Kauli za viongozi mbalimbali kuhusu mwanafunzi atakayepata mimba

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,276
6,584
SERIKALI.....


SERIKALI I
"Serikali imeweka dira itakayowawezesha wasichana kuendelea na masomo baada ya kujifungua huku wale waliowapa mimba, wakishughulikiwa kikamilifu." Paulina Mkonongo, Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari, Wizara ya Elimu - 01 Disemba 2015.
_______________________________

SERIKALI II
"Serikali imeamua kuwa wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa shuleni wasifukuzwe, bali waendelee na masomo." Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, akiwa Chuo kikuu kishiriki cha UDSM cha Elimu (DUCE), 27 Aprili 2017.
________________________________

SERIKALI III
"Serikali inaelekeza Wasichana wanaojifungua warudi na kuendelea na masomo shuleni." Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (06 June 2017- Gazeti la The Citzen).
________________________________

SERIKALI IV
"Katika kipindi changu cha utawala, mwanafunzi yeyote wa kike (shule ya msingi na sekondari) akipata mimba ni marufuku kurudi shuleni. Siwezi fanya kazi ya kusomesha wazazi." Rais John Pombe Magufuli, 22 Juni 2017, Bagamoyo - Pwani.
________________________________

 
Hayaa!Unasema hauwasomeshi? Kwani hela unatoa wewe au ni kodi za wananchi? Uongozi wako una mwisho. Hata Samuel Doe aliondoka. Jerry Rawlings aliondoka. Hitler, unamfahamu Hitler? Aliondoka. Sembuse wewe! Uta - go!! ! ! !
Pilipili mbuzi haha
 
Like tangazo la mtoto w shule aliebakwa akapata mimba halafu akarudishwa shule na baba yake ndo basi tena
 
Mnatumia nguvu kubwa sana kutetea hili jambo.....As if mwanafunzi kuacha ngono ni jambo lisilo epukika.....Nguvu hizi zitumieni kuwahamasisha watoto wenu na dada zenu wasijihusishe na ngono hali ni wanafunzi
hujielewi wewe, naomba usome vizuri uzi, ni maamuzi tofauti ya viongozi wa ngazi za juu kabisa wa serikali kuhusu mwanafunzi aliyepata mimba. Serikali moja maelekezo tofauti! Je tutafika?
 
Magufuli yupo sahihi hii pia itasaidia kujenga nidhamu ya wanafunzi na kupunguza ngono zembe na kubwa zaidi itaondoa upendeleo kama wanamfunga mwanaume (let's say school boy) Miaka 30 kwa kumpa mimba mwanafunzi (mwenzie) ili iwe fundisho kwa mamii,je adhabu kwa mwanafunzi wa kike ni ipi sasa!?
 
hujielewi wewe, naomba usome vizuri uzi, ni maamuzi tofauti ya viongozi wa ngazi za juu kabisa wa serikali kuhusu mwanafunzi aliyepata mimba. Serikali moja maelekezo tofauti! Je tutafika?
Wewe ndiye usiyejielewa maana unashindwa kusoma alama za nyakati.....Awamu hii maelekezo hutolewa na Mkuu tu...Hao wengine huwa wanatania tu
 
Tutaonekana wajinga tukikaa na kutetea ujinga kisa tu ni haki ya mtu.
Wazazi twatakiwa kuwafundisha watoto wetu na kuwaelewesha nini wafanye na nini wasifanye na madhara ya kile wanachokifanya.
wanafunzi na watoto wetu tuwafundishe kumcha Mungu maana ndiye chanzo cha maarifa

Tofauti na hapo twatafutana ubaya bure
 
Back
Top Bottom