Kauli za rais wa Tanzania na mtetezi wa wanyonge Dkt. Magufuli leo mkoa wa Manyara

Akijenga ukuta halafu kesho Tanzanite ikagunduliwa nje kidogo ya ukuta itakuwaje? Atavunja ukuta ili ausogeze au atajenga mpya?

Anajuaje wapi kuna Tanzanite na wapi hakuna Tanzanite?

Ukuta wa kuzinga kwenye Tanzanite na miundombinu ya kuzuia wachimbaji wasifukiwe machimboni, kipi muhimu?
Nimecheka sana sana aiseeeee, Tanzanite unaijengea Ukuta?? Kwanza kwa bajeti ipi? Halafu wakichimba chini kwa chini? Hahahahhaaahahaaaaa naogopa mfuko wa sandarusi
 
Nimecheka sana sana aiseeeee, Tanzanite unaijengea Ukuta?? Kwanza kwa bajeti ipi? Halafu wakichimba chini kwa chini? Hahahahhaaahahaaaaa naogopa mfuko wa sandarusi
Ni zile zile jitihada zao kutoa majibu mepesi dhaifu kwa maswali magumu muhimu katika kutafuta sifa rahisi za wajinga.
 
hakuna kitu huwa nachukia huyu mtu kuitwa mtetezi wa wanyonge, kwasababu wanyonge nchi hii ndio wanaoumia zaidi kwenye utawala wake. mnavyozidi kumpamba kwa mgongo wa chupa ndivyo mnavozidisha hasira kwa wananchi kwa 2020.

Kuna mijitu nafikri ilisharogwaa kwa maji ya benderza za kijani. Sijui wanaposema ni mtetezi wa WANYONGE ni wanyonge gani hasa waliolengwa...??? Ndugu zake akina Bashite anaowakingia kifuana kuwatetea kwa nguvu zote kila kukicha???Hawa wanaovunjiwa nyumba zao, wale waliofukuzwa kazi bila kupewa mafao yao kisa vyeti fake au Darasa la saba, Wale waliodhulumiwa fedha ya misaada ya Tetemeoko Kagera, wale wanaopigwa risasi kama kina TL na wanaopotezwa na katika mazingira ya kutatanisha au kusweka ndani kila siku na kufunguliwa kesi zisizokuwa na kichwa wala miguu wao si wanyonge..!!
Yawezekana tafsiri na maana ya neno MNYONGE kwa Rais Magufuli ni wale ambao hawako UPINZANI..........!!! Ukiwa mpinzani tu wewe siyo mnyonge hivo usitegemee msaada wowote kutoka Serikali ya Magufuli...!!!
 
Jamaa anajua kucheza na akili za wabongo na anafanikiwa kweli! Maneno debe vitendo kisoda... Kutawala nchi za kibashite ni rahisi sana
 
hakuna kitu huwa nachukia huyu mtu kuitwa mtetezi wa wanyonge, kwasababu wanyonge nchi hii ndio wanaoumia zaidi kwenye utawala wake. mnavyozidi kumpamba kwa mgongo wa chupa ndivyo mnavozidisha hasira kwa wananchi kwa 2020.
Mtetezi wa wanyonge asingeruhusu wanyonge wavunjiwe nyumba walizojenga kwa machozi, jasho na damu. Licha ya kuwa na court order kuzuia uvunjaji huo wa nyumba.

Magufuli muongomuongo tu.
 
Mwaka wa pili huu sasa kauli ni zilezile "copy and paste" eg tumeibiwa sana.....majizi yaondoke......mshahara haujapunguzwa lakini maisha magumu...... Hizi sio kauli za kujenga. Walioweka kwenye sheria kwamba annual increment ni lazima walikuwa na maana yao kwamba bei ya sukari au sembe au shati July 2016 haiwezi kuwa sawa na ya July 2017. Awe anasema "mshahara haujapunguzwa wala haujaongezwa".
 
Mwaka wa pili huu sasa kauli ni zilezile "copy and paste" eg tumeibiwa sana.....majizi yaondoke......mshahara haujapunguzwa lakini maisha magumu...... Hizi sio kauli za kujenga. Walioweka kwenye sheria kwamba annual increment ni lazima walikuwa na maana yao kwamba bei ya sukari au sembe au shati July 2016 haiwezi kuwa sawa na ya July 2017. Awe anasema "mshahara haujapunguzwa wala haujaongezwa".
 
Katika hii vita ya uchumi, watatugombanisha, na sisi tukikubali kugombana wataendelea kutuibia. Ni vyema tushikamane sana.

Ukiona kazi huwezi, acha uondoke, kuna watanzania wengi sana wanaotamani kufanya hiyo kazi.

Mtu analalamika maisha magumu, lakini mshahara wake haujapunguzwa ni ule ule. Basi hapo unajua kulikuwa na namna ya ziada.

Wengine wakisimama na kusema pesa zimepotea, sitawashangaa kwa sababu walizoea kuiba pesa zisizo zao, na kweli zimepotea.

Najua hamna hata ambulance, hiyo nitawaletea mimi. Nitakwenda kuwa katakata huko, nitapata ambulance itakuja.

Hii barabara watapita watu wote wa vyama vyote. Hata majizi wa Tanzanite, watapita barabara hii.

Najua kuna wawekezaji wameanza kuondoka, na wengine wameshaondoka kwa sababu walichokuwa wanakifanya hakikuwa sahihi.

Tanzania tunataka wawekezaji, lakini kama anadhani anakuja kutuibia, kwa sasa hawezi. Tumeweka mikakati kudhibiti mali zetu

Soko la madini ya Tanzanite liwe hapa hapa Simanjiro lisiwe Arusha. Wanunuaji waje hapa, wakae hapa, wale hapa hapa.

Kwa sababu Mungu hakukosea kuweka Tanzanite Tanzania, basi ni lazima tuitumie kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wetu.

Hapa patafungwa kamera za ulinzi, kutakuwa na mlango mmoja tu, na hata mtu akimeza Tanzanite itaonekana. Tumechoka kuibiwa.

naagiza JWTZ kupitia Suma JKT kujenga ukuta eneo la Block A-D ambalo ndilo lenye madini mengi ya Tanzanite, na kufunga kamera
Manyara mkoani Arusha
 
JPM ni chuma,hakuna kurudi nyuma na ukitaka kujua mafisadi yameshindwa pabaya angalia ambavyo wanarukuruka kama bisi zinazokaangwa.
 
Maisha ni magumu ata km mshahara upo vilevile, bidhaa zimepanda sn bei kwahiyo Purchasing power imepungua ndo maana watu tunalalamika maisha magumu
 
mi nasubiria milioni 50 kijijini kwetu
magufuli katoa hiyo ahadi asilimia mia inatekelezeka kabisa,sema hiyo ahadi ni jiwe takatifu kwa upinzani sababu alisema atatoa ndani ya awamu yake ya kwanza hakusema mwanzoni au mwishoni ila itatoka awamu hii hii.nasema itakuwa jiwe cos watu watapewa wakati tunajongea na kukaribia msimu wa 2020 ndipo wananchi watapokea hizo 50 na magu again huyu hapa.watu watasema hongo yeye atasema ahadi yangu,tunza haya maandishi tutakutana 2020.kama huamini hizo 50 zipo unajidanganya mkuu issue ni mipango tu watoe muda gani ila zipo,ni pesa ndogo sana kwa serikali.
 
Mimi sio ccm lkn huyu mzee anauchungu na nchi hii atii.
Lkn inaonekana kuna watu wapo nyuma yake wanatumia gharama yoyote ile ili asifanikiwe.
Mzee Magu kaza buti.
Nia ya Magufuli in fact ni njema sana katika kulinda rasilimali za taifa.Sema tatizo ni kwamba amejiongezea mzigo mwingine kwa kukimbizana na Wapinzani wake kitendo ambacho kinamfanya aonekane kwa wengi wa watanzania kuwa anabinya Demokrasia ambayo hata Katiba ya nchi inatambua uhalali wa Wapinzani na vyama vya Upinzani.
 
Mimi sio ccm lkn huyu mzee anauchungu na nchi hii atii.
Lkn inaonekana kuna watu wapo nyuma yake wanatumia gharama yoyote ile ili asifanikiwe.
Mzee Magu kaza buti.
Kwa ni ukimsapoti ni lazima uwe CCM? Mbona raia wasio na vyama ndio wengi! Huna haja ya kuanza na mimi sio CCM kwa sababu kuwa CCM sio dhambi
 
Back
Top Bottom