Kauli za wana ACT-Wazalendo: Zitto ni zigo zito lisilobebeka

kibokomchapaji

Senior Member
Aug 18, 2017
165
307
*Anaandika Msema Kweli*...

Watanzania wengi wamekua wakimbeba Zitto Kabwe kwa kusikiliza hoja zake zisizokua na mashiko.

Leo hii amewashangaza wanaomuunga mkono baada ya kumsifu Rais Magufuli kuwa amewekeza kwenye vitu.

Swadakta!!! Amewekeza kwenye vitu ili vitumiwe na watu ambao ni Watanzania wote.

"Hivi anaenufaika na barabara, madaraja, treni ya kisasa, umeme vijijini ni nyani au watu???" anahoji Humudi Kombo mwanachama wa ACT

"Sisi hatutaki azungumze mazuri ya serikali, ametukera japo hafahamu" anaeleza

Kiukweli, uwekezaji katika watu upo wa njia mbili; kuwekeza moja kwa moja kama kutoa elimu bure *au* kuwekeza katika vitu ambavyo vitatumiwa na watu.

Hicho kilimo anachozungumzia Zitto haoni kuwa kuna benki ya kilimo, bima za kilimo na kadhalika???

Tatizo la Zitto ni kujifanya anajua kila kitu Jambo ambalo haliwezekani.

Huo ndio ukweli mtupu ambao anapaswa kuufahamu.
 
Maendeleo ya vitu sio watu
na
Maendeleo ya watu bila vitu.

Hapo sijui itakaa vipi hakuna maendeleo ya watu bila vitu pia hakuna maendeleo vitu bila watu.. haya maneo ya wana siasa ni mikorogo korogo mengine
 
Back
Top Bottom