Kauli za "Serikali inakopa mwananchi alipe deni" ni kauli za kichochezi

mjarrab

Senior Member
Nov 13, 2015
108
55
Kume kuwa na kauli kutoka kwa baadhi ya wanasiasi kulitumia suala la mikopo na Madeni ya nchi kinyume na Uhalisia!.

Serekali ipo Madarakani kwa niaba ya wananchi. Hivyo Jambo lolote ambalo linafanywa na Serekali hufanywa kwa niaba ya wananchi walio ipa ridhaa kuwaongoza.

Serekali inapo chukua Mikopo kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Maendeleo,Mkusudiwa wa kunufaika na miradi hiyo ni Mwananchi,

Mfano: Nchi imechukua mkopo kwa ajili ya kukamilisha mradi wa SGR ili kuiunganisha nchi kwa mtandao wa reli ya kisasa na nchi za Jirani zikiwemo,Rwanda,burundi,Kongo n k.

Kukamilika kwa Reli hii kutafungua fursa za kiuchumi kwa nchi kuongeza mapato kwa sababu Bandari yetu itatumika kupokea Mizigo mingi ya nchi Jirani na Reli yetu itatumika kusafirisha mizigo hiyo kwa haraka na kufanya uchumi wa nchi kuongezeka kwa haraka!.

Pato la nchi linapo ongezeka ndipo huduma za Serekali kwa wananchi wake zinapo ongezeka na uwezo wa Serekali kulipa madeni unaongezeka.

Na mwananchi kunufaika na huduma za zinazo tolewa na Serekali ndipo kunako leta maana ya kufaidika kupitia mipango ya Serekali iliyo Madarakani kwa niaba yao.

Sasa utakuta watu Wanazungumza kwamba Serekali inakopa halafu mzigo wa kulipa deni hilo unakuwa ni wa wananchi.!
KAULI hii si sahihi kabisa!.

Kwa sababu kauli Kama hii inaonyesha kana kwamba mwananchi analipa deni ambalo hanufaiki nalo.jambo ambalo si kweli.!

Mkopo umechukuliwa na Serekali kwa niaba ya wananchi ili ufanyike mradi utakao wanufaisha wananchi.

kwa maana hiyo tunaweza kusema wananchi wanaofaidika na mradi uliopatikana kwa mkopo ndio wanao paswa kulipa deni ili waendelee kufaidika na mradi huo .!

Lakini kusema tu kwamba Wananchi wanabebeshwa mzigo wa kulipa madeni kana kwamba hawapati huduma inayo tokana na mkopo huo. inakuwa ni kutoitendea haki serekali iliyowekwa kwa niaba ya wananchi.!.

SEREKALI IMEKOPA KUKAMILISHA MRADI WA SGR Maana yake= Wananchi wamekopa ili wapate mradi wa SGR wanufaike na pato la reli hiyo na wanufaike na fursa zitakazo jitokeza kupitia reli hiyo.

Baada ya Mradi kukamilika:
SEREKALI INALIPA MKOPO WA SGR Maaana yake= Wananchi wanalipa deni la mkopo wa mradi wa SGR ambao umekamilika na wanafaidika kwa Pato la taifa(huduma mbali mbali zinazo changiwa na mradi huo) wanafaidika kwa fursa zinazotokana na uwepo wa mradi huo.
 
Sawa mkuu ila tozo zipunguzwe zaidi na ajira zitolewe.
Tozo zitapungua kwa kuwepo na vyanzo vingine vipya vya mapato!.
SGR ikikamilika itakuwa ni chanzo kipya cha mapato.
Hivyo tegemea tozo kupungua !
 
Vipi mtazamo wako juu ya wanaosema CCM inawenyewe na wenyewe ndio wanagawana vyeo.
Hebu toa muelekeo chanya ndugu mwana jukwaa
 
Sio kila linalofanywa na serikali basi ni Kwa niaba ya wananchi!
Walileta tozo wananchi tukapinga mpaka wakaenda kupunguza!Huo ni mfano mmojawapo kwamba hata serikali hukosea na inapaswa kukosolewa!
Tuache hii tabia ya kutaka kuaminisha watu kuwa kila linalofanywa na serikali ni sahihi!
Karne hii tunakopa Kwa ajili ya kujenga madarasa???
Miradi ya maendeleo ni sawa kukopa,ila hadi madarasa??
 
Mtazamo wangu haupo juu ya watu watu wanasema nini!
Bali upo kwa kile kinachoonekana kwa macho!
Naangalia SGR Dar to Moro imekamilika kwa zaidi ya asilimi 90. Moro to Makutupora zaidi ya asilia 77 na kazi inaendelea!
Sijaona hao Wana CCM wanavyo faidika Nje wa wajibu wao kisheria!
 
Kume kuwa na kauli kutoka kwa baadhi ya wanasiasi kulitumia suala la mikopo na Madeni ya nchi kinyume na Uhalisia!.
Serekali ipo Madarakani kwa niaba ya wananchi .Hivyo Jambo lolote ambalo linafanywa na Serekali hufanywa kwa niaba ya wananchi walio ipa ridhaa kuwaongoza.
Serekali inapo chukua Mikopo kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Maendeleo,Mkusudiwa wa kunufaika na miradi hiyo ni Mwananchi,

Mfano:Nchi imechukua mkopo kwa ajili ya kukamilisha mradi wa SGR ili kuiunganisha nchi kwa mtandao wa reli ya kisasa na nchi za Jirani zikiwemo,Rwanda,burundi,Kongo n k.
Kukamilika kwa Reli hii kutafungua fursa za kiuchumi kwa nchi kuongeza mapato kwa sababu Bandari yetu itatumika kupokea Mizigo mingi ya nchi Jirani na Reli yetu itatumika kusafirisha mizigo hiyo kwa haraka na kufanya uchumi wa nchi kuongezeka kwa haraka!.
Pato la nchi linapo ongezeka ndipo huduma za Serekali kwa wananchi wake zinapo ongezeka na uwezo wa Serekali kulipa madeni unaongezeka.

Na mwananchi kunufaika na huduma za zinazo tolewa na Serekali ndipo kunako leta maana ya kufaidika kupitia mipango ya Serekali iliyo Madarakani kwa niaba yao.
Sasa utakuta watu Wanazungumza kwamba Serekali inakopa halafu mzigo wa kulipa deni hilo unakuwa ni wa wananchi.!
KAULI hii si sahihi kabisa!.
Kwa sababu kauli Kama hii inaonyesha kana kwamba mwananchi analipa deni ambalo hanufaiki nalo.jambo ambalo si kweli.!
Mkopo umechukuliwa na Serekali kwa niaba ya wananchi ili ufanyike mradi utakao wanufaisha wananchi.
kwa maana hiyo tunaweza kusema wananchi wanaofaidika na mradi uliopatikana kwa mkopo ndio wanao paswa kulipa deni ili waendelee kufaidika na mradi huo .!
Lakini kusema tu kwamba Wananchi wanabebeshwa mzigo wa kulipa madeni kana kwamba hawapati huduma inayo tokana na mkopo huo. inakuwa ni kutoitendea haki serekali iliyowekwa kwa niaba ya wananchi.!.

SEREKALI IMEKOPA KUKAMILISHA MRADI WA SGR Maana yake= Wananchi wamekopa ili wapate mradi wa SGR wanufaike na pato la reli hiyo na wanufaike na fursa zitakazo jitokeza kupitia reli hiyo.

Baada ya Mradi kukamilika:
SEREKALI INALIPA MKOPO WA SGR Maaana yake= Wananchi wanalipa deni la mkopo wa mradi wa SGR ambao umekamilika na wanafaidika kwa Pato la taifa(huduma mbali mbali zinazo changiwa na mradi huo) wanafaidika kwa fursa zinazotokana na uwepo wa mradi huo.
ila lazima ukweli tusema....!! angalie ile video ya gwaji boy kuhusu yale maneno aliyotamka aliyekuwa spika....! kwamba mkopo utapelekea hii nchi kuuzwa" sasa ebu fanya tathmin halafuburudi tena kwenye bandiko lako kutupa mrejesho kama ni kweli mikopo ya serikali hii inatija maana tusiwe tunashabikia vitu ambavyo mbele tutakwenda kukwama....gwaj boy anakwambia mpaka mwenda zake anakufa deni la taifa lilikuwa trilion 56 sasa ngalia awamu hii tangu ichukue nchi deni limefika trilion 70 yaan ndani ya miezi 6 lime shot kwa trilion 14 sasa uyo mtu akikaa miaka 10 si itakuwa hatar? ukaangalia gharama za maisha zinazid kupanda
 
Sio kila linalofanywa na serikali basi ni Kwa niaba ya wananchi!
Walileta tozo wananchi tukapinga mpaka wakaenda kupunguza!Huo ni mfano mmojawapo kwamba hata serikali hukosea na inapaswa kukosolewa!
Tuache hii tabia ya kutaka kuaminisha watu kuwa kila linalofanywa na serikali ni sahihi!
Karne hii tunakopa Kwa ajili ya kujenga madarasa???
Miradi ya maendeleo ni sawa kukopa,ila hadi madarasa??
Hukatazwi kupinga lisilo kuwa sawa!.
Jifunze kuwa na mtazamo sahihi kwa kila Jambo!
Jiulize mahitajio ya Madarasa kwa sasa!
Je! Ni kiasi gani kimetumika kujenga madarasa?.
Je! Kiasi hicho cha fedha kilichotumika ! Uko tayari huduma zingine zisimama ili madarasa yajengwe?.
 
Ndugai alitakiwa aseme Yale maneno akiwa bungeni kwenye mamlaka yake.
Sio vichochoroni hapo ndipo alipomuudhi Samia .ni Kama anamteta wakati LAO MOJA
ila lazima ukweli tusema....!! angalie ile video ya gwaji boy kuhusu yale maneno aliyotamka aliyekuwa spika....! kwamba mkopo utapelekea hii nchi kuuzwa" sasa ebu fanya tathmin halafuburudi tena kwenye bandiko lako kutupa mrejesho kama ni kweli mikopo ya serikali hii inatija maana tusiwe tunashabikia vitu ambavyo mbele tutakwenda kukwama....gwaj boy anakwambia mpaka mwenda zake anakufa deni la taifa lilikuwa trilion 56 sasa ngalia awamu hii tangu ichukue nchi deni limefika trilion 70 yaan ndani ya miezi 6 lime shot kwa trilion 14 sasa uyo mtu akikaa miaka 10 si itakuwa hatar? ukaangalia gharama za maisha zinazid kupanda
 
Ndugai alitakiwa aseme Yale maneno akiwa bungeni kwenye mamlaka yake.
Sio vichochoroni hapo ndipo alipomuudhi Samia .ni Kama anamteta wakati LAO MOJA
Unaongozwa na video za wanasiasa unacha kuanglia vinavyoonekana kwa Macho.
Madarasa 15,000 na Madawati unayoaona kwa macho.
Vifaa vya maabara unaviona kwa macho!
Mkataba wa kumalizia ujenzi wa SGR umesainiwa unauona kwa macho.
Hizo trilioni za kwenye video hiyo unatakiwa wewe uzitolee maelezo!
 
Hukatazwi kupinga lisilo kuwa sawa!.
Jifunze kuwa na mtazamo sahihi kwa kila Jambo!
Jiulize mahitajio ya Madarasa kwa sasa!
Je! Ni kiasi gani kimetumika kujenga madarasa?.
Je! Kiasi hicho cha fedha kilichotumika ! Uko tayari huduma zingine zisimama ili madarasa yajengwe?.
Ndio kukosa focus Kwa watunga sera wa nchi,hivi inakuwaje ghafla tu tunakuwa na uhitaji Huo wa madarasa?Ndio hapo tunapokosoa,kungekuwa na Mpango endelevu Wala isingetokea tukawa na uhitaji wa madarasa 10,000 Kwa mpigo!!!
Wakati Huo Huo tunajisifu tuna Hela tunaenda kununua ndege Kwa cash amabazo nazo zinazalisha hasara!
Sijui unaelewa hoja yangu?Taifa likikosa focus ndio hapo mambo tunafanya kiholela tu!
 
Kama taifa tunayo mahitajio mengi!.
Kupanga ni kuchagua ! Tamaza usahihi wa uchaguzi wa Mambo muhimu na uyaunge mkono!.
Yale ambayo hayana umuhimu wa haraka unayo haki ya kuyakosoa!.
Lakini jifunze kupima kila Jambo kwa Uhalisia wake.
 
Ujumbe huu uliondika nadhani ukiufanyia kazi wewe mwenyewe basi utaona tutakuwa kwenye ukurasa mmoja!
Lazima tuwe na sera bora za muda mrefu!Ni aibu kukopa Kwa ajili ya madarasa,hatuwezi jitosheleza na Pato la ndani kwenye mambo kama hayo halafu miradi ya maendeleo ambayo itakuja kuzalisha faida ndio tukakopa kuitekeleza!
Huu ukopaji holela sio afya Kwa nchi!Nilikuwa namsikiliza mzee mmoja,ni mchambuzi wa masuala ya uchumi!Akasema tusikazanie kwamba deni ni himilivu,tusipoangalia tutakopa Leo kiasi kwamba tukawanyima watoto wetu wa kesho hiyo fursa ya kukopa!Akiwa na maana tusipoangalia tunaweza tukakopa halafu Marais wajao wakashindwa kufanya maendeleo Kwa mzigo wa madeni watakaokuwa wameachiwa!
 
Back
Top Bottom