Kawambwa aituhumu bodi ya ATCL kuwa haiaminiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kawambwa aituhumu bodi ya ATCL kuwa haiaminiki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Apr 13, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,350
  Likes Received: 5,653
  Trophy Points: 280
  ILIKUWA KAMA SINEMA AMA MOVIE YA WEMA NA KANUMBA PALE MAHAFALI WAWILI MH BALOZI M NYANGANYI NA WAZIRI WA MIUNDO MBINU MH DK KAWAMBWA
  PALE WALIPOANZA KUHOJIWA NA KUTUPIANA MANENO KAMA VILE AWAJAHI KUKUTANA
  WAH HAWA WALIKALISHWA NA KAMATI YA MIUNDO MBINU KUELEZEA KIFO CHA ATCL NA NANI ALIEHUSIKA KUIUA ATCL,,ALIANZA DK KAWAMBWA AMBAE ALILALAMIKIA SANA BODI YA ATCL KWA KUENDEKEZA UTAFUNAJI WA PESA ZA KAMPUNI HASAS PALE SERIKALI WANAPOPELEKA PESA ATCL NDIVYO HIVYO NYANGANYI NA BODI YAKE WANAKAA KUFIKIRIA VIKAO VYA GAFLA KUGAWAIANA MGAO ...HUKU WAKILALAMIKIWA KWA KUJIGAWIA PESA ZA KIKAO KWA DOLLER NYANGANYI AMEKUWA AKIPEWA DOLLER 500NA WENZAKE KUAMBULIA 400DOLLER KILA KIKAO NA MARA NYINGINE WANAWEZA KUFANYA VIKAO 4 KWA WIKI MOJA WAKIGAWIANA PESA MBAYA ZAIDI WAFANYAKAZI WA ATC WAMEKUWA WAKILIPWA MISHARA YAO KILA BAADA YA MIEZI MIWILI NA HUKU WAUNGWANA HAWA KIPEANA DOLLER KILA KIKAO NA HAKUNA VIKAO SIKU INASEMEKANA AKUNA HELA YA KIKAO....

  BAADA YA KUTOA MALALAMIKO MENGI BODI YA NYANGANYI IMEKUWA IKIFUMBIA MACHO UCHAFU UNAOFANYWA NA MENEJIMENT YA ATCL ILIGUNDULIKA TENA NYANGANYI KUPEWA NAMBA KAMA MFANYAKAZI WA ATCL NA KUPATA MKOPO WA GARI AMBAO MPAKA SASA AUJAMALIZIKA KULIPWA HUKU AKIJITAMBA ANAONDOKA MWEZI HUU KAWAMBWA ATAFUTE WATAKAOINYNYUA ATCL....

  MWISHO DK KAWAMBWA AKAHITIMSHA KWA KWELI WANA KAMATI MI TANGU HII BODI ICHAGULIWE NA MENEJIMENT YAKE SINA IMANI NAYO NA MSIONE SERIKALI IMEKAA KIMYA KUTOTOA HELA NI KWAMBA HAWA MABWANA SIKUWAHI KUWAAMINI KABISA KATIKA MUDA WAO WOTE UONGOZINI

  DUH AKAJA MH SANA balozi NYANGANYI.MUSTAFA KAMA MUMJUAVYO MZZEE WA KU FREZE AKAANZA KUMWAMBIA WE KAWAMBWA UNAJUA NI MDOGO SANA KWANGU...PILI KUMBE WAKATI TUNAHANGAIKA SERIKALINI WE UMEKALIA PESA ZA KUENDELEZA KAMPUNI UTUWAMINI..KAMA UKUTUWAMINI MBONA UKUVUNJA BODI,,AMA KUMSHAURI RAIS AVUNJE BODI HUNA IMANI NAYO...MI NAWASHANGAA SANA MAWAZIRI WA SIKU HIZI UNAKAA KUONA KAMPUNI INAKUFA UNAAZA KUTANGAZA NYANGANYI AMEUA ATCL,,,,MWISHO MZEE MUST KAMA AITWAVYO AKAHITIMISHA SASA NAKWAMBI MI NAMALIZA APRIL BODI YANGU TUNAONDOKA KATAFUTE BODI AMBAYO UNAHISI UNAWEEZA KUWAPA PESA NA UKAWAAMINI...AKATULIZWA KIDOGO MZEE AKAJA TENA MI NAWAAMBIA UKWELI AKAWEKE WATU WAKE ANAOWAJUA WAINYNYUE ATCL ILIPO.......

  WATANZANIA HAO NDIO VIONGOZI WETU BAYA ZAIDI KWA AKILI YA HARAKA MNAWEZA KUJUA ,MATAIZO HAYA SRC NI RAIS KIKWETE ANGALIA WAZIRI ANATEULIWA NA RAIS,,MWENYEKITI WA BODI RAIS..WHT NEXTY......RUDI KWA MKURUGENZI WA ATCL ANATEUA RAIS...HUYU RAIS ATATEUA VINGAPI JAMANI ANATUARIBIA NCHI YETU...WABUNGE YEYE NDIO WAKINA SOPHIA SIMBA...NK...HUKU NAKO....

  NA WEWE KAWAMBWA MUDA WOTE ULIKUWA WAPI UJAONGEA KUMWAMBIA RAIS MI SIWAAMINI BODI YA ATCL..UONI KUUMBULIWA HADHARANI AIBU>>ANGALIA DHAMBI ZINAKURUDIA UMEWADANGANYA UMMA NA TUME YAKO YA PROF MSHORO UJASEMA WAMESEMA NINI HUKU ZIKITOLEWA PESA NYINGI KUTUMIKA KWENYE TUME ILE.....DHAMBI ITAKUFWATA MPAKA MWISHO

  WATANZANIA SWALI LINARUDI NANI ANAIUA ATCL?????
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Apr 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Tumia herufi ndogo pdidy..
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,350
  Likes Received: 5,653
  Trophy Points: 280
  kabisaa kazi anayo mkulu wetu na usharika wake mtakatifu
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,350
  Likes Received: 5,653
  Trophy Points: 280
  ahsante mkuu ntatumia ndogo nilipitiwa
  mwana KJ
   
 5. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Huu usimulizi unaonekana kama una kaukweli ndani yake
  Chanzo tafadhali Bwana Pdiddy
   
 6. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  Nahisi aliogopa kuvunja hiyo bodi sababu anaogopa mkuu wake angemuumbua, Hivi ungejisikiaje anvunja bodi leo then baada ya wiki chache anasikia bodi ileile imeteuliwa kusimamia TPDC/NHC. Kifupi Raisi hatuna.
   
 7. k

  kaka2002 Member

  #7
  Apr 14, 2010
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 30
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Mimi nadhani wengi wa wanaopewa nafasi kuliongoza ATC(L) wanamiliki hisa katika mashirika mengine ya ndege. Wanaua kwa makusudi ili kuondoa ushindani wa kibiashara. wamweke DR. MAGUFULI wizara ya Miundombinu anaweza kuleta Tija. Kumeoza sana TICTS, TRL, ATCL, barabara chini ya kiwango kwa gharama kubwa mno na ujenzi kuchukua muda mrefu sana.
   
 8. W

  WaMzizima Senior Member

  #8
  Apr 14, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huu uozo wa ATCL ni bora serikali itafute mtu impe hiyo kampuni for $1, yaani bure. Maana ukweli ni kuwa katika hali ya sasa shirika lina ndege kubwa nafikiri moja au mbili, sasa hesabu za haraka haraka ziko wazi kuwa haiwezekani katika hali ya kawaida kuwa na ndege hizo na wafanyakazi mamia na kutegemea kuwa kampuni itaendeshwa kwa faida.

  Hii ruzuku ambayo serikali kila mara inaendelea kuwapa hawa ni bora tungejengea shule au barabara. Vunja huo uozo ama mpe mtu bure tuachane nao, haina maana yeyote kuwa na hii kampuni, mbona zipo nchi nyingi tu ambazo serikali zake hazina mashirika ya ndege, ndege zao ni za binafsi mi naona bora na sisi tuende huko. Tena sio mpango wa Serikali kubakisha hisa humo (Kama wakati wa SAA na ATCL ambamo walikuwa 50/50) maana hiyo itawapa nguvu hao wawekezaji kuwa wakivurunda serikali itawa bail out. Ni bora wawe nje kabisa ikifa basi na ife hamna mpango wa kuwainua tena, it's ridiculous...

  Hapa wanachofanya ni kutupiana lawama huku ni wazi kuwa kampuni iko hoi...acheni kupoteza hela za walipa kodi, mbona Precision inaenda bila wasiwasi yaani hata Coastal Air ni bora kuliko ATC wakati ATC ina wafanyakazi lukuki...huu ni wizi kwa wananchi
   
 9. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Natamani kujua source ya hii habari ambayo kunaonekana kuna ukweli maana viongozi wa awamu hii hawaachi kutupiana maneno. lakini tukipata source tunaweza kuwa na discussion nzuri sana pdidy. Hata hivyo lawama za kwanza zitamfikia waziri husika maana mpaka ATCL inakufa alikuwa wapi kumwambia aliyeteua bodi kuwa kule hakuna kitu mkuu ili atengue uteuzi?
   
 10. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mustapha Nyang'anyi has never been a performer!!! How comes you expect to perform at his current age if he failed when he was strong and young?!!! Can someone post a proven evidence of his perfomance in the system? He is a Msanii, I say Msanii? Hivi Mamlaka husika zinasubiri nini kumwondoa pale?
   
 11. bht

  bht JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  he was diqualified ab initio!!!
  bora hata wangeniuliza mimi (kama refa) ningewaambia ukweli kabla hawajamgaia 'uenyekiti' wa kampuni muhimu kama ATCL

  NAKUBALIANA NA WEWE HAJAWAHI NA HATAWAHI KUWA 'PERFOMER'.........
   
 12. Bob

  Bob JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2010
  Joined: Sep 10, 2007
  Messages: 277
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Wapewe Precision Air. "Zimwi likujualo..........!"
   
 13. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kwahiyo kwa kifupi aliyemchagua ndiye abebe lawama. Lakini wote ni wakubeba tu lawama maana kama unaona umepewa na kuapishwa kufanya kazi muhimu kama ile kwa ajili ya nchi yako ukaona inakushinda kwanini wala usionyeshe nia ya kujiuzulu? Huyu ni zao halisi la CCM. Hakuna kitu hapo!
   
 14. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ukweli wanaosema wafanyakazi wa ATCL ni kwamba tatizo kubwa katika bodi ile ni Mwenyekiti aliyekuwa anajaribu kuwazunguka wakurugenzi wengine wa bodi na kuwa karibu sana na menejimenti kwa maslahi yake binafsi; ushahidi wa tuhuma hii ni pale Mwenyekiti alipoingilia utendaji wa kukodisha ndege ya kupeleka mahujaji Mecca na kukawa na crisis, ambayo ingeashilia huyu Mwenyekiiti aidha kujiuzuru au kufukuzwa lakini no action was taken; na ikabidi wajumbe wengine wa bodi wajiuzuru as a sign of protest!! Shukuru Kawambwa amekuwa akilihujumu shirika la ndege kwa kutolisaidia bila kufahamu kuwa kuliimalisha shirika hili ni moja ya ahadi za CCM katika ilani yao ya uchaguzi ya 2005!!
   
 15. SOARES

  SOARES Member

  #15
  Apr 14, 2010
  Joined: Jul 6, 2007
  Messages: 88
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Maane, nikwambie, aliwahi kufanya kitu. Alinunua "UNIFLOTE" wakati wa shida kubwa ya usafiri kwenda na kutoka Kigamboni. Tehe tehe
   
 16. Mujuni2

  Mujuni2 Senior Member

  #16
  Apr 14, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi sie yule aliyenunua Kivuko Kibovu (MUST)? watu kama hawa China wangekuwa wameshasahaulika, HANGED & BURRIED period.
   
 17. K

  Kilian Senior Member

  #17
  Apr 14, 2010
  Joined: Apr 26, 2009
  Messages: 147
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Naomba niulize swali nielimishwe hapa kidogo.
  Hivi, Bodi kazi yake si kusimamia utendaji? Huwa inalipwa na nani? Inahusisha wafanyakazi au ni watu wanje tu? Wanatumia vigezo gani kuteua bodi?

  Kinachonishangaza hapa ni hicho kiwango cha pesa wanayolipana kwaajili ya vikao, $500 kwa kikao, (day) ni nyingi sana. Wafanyakazi kwa mwezi wanapata ngapi kama mshahara? Hivi vikao si nisehemu ya ajira ya mfanyakazi? na hivyo vikao vinajadili nini, mbona maendeleo hayaonekani? Kwa mtindo huu hatuwezi kuendelea kabisa.
  Mbona huku kwa wenzetu ufujai huo wa pesa haupo na wanakaa vikao na unaona matokea ya vikao vyao. Ndo maana kweli wnatuzarau sis waafrica kwani hatuna akili kabisa. Ubinafsi umetutawala sana. NATAMANI KUINGIA MSITUNI....
   
 18. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #18
  Apr 15, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hahaaaaaaaaa !!!!!!!!!!!!!!................. Katafute wa kwako.
   
 19. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #19
  Apr 15, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Kama nilivyoeleza awali kwenye similar subject ni kuwa matatizo ya ATC ni complex lakini serikali imechangia sana na hali hii ndiyoi matokeo yake. Serikali imekuwa ikiinfluence kuanzia appointments za juu hadi maamuzi ya shirika. Na vilevile uongozi ndani ya shirika ilikuwa na tabia ya kulindana sana . Matumizi mabaya ya fedha ni kuanzia board member hadi wafanyakazi. Ninakumbuka katika kile kipindi ambapo ATC ilikuwa inaenda UAE, ndani ya ndege ilikuwa wakati mwingine abiria ndani ya ndege nusu ni wafanyakazi[ambao ni wafanyabiashara pia] na mizigo ya wafanyakazi ni kiasi hicho hicho. Safari za kikazi kwa viongozi wa ATC ni mzigo mwingine mkubwa sana maana ingewezekana ku-compute pesa ambazo kwa miaka kumi tu zilizotumika kama allowances [per diems/sitting etc] zingeweza kulipa madeni yote ya shirika.
  Nyanganyi hawezi kukwepa lawama kwani hata kipindi alipokuwa kuwa waziri alikuwa anatabia ya kuingilia sana utendaji wa shirika na matokeo yake ilibidi viongozi mahiri wa shirika hili waliachia ngazi na matokeo wakawa wanaweka viongozi ambao wakiwaongoza remotely.Vilevile kama mnakumbuka scandal ya ukodishaji wa ndege ya mahujaji huyu mzee alijiingiza kwenye utendaji na matokeo yake yakawa aibu.
  Dawa ya kufufua shirika hili ni kuwa serikali iverhaul hilo shirika kwa kustreamline establishment na itoe capital ya kuanzia. Halafu kampuni hiyo ibadilishwe kuwa public company kwa kufloat hisa DSE hii itasaidia kuraise capital na vilevile kubroaden uwajibikaji wa menejiment vinginevyo tax payers wataendelea kuumia kwa kubeba mizigo ambayo haina maana
   
 20. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #20
  Apr 17, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,350
  Likes Received: 5,653
  Trophy Points: 280
  mkuu ilitoka gazeti la nipashe siku hiyo naandika
   
Loading...