Kaulimbiu za Kijeshi/Kijasusi Duniani zinazotia Hamasa Katika kupambana na Ugumu wa Maisha na changamoto zake...

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,701
1: "WHO DARES WINS"
"ANAYETHUBUTU HUSHINDA"

Hii ni kauli au Motto wa kikosi maalumu cha makomando wa jeshi la Israel (IDF) "SAYERET MATKAL". Hawa jamaa ni hatari sana. kwa motto huu wanaingia hadi moyoni mwa nchi ya adui.
Miongoni mwa watu ambao walifanya kazi kubwa ktk kikosi hicho hatari ni aliyewahi kuwa PM wa Israel EHUD Barak. Kauli hii hutumiwa na makomando wa uingereza SAS pia.

Binafsi kauli hii, nikiichanganya kwenye mishemishe zangu za maisha hunipa ujasiri kufanya mambo mengi kwa uthubutu.

2:The Only Easy Day Was Yesterday", "It Pays to be a Winner"
Siku rahisi pekee ilikuwa ni jana, ' Inalipa kuwa mshindi'

Huu ni MOTTO wa kikosi hatari chenye weredi wajuu wa kijeshi cha Marekani "NAVY SEAL".
Kauli hii huondoa uzembe wa kulala ukidhani jana ulichoka sana.

3:S'engager pour la vie
" To enlist for life"
'Kujisajili kwa Maisha '

Huu ni motto wa shirika la kijasusi la Ufaransa lenye weledi uliotukuka. Unanifundisha kuna vitu ambavyo ukijisajili ni kwa maisha yote au vitaathili maisha yako yote. Maamuzi kama KUOA. Ukikosea kuoa umekosea maisha wengi husema hivyo. Uamuzi ambao wengine tumejisajili kwa maisha yote ni kukubali kuwa Wafuasi wa Yesu Kristo. Hakuna kurudi nyuma.

4:Facta Non Verba,
'Deeds not words'
"Matendo sio Maneno"

Hii ni kaulimbiu ya Kikosi maalumu ya kijeshi cha Kanada JTFT. Kuna mambo katika maisha yanahitaji Matendo sio maneno. Na matokeo yake hupimwa kwa namba sio stori.
Mfano, Umesoma vitabu vingapi mwaka huu, au umepanda miti mingapi mwaka huu, hakuna porojo jibu ni namba sio sentensi.

5:Facit Omnia Voluntas
The Will is Decisive
Nia Inamaamuzi.

Hakuna kitu kibaya kama mtu kutokuwa na maamuzi. Maamuzi ambayo yanatoka katika NIA yako, sio Mazingira na misukumo ya jamii. Hapa napo kutoka kwenye kaulimbiu ya kikosi hiki cha makomando wa kijerumani " Kommando Spezialkräfte" au KSK.


zitaendelea...
karibu kwa Muendelezo....
 
Back
Top Bottom