Kaunda alipomwita Kikwete "bwanamdogo toka Tanzania" mazishi ya Mandela Afrika Kusini

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,883
tanzania.jpg Keneth Kaunda anapomwita Kikwete bwanamdogo Kenneth-Kaunda.jpg

Rais Kikwete afichua siri kuhusu Mandela


  • Kaunda pia alisababisha watu kuangua kicheko pale alipomwita Kikwete kuwa "bwana mdogo" wakati alipokuwa akianza mazungumzo yake. "Waheshimiwa marais, akiwamo huyo bwana mdogo kutoka Tanzania……," alisema Kaunda.

Rais Jakaya Kikwete jana aliyateka mazishi ya Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, alipotoa salamu mbele ya maelfu ya waombolezaji na wageni wa kimataifa walioshiriki katika mazishi hayo. Rais Kikwete aliweka bayana jinsi Tanzania ilivyoshiriki katika vita ya ukombozi si kwa Afrika Kusini pekee bali kwa nchi nyingi za Kusini mwa Afrika zikiwamo Angola, Msumbiji, Zimbabwe na Namibia.

Kadhalika alizungumzia jinsi wapigania uhuru wa ANC walivyoweka kambi zao na kufungua ofisi za chama hicho nchini Tanzania ambako walipewa makazi na vifaa, maelezo ambayo yalishangiliwa na umati wa watu uliohudhuria. "Kwa hakika ANC walipata makazi mapya Tanzania ambayo waliyatumia kuendesha mambo yao, kujipanga na kuendeleza vita ya ukombozi. Kutoka Tanzania ANC waliweza kuwafikia makada wake na wanachama waliobaki Afrika Kusini kwa kutumia mawasiliano ya siri," alisema Kikwete na kuongeza: "Kimsingi Serikali ya Tanzania ililazimika kuanzisha redio maalumu kwa ajili ya vita ya ukombozi ambayo ANC waliitumia kupaza sauti ambazo walikuwa wamenyimwa na utawala wa ubaguzi wa rangi."

Rais Kikwete aliyekuwa na kazi ya kumwelezea Mandela kama mpigania uhuru, alieleza jinsi Mandela alivyofika Tanzania Januari 1962 bila kuwa na hati ya kusafiria na kwamba katika mazungumzo yake na Hayati Mwalimu Nyerere alieleza mpango wa kudai uhuru kwa njia ya mapambano. "Mwalimu Nyerere alikuwa na maoni tofauti kuhusu mpango wa kuendesha mapambano kwa kutumia silaha, lakini baadaye walikubaliana na Tanzania ilikubali kuanzishwa kwa kundi hilo na mwalimu (Nyerere) aliwapa sehemu ya kuendeshea shughuli zao na vifaa," alisema Kikwete na kuongeza: "Kwa hiyo, kwa wale walioshiriki katika vita vya ukombozi na askari wa MK (Jeshi la ANC), majina kama Kongwa, Mgagao, Mazimbu na Dakawa hayawezi kuwa mageni na pengine mtakumbuka enzi zile maisha yalivyokuwa."

Kikwete alisema wakati akiwa Tanzania, Mandela alikuwa akiishi kwa aliyekuwa Kada wa TANU, Marehemu Nsilo Swai na kwamba baada ya kusaidiwa kupata nyaraka za kusafiria kwenda Nigeria, Morocco na Ethiopia, aliacha buti zake nyumbani kwa mzee huyo. "Familia hii iliendelea kutunza buti hizo wakitaraji kwamba Mandela atarudi, lakini wakati anatoka katika safari yake hakupita tena Tanzania na kwa bahati mbaya alipofika Afrika Kusini alikamatwa na kufungwa," alisema Kikwete katika hotuba iliyorushwa na vituo vyote vya televisheni vya kimataifa.

Aliongeza: "1995 ikiwa mwaka mmoja tangu Mzee Mandela aingie madarakani, viatu vile vililetwa na mjane wa marehemu Swai, Vicky Nsilo Swai ambaye nimekuja naye leo ili ashirikiane nanyi katika msiba huu ninyi mlio ndugu zake." Alisema vita ya ukombozi haikuwa rahisi kwani wakati mwingine Tanzania mbali na kuwasaidia wapigania uhuru hati za kusafiria, ililazimika pia kuwapa majina ya bandia ili waweze kutekeleza majukumu yao vizuri.

Alimtania Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki akimuuliza iwapo alirejesha hati yake ya kusafiria na kusababisha waombolezaji kuangua kicheko. "Sifahamu kama Thabo amerejesha ya kwake," alisema. Alisema kwa kuzingatia mazingira hayo, uhusiano baina ya Tanzani na Afrika Kusini si wa bahati mbaya kwani umejengwa katika mizizi ambayo ilistawishwa na Hayati Mwalimu Nyerere na Mzee Mandela. "Huzuni yenu, ni huzuni yetu na majonzi yenu ni majonzi yetu pia maana kama alivyo kwenu Mandela kwetu alikuwa kiongozi, baba na mfano wa kuigwa," alisema Rais Kikwete huku akimtambulisha Mama Maria Nyerere katika ibada hiyo.
Alisema baada ya kutoka gerezani, Mandela alifika Tanzania ambako alipokewa na umati mkubwa wa watu katika rekodi ambayo haijawahi kuvunjwa na ujio wa kiongozi mwingine yoyote. Katika hatua nyingine, Rais mstaafu wa Zambia, Kenneth Kaunda jana aliuchekesha umati wa waombolezaji pale alipokwenda kwa kukimbia wakati alipoitwa jukwaani kwa ajili ya kutoa shukrani.

Kaunda pia alisababisha watu kuangua kicheko pale alipomwita Kikwete kuwa "bwana mdogo" wakati alipokuwa akianza mazungumzo yake. "Waheshimiwa marais, akiwamo huyo bwana mdogo kutoka Tanzania……," alisema Kaunda.

Hisani ya Mwananchi Publication
 
Mambo yake ya kutokuwa serious na mambo ya nchi yake yanamfanya aonekane mdogo amshukuru Nyerere jana ameonekana dunia bila Nyerere asingepanda pale.
 
Kaunda kumwita Kikwete kuwa ni "Young President from Tanzania"...kuna jambo...
 
Kaunda kumwita Kikwete kuwa ni "Young President from Tanzania"...kuna jambo...

acheni ushabiki jamani ni lugha ya kawaida tu kwa mtu mzima kama yeye wala hakuwa na ajenda yoyote kwa kumwita jk bwana mdogo
Halafu mbona hili jambo limekuwa gumzo hapa mjini ? kunanini nyuma ya pazia?
 
Nakumbuka alisema....''....young man from Tanzania...'''

Kifalsafa kauli hiyo ina maana kubwa ikitoka kwa mtu mkubwa na mzoefu kwa masuala ya utawala na kimataifa, kisiasa, kiuchumi hali kadhalika kiutamaduni. Mpaka nilete mada hii kwa sababu ya kauli hiyo ni kitu kilichonifikirisha kutolewa kwa nafasi ile na kwa lugha ile. Pengine tunachukulia mambo kirahisi mno na kutoa tafsiri nyepesi isivyo stahili.
 
acheni ushabiki jamani ni lugha ya kawaida tu kwa mtu mzima kama yeye wala hakuwa na ajenda yoyote kwa kumwita jk bwana mdogo
Halafu mbona hili jambo limekuwa gumzo hapa mjini ? kunanini nyuma ya pazia?

Anayejua nyuma ya Pazia ni Kaunda tu...Kumbuka hata yule MC baada ya kuleta za kuleta kwa Kaunda, akamwita "Young MC"
 
Kaunda kumwita Kikwete kuwa ni "Young President from Tanzania"...kuna jambo...

He was young, He is still young, he will remain young...hii ni kashfa, i bet alikuwa anachekacheka kama kadawia yake
 
Prezdaaa Kawanyima baadhi ya watu usingizi jana......C'mon guys chuki ni ugonjwa!!

P.S.......My president is young......Forever Young!

XoXo.....
 
Back
Top Bottom