Kauli za viongozi wa Tanzania zenye utata!

Madikteta wa kweli wanafanya mambo makubwa sana kwa nchi zao ingaweje wanakuwa na mambo ambayo yanakera sehemu fulani ya jamii...rejea dikteta wa Kuwait (mkulu alisema hvo)...dikteta wa Libya....dikteta wa Singapore...na wengineo....nimejaribu tu kutaja wachache....huyu wa kwetu ni dikteta.........(rejea kauli ya Lissu)....naogopa kuzingirwa mie..
Kwa mtazamo huo kwa Tanzania yetu ilipofikia basi ni heri kuwa na kiongozi wa hivyo, maana watu walikua wanazoa sio kuchota, wewe fikiria makontena ya udongo wa madini yanasafirishwa bila hatua yoyote kuchukuliwa, tulizidi kuwa shamba la bibi
 
Uhuru tulionao ni haki ya kikatiba hakuna yeyote
mwenye ruhusa kwa mfano kutaka kuvithibiti vyama vya upinzani ndani na nje ya Bunge. Hili la kudhibiti vyama vya upinzani ni kwenda kinyume na katiba. Na katiba ya nchi inapokiukwa ni dalili za udikteta na hatujui huko siku za usoni ni kiasi gani cha haki za Watanzania zitaendelea kukiukwa nchini. Wewe unaweza kuona wanachojadili wengine ambacho wewe hukubaliani nacho ni ujinga. Kitu ambacho hakina ukweli wowote.

Kwa mtazamo wangu nadhani chini ya utawala wa JPM tumesikia na kuona mengi sana na naamini tutapata mengi jambo ambalo lilikuwa ni vigumu sana kulisikia kuliona kwa kiongozi wetu aliyestaafu juzi tu. Bila watu kupenye Bunge ndipo ije kama hoja na kuundiwa kamati. Sasa kulinganisha hili na commedian nadhani ni kutokuwa na nidhamu pia uhuru uliopitiliza. Halafu mtu anathubutu kuandika huu ujinga na kuadai kuwa Rais ni Dikteta, mimi nadhani uhuru tulionao tusibweteke sn dikteta wa kweli hata hii nafasi ya kujadili tu huwezi kupata. Nawasilisha
 
Mnashindwa kumuelewa JPM...akiongea hivyo hamaanishi kutojua, anazungumza kwa kadri mnavyojua nyie Watz.
Hata wakati wa kura ya maoni kuhusu kuanzishwa kwa vyama vingi nchi 80% walisema wanataka chama kimoja Na 20% walisema vyama vingi....mwl nyerere akasema hawa 20% wana impact kubwa kuliko hao 80% ...alimaanisha hao 80% walikuwa ni bendera fuata upepo....hata sasa mnaomuelewa na kushadadia kauli tata za mh ndo hao hao 80% ila 20% bado wanahoji kauli tata za mkulu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwanza hakuna mtu aliyekuambia you believe in one man show. Hizi ni inferiority complex zako tu zinazokufanya udhani someone is telling you that you believe in one man show. You can believe in anything suits your mind.

If that is the case, kafanye ujambazi halafu umsubiri Rais Magufuli aje kukukamata kwa sababu ni one man show na hakuna system.

Unatuambia unataka change in system halafu hapo hapo unasema he is one man show. Huoni kama kwa angalizo lako tayari system imebadilika labda uniambie hata kwenye Awamu ya nne ilikuwa pia one man show.

Kile anachokifanya Rais unaweza kukiweka katika taswira yako kwa jinsi unavyopenda kulingana na mtazamo wako.

Fikra zako zinaweza kukutuma kama anachokifanya ni comedy au dancing. Huo ni mtazamo wako na haki yako.

Nani amekuambia Rais is unsure kwa kile alichokuwa anakisema?

Rais ametumia maneno yenye tamathali za semi halafu wewe unatuambia ni comedy.

Unasema tutakapogundua Rais ni Dikteta? Umejuaje kama hatujagundua?

Hizi ndo kachumbali za changudoaz wa sisiem hasa.
 
Kwa mtazamo huo kwa Tanzania yetu ilipofikia basi ni heri kuwa na kiongozi wa hivyo, maana watu walikua wanazoa sio kuchota, wewe fikiria makontena ya udongo wa madini yanasafirishwa bila hatua yoyote kuchukuliwa, tulizidi kuwa shamba la bibi

Mkuu wangu Huyu wa kwetu hafanyi kama hao niliowataja Mkuu..
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Umeandika vizuri sana kuhusu uwepo wa vyama vingi nchini na kauli ya Baba wa Taifa ambaye kama si yeye labda tungekuwa bado ni nchi ya chama kimoja.

Hata wakati wa kura ya maoni kuhusu kuanzishwa kwa vyama vingi nchi 80% walisema wanataka chama kimoja Na 20% walisema vyama vingi....mwl nyerere akasema hawa 20% wana impact kubwa kuliko hao 80% ...alimaanisha hao 80% walikuwa ni bendera fuata upepo....hata sasa mnaomuelewa na kushadadia kauli tata za mh ndo hao hao 80% ila 20% bado wanahoji kauli tata za mkulu
 
Lol! hakukuwa na haraka yoyote ya kukurupuka kama hakuwa na hakika na alichoongea. Inaonyesha ni jinsi gani asivyo mtu wa kufuatilia details kwa makini, vinginevyo huku ni kukurupuka kwa kiwango cha juu kabisa.

Ukiniuliza naona "URAHISI" sasa hii unaonekana ni mrahisi kuliko kuimba
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Madikteta wa kweli wanafanya mambo makubwa sana kwa nchi zao ingaweje wanakuwa na mambo ambayo yanakera sehemu fulani ya jamii...rejea dikteta wa Kuwait (mkulu alisema hvo)...dikteta wa Libya....dikteta wa Singapore...na wengineo....nimejaribu tu kutaja wachache....huyu wa kwetu ni dikteta.........(rejea kauli ya Lissu)....naogopa kuzingirwa mie..

Madikteta uliowataja speech zao karibu zote zilikuwa za kuwapa wananchi moyo na matumaini. Huku kwetu hotuba haijakamilika bila kutaja wizi na ubovu wa watendaji wa serikali, mambo ambayo si mageni masikioni mwa Watanzania. Madikteta wa ukweli waliwaadabisha waliokwenda kinyume na sera zao kimya kimya. Hawakufanya matangazo. Zama zimebadilika mbinu za waliopita haziwezi kutumika karne hii.

Ingekuwa bora zaidi Kama raisi angetumia mamlaka yake kikatiba na vyombo vilivyopo kisheria kudeal na Wabadhirifu. Watanzania tumechoka kusikia watu walivyo jichotea chao mapema. Watanzania tunataka kusikia hatua zilizochukuliwa na si kingine. Tunataka kusikia kesi ziko mahakamani, watu wamefungwa miaka ya kutosha, mali zao zimetaifishwa kama watapatikana na hatia.

Hainiingii akilini wapinzani wawataje wabadhirifu kwenye majukwaa na kiongozi mwenye mamlaka ya juu kabisa afanye hivyo hivyo.
 
Huyo anaejiita BAK na huyo anaejiita Pasco huwa ni wagumu sana kuelewa aka vichwamaji.

Kwa uelewa wangu, Magufuli simply alikuwa anaelezea mlolongo na si tukio moja. Huyu 20, yule 60, yule 40.

Inapaswa mfahamu kuwa Magufuli Kiswahili si lugha mama kwake ni lugha ya kujifundisha pengine alipoanza shule kama ilivyo kwa wengi wenu.
Tena kama wewe ndo muongo balaa,kwa hiyo usipojua kiswahili ndo unakuwa unahisi hisi tu???acheni kumfanya raisi hamnazo bhana,kila kitu mnampigia makofi hata kama kakosea
 
I believe in "better be sure than sorry!", kuna haaka gani?!. Hilo la milioni 7 au 8 kwa dakika, japo ni kweli, ila limegeuka kichekesho!, kama rais anaweza kusema vitu ambavyo haviaminiki, then nani wa kuaminika?!.

Milioni 7 au 8 kwa dakika ni shocking!, watu wameingia shock, mwisho wa siku hata bilioni 100 !, hazijafiki watu wikihesabia ni matrilioni!. Hizi mimi naziita ni comedy!, comedy awaachie ma comediana kina Masanja, with inf at his finger tips, we expect hard facts na sio gues work ya sijui hivi, sijui vile!, hizo ni zetu huku jf na sio pale mahali patakatifu!, urais ni taasisi ya presidential, sasa mtu anapokuwa president, hata kama mwanzo haukuwa presidential material, unapaswa kuivaa hiyo taasisi ya presidential na kubadilika kuwa presidential material!, sisi ma conservatives kiukweli tunatatizwa na hizi kauli za paying "lip services", nyingine ndio hizi sasa zinakuja kugeuka ze comedy!.

Pasco
bottom line.....rais wetu ashauriwe kutumia prepared speech. free styling bado sana and I fear someday atakuja tamka kitu kinachoweza kutikisa ile misingi (cornerstones) inayotuweka pamoja kama Watanzania.

nakumbuka BMW >90% ya speech zake alikuwa akisoma - there was nothing bad at all with that.
 
Back
Top Bottom