Kauli za Rais zanisababishia ugonjwa wa moyo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli za Rais zanisababishia ugonjwa wa moyo.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ufunguo, Oct 27, 2012.

 1. Ufunguo

  Ufunguo JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi Rais anaposema,
  "Nawaambieni, mkifanya mchezo ipo siku mtakuja kujuta maana mkishamchagua kiongozi asiyefaa, mtalazimika kuwa naye huyohuyo hadi 2017, na kama Waswahili wanavyosema majuto ni mjukuu," (Mwananchi, Octoba 27, 2012)
  And,
  "siku zilizopita vitendo vya rushwa vilikuwa vikihusishwa zaidi na wanaume, lakini sasa hata makundi ya kina mama nao wameanza kujihusisha na rushwa (Mwananchi, Oct 27, 2012).
  Mimi mlalahoi sipati picha.
  Au anasema kwamba sasa rushwa inazidi kuota mizizi na muda si mrefu hata watoto wetu wataanza kuomba rushwa?, maana baba tayari, mama naye tayari, Kijana nae kama baba, kama mama. Kwa hiyo kwa hesabu zile za kale kama A=B=C =D then B=C=D=?.
  Au anataka kusema kwamba taasisi zilizopo za kupambana na rushwa zimeshindwa kazi na kama ndo hivyo kwanini zinaendelea kuwepo?, kwani madaraka aliyonayo kazi yake ni nini?
  Halafu anaposema mkichagua asiyefaa mtaendelea kuwa naye huyohuyo hadi mwaka 2017 maana yake ninii?. Anataka kusema hata kama mtu ni kilaza kwasababu tu amechaguliwa ndani ya CCM ataendelea kuongoza hadi uchaguzi mwingine ufanyike?. Au ansema mfumo wa uongozi ndani ya chama ni mbovu kiasi kwamba haiwezekani kumwajibishwa mwenye makosa?.

  Napata kizungumkuti, sielewi hata Madaraka ya Rais yako wapi,
  Naomba ushauri.
   
 2. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ushauri wa nini? tulimchagua kiongozi asiyefaa na tunalazimika kuwa naye hadi 2015. liwalo na liwe
   
 3. Jagarld

  Jagarld JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 1,531
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Kashatimiza ndoto yake"URAIS"mengine mnamsumbua mwacheni rais wetu sikivu amalizie kipindi chake kwa amani!
   
 4. C

  Cool C Member

  #4
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 26, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tuwe wavumilivu jamani.. dhiki inaposhamiri maana yake faraja imekaribia! historia ina sifa ya kujirudia, na sijakata tamaa kuwa ipo siku itajirudia kwetu tanzania kupata raisi aina ya nyerere tena. hofu yangu ni kwamba kihistoria kama ilivyotokeaga kwa mwalimu, mapambano lazima!!
   
 5. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mie hata huwa simsikiliz.....
   
 6. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mheshimiwa JK, tayari tunajuta..maana tulikuchagua wewe 2010 na sasa tunajuta maana tunalazimika kua na wewe hadi 2015 na ni kweli majuto ni mjukuu
   
 7. K

  KANGILE New Member

  #7
  Oct 27, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hana uwezo wa kufanya zaidi ya hapo
   
 8. F

  Fenb Member

  #8
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 18, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  No Comment.
   
Loading...