Kauri mbiu ya miaka 50 iwe TUMEJARIBU, TUMESHINDWA TUJIPANGE UPYA

Invarbrass

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
504
111
Naona matatizo tuliyonayo sasa baada ya miaka 50 ya uhuru hayaendani na kauri mbiu ya kushehekea maadhimisho ya miaka 50 inayo sema tumedhubutu, tumeweza tusonge mbele. Kwakuwa tunarudi nyuma katika mambo mengi badala ya kusonga mbele (umeme mabwawa kukauka badala ya kuongeza mapya, nk.) Kauri mbiu yetu ingekuwa; TUMEJARIBU, TUMESHINDWA TUJIPANGE UPYA. Toa maoni yako.
 
Hilo nalo neno 7bu maisha ya waTZ tunayoishi leo tungetakiwa kuwa nayo mwaka 1981 yaani miaka 20 baada ya uhuru na sio 50 na hii inatokana na ulevi wa waTZ kuking'ang'ania chama kimoja pamoja na chama hicho kuwa wezi matapeli na kila sifa mbaya ni yao
 
umeniacha njia panda,naomba maana ya neno kauri
na kama hujui kiswahili usipost upupu wako hapa
 
Naona matatizo tuliyonayo sasa baada ya miaka 50 ya uhuru hayaendani na kauri mbiu ya kushehekea maadhimisho ya miaka 50 inayo sema tumedhubutu, tumeweza tusonge mbele. Kwakuwa tunarudi nyuma katika mambo mengi badala ya kusonga mbele (umeme mabwawa kukauka badala ya kuongeza mapya, nk.) Kauri mbiu yetu ingekuwa; TUMEJARIBU, TUMESHINDWA TUJIPANGE UPYA. Toa maoni yako.

Kauli mbiu na sio kauri mbiu
 
Kauli mbiu yako kwa mbaaaali naona kaukweli ndani yake, ingawa sina hakika na hiyo kesho yetu.

Ila tujipe moyo tu.
 
kukubali kushindwa ndio uungwana.
Pia kuanza upya sio ujinga.
Tukisema tumejaribu, tumewe tunasonga mbele tutakuwa tukijidanganya.
Maendeleo gani baada ya miaka 50 ya uhuru hamna umeme wa uhakika, huduma za afya ni duni, maji ni msamiati mgumu vijijini na mijini pia?
 
Naona matatizo tuliyonayo sasa baada ya miaka 50 ya uhuru hayaendani na kauri mbiu ya kushehekea maadhimisho ya miaka 50 inayo sema tumedhubutu, tumeweza tusonge mbele. Kwakuwa tunarudi nyuma katika mambo mengi badala ya kusonga mbele (umeme mabwawa kukauka badala ya kuongeza mapya, nk.) Kauri mbiu yetu ingekuwa; TUMEJARIBU, TUMESHINDWA TUJIPANGE UPYA. Toa maoni yako.
No comment !
 
Kweli hii kauli mbiu inawalakini.Ila sishangai sana kwa sababu ni hulka ya serikali hii ya Jk kuleta kauli mbiu ambazo badae zinamsuta yeye na serilkali yake.Nadahani huwa anazitoa kwenye maongezi yake na mafisadi wenzake kwa sababu ukiingalia kwa upande wa ufisadi wametimiza yaliyo mengi na wanasonga mbele.
Kama wamefanikiwa hata kushinda kesi na Tanesco inatakiwa iilipe Dowans bil 94 kwa nini wasijigambe wamethubutu wameweza na wanasonga mbele.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom