Kauli za Rais zanisababishia ugonjwa wa moyo... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli za Rais zanisababishia ugonjwa wa moyo...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ufunguo, Oct 27, 2012.

 1. Ufunguo

  Ufunguo JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi Rais anaposema,

  And,
  Mimi mlalahoi sipati picha.

  Au anasema kwamba sasa rushwa inazidi kuota mizizi na muda si mrefu hata watoto wetu wataanza kuomba rushwa?, maana baba tayari, mama naye tayari, Kijana nae kama baba, kama mama. Kwa hiyo kwa hesabu zile za kale kama A=B=C =D then D=A=B=C.
  Au anataka kusema kwamba taasisi zilizopo za kupambana na rushwa zimeshindwa kazi na kama ndo hivyo kwanini zinaendelea kuwepo?, kwani madaraka aliyonayo kazi yake ni nini?

  Halafu anaposema mkichagua asiyefaa mtaendelea kuwa naye huyohuyo hadi mwaka 2017 maana yake ninii?. Anataka kusema hata kama mtu ni kilaza kwasababu tu amechaguliwa ndani ya CCM ataendelea kuongoza hadi uchaguzi mwingine ufanyike?. Au ansema mfumo wa uongozi ndani ya chama ni mbovu kiasi kwamba haiwezekani kumwajibishwa mwenye makosa?.

  Napata kizungumkuti, sielewi hata Madaraka ya Rais yako wapi.

  Naomba ushauri.
   
 2. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Logic yako hapo kwenye red ina makosa, inatakiwa kuwa A=B=C =D then B=D=A=C
   
 3. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Huyu rais alishawahi kusema ana majina ya wala rushwa na wauza madawa ya kulevya kwa hiyo anawapa muda wajirekebishe, sijui walishajirekebisha. Au yale majina yaliandikwa kwenye toilet paper na ameshaitumia msalani so amesahau.

  Anaetegemea rais aliyeingia madarakani kwa rushwa na wizi wa EPA akemee rushwa amepotea.
   
 4. Ufunguo

  Ufunguo JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimekuelewa mkuu, nashukuru kwa kuiweka vizuri na nahisi ujumbe umekamilika.
   
 5. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  si mnaona sharia za nchi hii zilivyo, mliambiwa ubya na udhaifu ya ccm na yeye mwenyewe mwaka 2010 mkabisha na kushindwa kulinda kura sasa si hao wanaelekea 2015 huku nchi ikifilisika!!!??
   
 6. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #6
  Oct 27, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,955
  Likes Received: 6,717
  Trophy Points: 280
  This is very true, inajulikana wazi kuwa 2005, JK aliingia madarakani kwa pesa za EPA-KAGODA,ambazo zilibwa benki kuu, kiasi cha shilingi bilioni 40. Inaeleweka wazi pia mastermind wa wizi huo alikuwa Rostam na Lowasa, ndiyo maana kundi la Lowasa linagawa pesa waziwazi mbele ya vijana wa TAKUKURU, lakini kwa maelekezo ya mkulu, watu hao hawaguswi hata kidogo. Hivi sasa ndiyo tutaanza kukumbuka maneno ya hekima sana ya mwalimu Nyerere, aliposema, Ikulu hakuna biashara, sasa inapotokea mtu anatumia mabilioni ya pesa kwenda Ikulu, lazima tujiulize, kama hizo ni pesa zake, zitarudi vipi, kama amekopeshwa, atazilipaje? Kwa hali tunayoiona nchi hii kwa namna rushwa inavyotembea kwenye chaguzi za CCM, ni vyema tukakumbuka wosia wa mwalimu aliposema anayekimbilia Ikulu kwa kuhonga wapiga kura, ni wa kumwogopa kama ukoma!!
   
 7. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Nikisema kiongozi wetu ni mnafiki au ni mwongo au ni mbabaishaji nitakosea?

  Mnafiki: Kama aliwajua halafu anajifanya hawajui!

  Muongo: Ahadi kibao ambazo hazijatekelezwa, (yes natambua muda wake haujaisha) lakini dalili za utekelezaji hazipo!

  Mbabaishaji: Kushindwa kuwachukulia hatua wala rushwa(ambao alikuwa nao katika ile orodha), AKIOMBA wajirekebishe/kuwapatia muda! ..Mbona walalahoi huwa hawapewi muda hata kama wakijulikana?

  Sasa Mr. President anaposema hadi 2017, ni "katiba mpya" aliyoipitisha mwenyewe kuwa Presidential terms ni miaka miwili miwili(2015- 2017).
   
 8. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mbona hata watoto walishaanza kula rushwa!!! hebu tembelea pale mlimani [UDSM] kaseme unataka room katika hostel uone madalali wa rushwa!! pitia chaguzi za serikali za wanafunzi uone wanavyoshindana kutoa rushwa!! halafu hao hao ndo wanaingia makazini baada ya kuhitimu inafikiri rushwa itaisha?
   
Loading...