SoNotorious
JF-Expert Member
- Sep 11, 2011
- 2,422
- 859
Hivi elimu ya Tanzania ni kwa mujibu wa maelekezo ya wizara au ni kwa mujibu wa sera ya elimu ?
ndio maana wanachukua creme students wanaoelewa kwa haraka ili kwenda na muda. Kumbuka kunawanafunzi wanahitaji nguvu za ziada kufundishwa individualy kitu ambacho private hawataki coz wanaona watapoteza muda!
hakuna mzazi anayelazimishwa kupelka mtoto wake hizo shule za private ni wazazi wao ndio wanawapeleka hasa baada ya kuona kuwa shule za serikali au mnazoziita za kata hazifanyi vizuri.....
kingine ni kwamba hata kawambwa aseme nini hili tammo lake kwa shule za seminari za kikatoriki amechemka wale watasimamia msimao wao labda hizi private zingine hizi....
sijaui kama una ushahidi unaoonyesha kwa wanafunzi wa private wengi wao ndio wanaofanya vibaya kwa kiwango cha kishindwa kuandika hata barua ya kazi....hili siwezi kulizungumzia maana sina ushahidi nalo... na pi mwl kufundisha shule zaidi ya moja kuna sababu nyingi ikiwa ni pamoja na malipo duni wanayoyapata huko serikalini nk..hili ni tatizo la kimfumo..
wastani wa 30% ni mdogo sana...na kama ndio wastani wa serikali basi shule binafsi wasilazimishwe kufata wastani wa serikali....
mzazi kumpeleka mtoto wake shule hata kabla ya matokeo kutoka ni kwa sababu pengine shule husika ina ubora wa hali ya juu na hivyo wazazi wengi kupenda kuwapelka watoto wao hapo so ili kuwahi nafasi basi wanawahi lakini pia hawalazimishwi kufanya hivyo ....mzazi anaweza kusubiri tu matokeo ya serikali na kumpeleka mtoto wake huko....
wewe unatoa mfano wa muhimbili,muhimbili ni hospitali ya serikali,labda ungetolea mfano hospitali ya AMI hapo tungeenda sawa,hizi ni shule za private,hivyo mzazi halazimishwi kupeleka mwanae,cha muhimu hapa ni kuboresha shule za serikali,kuzipa vitendea kazi na walimu.
Viwango vya ufaulu shule zote n vimoja tu sasa iweje wao wapandishe Mara 50,70,80 .Ina maana awataki kuwap heshima watu wanao watawala mpaka wakiuke sheria? Futa leseni zao Mr Kawambwa
Kwa hiyo wewe unaona kuchukua wanafunzi wanaoelewa haraka halafu kuendelea kuwachuja ndio njia ya kuongeza viwango vya Elimu Tanzania?
Unaona sahihi average students kunyimwa haki ya kupata elimu?
unajua hata mwanafalsafa wa zamani plato aliwagawa wanafunzi kwa makundi kulingana na uwezo wao darasani hata walimu wanalijua hilo. Unajua ingelikuwa gs ndo zinafanya hicho kinachofanywa na ps mi nadhani mngekuwa mnahoja za kuongea!
Ukipenda boga penda na ua lake ndichokinachofanyika ps, wewe ukiamua kumpeleka mwanao ps kubali na taratibu zao na kama huwezi basi nenda shule za kawambwa!
Ni aibu kwa taifa lenye mpango wa kuinua elimu halafu inataka alama za ufaulu zishushwe hili halikubaliki kabisa. Serikali inapaswa kujiuliza kwnn ps zinafanya vizuri ktk mitihani ya taifa ukilinganisha na gs na sio kuja na hoja mufilisi eti gs zishushe wastani wa alama zao.
Labda km tu unataka kujipima uwezo wako wa kubishana kwa hoja lakn ukweli unaujua kuwa hii hoja ya kawambwa haina tija kabisa kwa elimu yetu ya tz.
Wewe unaongea nini,darasa linakuwa na watoto 45,then 40 wanafanya vizuri,5 wanafeli halafu unasema mwalimu kasababisha,ulitaka nwalimu amfanyie mtihani???hapo ni dhahiri kuwa either mtoto mwenyewe ni mzembe au IQ yake ni zao la mama mbumbumbu,(according to genetics)
Wewe unaongea nini,darasa linakuwa na watoto 45,then 40 wanafanya vizuri,5 wanafeli halafu unasema mwalimu kasababisha,ulitaka nwalimu amfanyie mtihani???hapo ni dhahiri kuwa either mtoto mwenyewe ni mzembe au IQ yake ni zao la mama mbumbumbu,(according to genetics)
mtoa mada haufaham trend ya elimu tanzania.kama hauhusiki na maswala ya elimu bora usilete mada hizo.acha wanaohusika na maswala ya elimu ndo walete mada hizo.ningekuwa mimi ningediliti thread yangu.
Sasa kwa Mkoa wa Pwani nani anafaa kuwa waziri? Yule mhuni mliwa tigo wa Kisarawe?
Kwa mtazamo huu kuna siku mtaambiwa mnalazimishwa kupeleka wagonjwa wenu Muhimbili, si muwapeleke India na marekani wakafanyiwe checkup?
You are not getting the big picture. Private schools are systematically destroying government schools by artificially gaming with results because they can. When they can't do this anymore and they are forced to work with students they have within the boundaries that are similar to government schools, the bubble will burst. The distribution of students will go back to normal, where you have best performing students,average performing and ones that will perform poorly. Key to these schools is to make sure this number gets smaller by innovating in teaching, not discarding students they can't teach to be best performers.
Ndio shida ya wizara ya elimu kuongozwa na mtu asiye na nasaba na elimu,yeye kaipata kwa bahati mbaya unategemea nini, angependa shule zote zitoe matokeo kama za kata ili seirkali isiendelee kuumbuka, wenye shule binafsi komaa,msikubali kubeba kila kokoro kama ilivyotokea mwake ulee mtoto wa mkubwa iliamiliwa lzima asome FEZA secondary, MWISHO WA SIKU ilikuwa "azungushe", division 4 ya kutafuta kwa torch.
Hapo ndipo umeonyesha udhaifu kabisa watoto 45 wanashinda watano 40 zero hapo ni kosa la mwalimu pamoja na vitendea kazi, sio IQ, haiwezekani wamama na mababa wakapeleka watoto 45 watano ndio wajanja au IQ zao za juu wao peke yao hapo kuna ukosefu dhana mdomo kumwelewesha mwanafunzi.
I would agree if these schools did the same as plato.
Put students according to their level of understanding teach them. mwalimu hakimbii jukumu la kufundisha.
Hoja ya kawambwa iko sahihi, mimi sio mnafki kuping akila kinachosemwa na CCM just for the sake of it.Private schools wakae na MOE wapandishe viwango vya ufaulu vifikie wanvyoona wao vinafaa. Then from then on hakuna biashara ya kila shule kuwa na kiwango chake.
sioni privcate schools zikiongeza kiwango cha elimu tanzania, zaidi ya kuharibu watoto wetu.
Embassy of Japan in Tanzania - Study in Japan
- Undergraduate Students
*Unfortunately no Tanzanian student has passed the screening for several years.
Pingana na wajapani hao hapo.
Wewe ndio unabisha bila sababu za msingi kwa kuamini illusion ya kuwa kiwango cha elimu kinaongezeka kwa kuwa watoto wako wameenda private na wamfaulu necta kwenda kidato cha sita na baadae chuo kikuu.
Kumbe cha maana walichosoma ni vitabu vya nyambri nyangwine na past papers.
I repeat, Private schools are destroying education in Tanzania by removing a healthy balance that must exist.
Ukweli ni fedheha kuambiwa mwanao hawezi kufaulu kwa kuwa ni mjinga na hafundishiki, ni fedheha kutumia fedha nyingi kumsomesha mtoto na mwisho wake anafeli, lakini ni fedheha zaidi mtoto kufeli darasani peke yake, tatizo hapa sio kawambwa tatizo ni muuliza swali, tuambieni kwanza huyo mbunge aliyeleta hiyo hoja anaelimu gani ndio tuendelee kujadili, zipo shule ada yake hadi milioni 15 kwa mwaka, sasa kama toto pumbafu si ni bora nilipeleke kinondoni muslim ada laki mbili.
kuna mama mmoja alizaa watoto wawili na baba tofauti, mtoto mmoja alikuwa kipanga darasani, mama aliuza nyumba yake na kumpeleka mtoto kusoma canada, kwa sasa yule mtoto ni meneja katika benki kubwa na alishamnunulia mamayake nyumba nyingine na magari. huyu wa pili mzazi alifanya kila namna ikashindikana ilishalifungulia shamba la kuku na bata mzinga.
kumbuka shule hizi huchukua watoto kutoka familia zenye uwezo, ukae na litoto lipumbavu hakianani litawatia mimba hadi walimu na shule nidhamu itavurugika na shule itakufa. hebu fikiria unaletewa litoto kama Le Mutuz shule itakuwepo kweli?
mtoa mada haufaham trend ya elimu tanzania.kama hauhusiki na maswala ya elimu bora usilete mada hizo.acha wanaohusika na maswala ya elimu ndo walete mada hizo.ningekuwa mimi ningediliti thread yangu.