KAUTIPE na utumbo wa kuku………………………..!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
Heading isiwachanganye……..Niko hapa Buguruni kwa Mnyamani napata utumbo wa kuku ulioviringishwa kwenye firigisi na chachandu ya pilipili na mbilimbi. Halafu bei powa tu shing mia tano.
Uswazi tunafaidi kweli……………………………….
 
Umenikumbusha hadithi ya enzi hizo "Kautipe utumbo wa kuku" kwenye moja wapo ya vitabu maarufu vya "Ujinga wa mwafrika"!
 
Unaliwa bana, siku ya kwanza kuona nilishangaa hadi kidogo wanichape.

Na miguu ya kuku ya kukaanga na vichwa.
 
Aisee Kongosho kumbe na wewe unaijua hiyo menyu................ yaani hapa pilipili imekolea kwenye chanchandu mpaka nimepata vijimafua....!
 
Naijua sana menu hiyo

pilipili ya rojo rojo, tena walikuwa wanasukumia na vikarangizo vingine kama mihogo ya kukaanga au viazi.

Aisee Kongosho kumbe na wewe unaijua hiyo menyu................ yaani hapa pilipili imekolea kwenye chanchandu mpaka nimepata vijimafua....!
 
Yeah..........hapa kuna mihogo ya kukaanga pia wanaita chipsi dume
 
Mtambuzi hayo machachandu kwa ujumla wake ukiyataja kwa mpiga tarumbeta au mpuliza filimbi ndiyo hatopiga tena kwakua domo lazima limjae mate!
 
Erickb52......... hiyo menyu nakumbuka wakati ule nikikaa Mwananyamala Kwa Mama Zakaria jirani kabisa na Kwa Ali Manjunju pale makaburini karibu na ule mbuyu usiozeeka kulikuwa na Mpemba mmoja alikuwa ni mtengeneza chachandu na urojo usipime mzee ..................Mihogo na Vihepe ndiyo ilikuwa mwake.................
 
Last edited by a moderator:

Hahahahahaaaa Dar kuna vyakula vya ajabu ila vitamu sanaaaaaaa
Dah huwa nakumbuka sana wakati nakaa Tazara na Kigamboni mitaa yangu ilikuwa pale Feri na Buguruni....
Mh Dar pako juu na napamiss sana aisee
 
ha ha ha Mtambuzi kiboko. Enjoy mwaya while it lasts.
Juzi nimesikia kuna vitu vinaitwa viwowowo ( sijui hata nitafsirije) lakini vinaliwa. Viwowowo vya kuku. Huko Mbagala /Kijichi. Sh.200.
Kama niliwaelewa watoa mada, ni vile vinavyobeba , ashakum, kinyeo cha kuku, ambacho kwa kawaida, huwa tunavinyofoa na kutupa. Sasa nasikia ni vitamu balaa vikikaangwa na utumbo wa kuku.
Ama kweli, najisi yako ni halali yangu.
 
Back
Top Bottom