni cha kununua. Hivi hapa kuna saving kweli? Hebu jaribu kufikiria kabla ya kuchangia,kama upo DAR tembelea hapo Kisarawe,nenda hadi VIKUMBULU uone wananchi wa vijijini jinsi walivyo na maisha magumu vitoto vinatembe uchi wa mnyama.Ngoja niishie hapa

Back
Top Bottom